Search This Blog
Monday, 26 September 2016
Umuhimu wa vikoba kwa wananchi wa kipato cha chini
UTANGULIZI
Takribani miaka 23 sasa tunashuhudia ukuaji mkubwa wa huduma za kifedha na
mifumo mbalimbali ikiibuliwa na kuainishwa kwa wanajamii mbalimbali hasa walio
katika kipato cha chini na cha kati. Japo mifumo ya kifedha imekuwa ikiongezeka
vado taratibu na mifumo ya upatikanaji wa huduma hiyo kwa watu wengi wa kipato
cha chini imekuwa ni tatizo hasa kutokana na msharti magumu.
Masharti magumu ya upatikanaji wa huduma ya kifedha yanawafanya watanzania
wengi kutonufaika na huduma za kifedha na matokeo yake kundi kubwa la watu
wenye kipato cha chini kuendelea kuwa na umaskini uliokisiri. Masharti hayo ni pamoja
na riba kubwa, gharama za maombi ya mikopo, kitangulizi cha mkopo, salio kwenye
akaunti, dhamana isiyohamishika, kuapa mahakami na masharti mengine mengi.
Kuanzishwa kwa vikundi vya VICOBA kumesaidia wananchi mbalimbali wakiwemo
wenye kipato cha chini na cha kati waishio mijini na vijijini kuweza kunufaika na
huduma za kifedha pamoja na za kijamii. Huduma zimekuwa zikiongezeka siku hadi siku
kutokana na ukuaji wa mitaji ya kikundi na Viwango vya mikopo ndani ya vikundi.
Mwongozo huu utamsaidia mtumiaji kuelewa vizuri maumbile na taratibu za uendeshaji
wa vikundi vya VICOBA. Mwongozo huu umeandaliwa baada mfumo wa VICOBA
Tanzania kutimiza miaka kumi kuanzia mfumo huu uanzishwe mwaka 2002 na
utatumika kwa vikundi vyote vya VICOBA, IR-VICOBA, BENKIMANI na wadau
mbalimbali wanaendesha na kusimamia vikundi katika maeneo mbalimbali ndani na
nje ya nchi.
CHIMBUKO LA MFUMO
Mfumo wa VICOBA ulianzishwa mwaka 2002 kwa mara ya kwanza na shirika la
Intereligious Council for Peace of Tanzania (IRCP) na kwa kipindi hicho shirika
likijulikana kama World Conference on Religion for Peace (WCRP). Shirika la IRCP
lilianzisha mfumo huu kwa mara ya kwanza kama mpango wa majaribio eneo la
Ukonga mazizini wilaya ya Ilala Mkoa wa Dar es salaam na wilaya ya Kisarawe mkoa
wa pwani ambapo vikundi vilianzishwa katika maeneo ya Kisarawe, Masaki, Sungwi na
Kifuru.
Shirika liliamua kufanya majaribio haya katika eneo la Ukonga na kisarawe ili kubaini
umadhubuti wa VICOBA kati ya maeneo ya mjini na maeneo ya vijini. Mwaka 2006
IRCP walifanya tathimini na matokeo yalionyesha mfumo unafanya vizuri lakini Ukonga
ilifanya vizuri zaidi kwa sababu ya mzunguko wa biashara za wanakikundi na mzunguko
wa fedha wa Ukonga ulikuwa mkubwa ukilinganisha na kisarawe.
6
UTEKELEZAJI WA MRADI WA MAJARIBIO
Katika utekelezaji wa mradi huu kwa upande wa Ukonga IRCPT waliingia ubia na
UYACODE na kwa upande wa kisarawe waliingia ubia na KIYODENI. Dhumuni kubwa la
kuingia ubia na taasisi hizi lilikuwa ni kuufanya mradi kuwa imara na endelevu na hasa
mradi utakapo kwisha muda wake. Taasisi hizi zilishirikiana na IRCPT katika uhamasishaji
ngazi ya jamii na maeneo ya taasisi hizi yalitumiwa na vikundi kukutanika na kufanya
shughuli zao.
Mfumo ulifanyiwa maboresho mbalimbali kulingana na mazingira ya kitanzania na
kuufanya kuwa endelevu zaidi. Maboresho yaliyofanyika baada ya kuanzishwa na
IRCPT ni pamoja na kuanzishwa kwa mfuko wa Bima, kushauri Viwango vya Ziada ya
mikopo, vikundi kutovunja mzunguko kila mwaka kwa kugawana kila kitu badala yake
kugawana faida tu kila mwisho wa mwaka, mfumo wa urejeshaji wa mikopo, muda wa
urejeshaji wa mikopo, idadi ya hisa kuongezeka kutoka hisa moja hadi hisa tano na
uboreshaji mfumo wa utunzaji wa kumbukumbu.
Maboresho hayo yameufanya mfumo huu kuwa imara, na endelevu na kuweza
kuonyesha mafanikio makubwa na ambayo hayakutarajiwa. Mafanikio haya ni
pamoja na ukuaji wa Viwango vya mikopo, ukuaji wa uelewa wa uwekezaji na
nidhamu ya urejeshaji wa mikopo. Wanachama wa vikundi wameweza kuboresha
biashara, kujenga nyumba, kupanua miradi, kusomesha watoto na wengine
wameweza kulipia huduma ya bima ya afya (CHF) na ni jambo ambalo halikuwepo
kabla ya kujiunga kwenye vikundi vya VICOBA.
Mafanikio haya yamechangiwa sana na mafunzo ya kina ya uendeshaji na usimamiaji
wa vikundi vya VICOBA ,ushirikiano wa wanakikundi, sheria za kikundi, uwajibikaji wa
viongozi, uwazi katika uendeshaji wa shughuli za kikundi, utunzaji wa kumbukumbu,
ufuatiliaji wa wawezeshaji na uwajibikaji wa kila mwanachama katika shughuli za
kikundi.
MADHUMU YA KUANZISHWA KWA MFUMO WA VICOBA
VICOBA ni Benki Jamii Vijijini na kwa kingereza ni Village Community Banks.
VICOBA ni mpango wa kujenga uwezo wa ki-uchumi na ki-jamii kwa kutumia rasilimali
za wananchi zinazowazunguka. Mfumo huu huwawezesha wananchi kujiunga katika
vikundi na kuanzisha mfuko wa kukopeshana kwa ajili ya miradi ya kuingiza kipato na
kutatua matatizo ya dharura yanayowakabili hasa matatizo yanayohusu elimu na
afya. Mifuko hii hujengwa kwa njia ya kununua hisa na kuchangia mfuko wa jamii kila
wiki.
7
Mradi huu ulipoanzishwa na IRCPT ulijulikana kama mradi wa Mtoto Nuru VICOBA
ukiwa na malengo ya kuleta matumaini kwa vijana, wanawake na makundi
yaliyotengwa kwa njia ya kuwekeza na kupata mitaji ya kuendeleza na kuanzisha
miradi/biashara mbalimbali ili kupambana na umaskini, kusaidia watoto yatima na
watu waishio na Virusi vya Ukimwi.
MATOKEO YA TATHIMINI.
IRCPT mwaka 2006 walifanya tathimini ambayo ilionyesha mfumo wa VICOBA ni mfumo
imara, rahisi na endelevu hasa katika kukusanya rasilimali za wananchi na usimamizi
wake. Mfumo huu ulionyesha jinsi unavyojiendesha kwa uwazi hasa katika kufanya
maamuzi na taratibu za uendeshaji ambazo hufanywa kila wiki kwenye kikao kinacho
hudhuriwa na wanachama wote. Tofauti na mifumo mingine mfumo wa VICOBA
maamuzi hutolewa na wajumbe wote kwenye mkutano wa kikundi na viongozi wakiwa
na majukumu ya kusimamia na kutekeleza.
Vikundi 10 vilivyo anzishwa Ukonga na kisarawe mwaka 2002 vilikutwa vikiwa hai na
imara. Mitaji ya vikundi ilikuwa imeongezeka, wanavikundi wapya walikuwa
wamejiunga katika nafasi zilizo achwa wazi. Mikopo ilikuwa imekua, mfumo wa
urejeshaji ulikuwa mzuri na mikopo yote ilikuwa ina lipwa kwa wakati.
Mradi ulionekana endelevu na imara japo kuwa vikundi hivi viliachwa muda mrefu bila
kupata msaada wa karibu kutoka IRCPT kutokana na sababu mbalimbali. Katika
tathimini hii pia vikundi vyote vilionyesha wazi wanavikundi waanzilishi walikuwa
wamefanikiwa na wanavikundi wapya walikuwa wanaonja Mafanikio.
Idadi ya wanakikundi katika kila kikundi walikuwa ni 30 na hii ikionyesha walikuwa
wanajiunga mara tu inapobainika kunawajumbe wamehama au kujitoa. Jamii
ilionyesha kufurahishwa na manufaa na mabadiliko wanayoyapata wanakikundi wa
VICOBA ukilinganisha na mifumo ya mingine.
Wanawake walionekana wengi katika vikundi hivi na ambao walikuwa zaidi ya asilimia
sabini na tano (75%) ya wanakikundi wote na hii ilijionyesha wazi katika vikundi vya
VICOBA suala la jinsia lilikuwa siyo kikwazo. Miongoni mwa wanakikundi hawa ni
pamoja na wafanya biashara, wakulima wa bustani, na wafanya kazi.
Baada ya mafanikio haya taasisi mbalimbali za kidini, kiserikali na zisizo za kiserikali
zimeweza kuanzisha mfumo huu katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi na ni
mfumo ambao unauwezo wa kuwa na maingiliano na shughuli nyingine.
8
WADAU WANAOTEKELEZA MFUMO VICOBA TANZANIA
Kwa miaka mingi sasa wadau mbalimbali wanahamashisha vikundi katika maeneo
mbalimbali na miongoni mwa wadau hao ni pamoja na TEC, CCT, BAKWATA, AEE,
Pathfinder International, AFRICARE, LAMP, LIWODET, MEPP, RUMAKI, Social Economic
Development Initiative of Tanzania, SELL, VDSA, WWF, ORGUT, FLORESTA, ELCT(ND, ECD,
Mbulu) TCRS, TANARELA, AXIOUS Foundation, WCST, ITECCO, Frankfurt Zoological
Society, UYACODE, YWCA, EFG na wengine wengi. Maeneo mbalimbali ya Tanzania
yameweza kufikiwa japo siyo wadau wote wanatekeleza mfumo huu kama inavyo
takiwa.
UMADHUBUTI WA VICOBA
1.3.1. Uanzishaji wa kikundi cha VICOBA hauhitaji mtaji. Makusanyo ya kila wiki
yanayotolewa na wanakikundi ndiyo huanzisha mfuko wa kukopesha.
1.3.2. Vikundi huanzishwa karibu na maeneo ya wanachama wanayoishi hivyo
hupunguza gharama ya nauli na matumizi mabaya ya muda.
1.3.3. Mikopo ya VICOBA haina ukiritimba kama fedha zipo, maana wanakikundi
wanajua mwenendo mzima wa fedha za kikundi kwa sababu shughuli zote za
kikikundi hufanywa mbele ya wanakikundi wote.
1.3.4. Kupitia mfumo huu wanakikundi wanatumia mikutano ya kikundi kama sehemu
ya kujifunza mambo mengine kama vile elimu ya biashara, masuala ya kisheria,
ukatili wa kijinsia, jinsi ya kuhudumia watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi,
kuelimishana haki za kila mtu na mambo mengine ambayo wanakikundi
wanaona ni muhimu kwao kuyajadili na kujifunza.
1.3.5. Mfumo wa utunzaji wa kumbukumbu ni rahisi ambao unawawezesha
wanakikundi kusimamia kumbukumbu zao za fedha bila kuhitaji elimu ya juu ya
utunzaji wa fedha.
1.3.6. Ziada ya mikopo inayopatikana hutolewa mgao kwa wanakikundi wote mwisho
wa mwaka kwa njia ya mgao na kila mwanakikundi hupata faida kutokana na
idadi ya hisa zake.
MAPUNGUFU YA VICOBA
1.3.7. Viwango vya mikopo vinavyotolewa wakati kikundi kinapo anzishwa vinakuwa
vidogo. Mikopo inaanza kutolewa katika kikundi baada ya kumaliza wiki nne za
kuwekeza fedha.
1.3.8. Mikopo kutopatikana kwa wakati kama wanakikundi wasipo rejesha kwa wakati.
1.3.9. Mfumo wa VICOBA kutotambulika kisheria na kutokuwa na sera za uendeshaji
kama mifumo mingine mfano Saccos na taasisi zingine za fedha.
9
1.3.10. Vikundi kutokupata mafunzo sahihi ya uendeshaji wa mfumo wa VICOBA hivyo
vikundi kutoendeshwa kama inavyotakiwa.
1.3.11. Wawezeshaji wachache na baadhi ya watu kufundisha vikundi bila ya kupata
mafunzo ya kina.
TOFAUTI KATI YA VICOBA NA MIFUMO MINGINE
VICOBA TAASISI NYINGINE ZA KIFEDHA
Vikundi ni mali ya wanakikundi wenyewe Vikundi ni mali ya mashirika husika
Mali za kikundi ni mali za wanakikundi
wenyewe
Mali za kikundi huwa chini ya
mhamasishaji/mwenye taasisi husika
Maamuzi ya kikundi yanafanywa na
wanakikundi wote wakiwa pamoja
Maamuzi ya kikundi yanafanywa na
wanakikundi wachache (Viongozi).
Wanakikundi hujenga mifuko
yakukopeshana kwa kutegemea fedha
zao wenyewe.
Hutegemea sana misaada na michango
kutoka kwa wahisani mbalimbali.
Huanzishwa kutokana na malengo
maalumu.
Ziada ya mkopo ni mali ya wanakikundi
wa kikundi husika na wanagawana
mwisho wa mwaka.
Riba ni mali ya taasisi husika kwa ajili ya
kuendesha shughuli za taasisi husika
Riba hupangwa na wanakikundi wa
kikundi husika
Riba hupangwa na taasisi husika
10
SEHEMU YA KWANZA
KUANZISHA NA KUKUA KWA VIKUNDI VYA VICOBA
Lengo:
• Taratibu za kuunda kikundi
• Kuonyesha vifaa vinavyo tumika
• Kuelewa taratibu za uwekaji na uchukuaji wa mikopo
• Kujibu maswali na kuondoa hofu
Muda: Dakika 45
Vifaa:
• Bango kitita
• Marker pen
• Flipchart stand
Mbinu za kufundishia:
• Kuwasilisha mada
• Majadiliano
• Maswali na majibu.
• Mifano
MADA YA KWANZA: MKUTANO WA UHAMASISHAJI KWA WANAJAMII
MAELEZO YA MWEZESHAJI
Mkutano huu ni mkutano wa awali kwa wanajamii husika ambao wanataka kuelewa
au wanashauku ya kuujua mfumo wa VICOBA kwa undani. Mkutano huu unashauriwa
uendeshwe na watu wenye ufahamu wa kina wa mfumo wa VICOBA.
Mhamasishaji ni vyema kujitayarisha vizuri kwenye mikutano hiyo na vyema pia
kujiepusha na ahadi ambazo hazitatekelezeka na ambazo zipo nje ya uwezo wake.
Mara nyingi washiriki hupenda kumwambia mwezeshaji wamesikia na kuufahamu
ujumbe na hutaka kujua mhamasishaji atawapa nini? Mwezeshaji afafanue kuwa
hatawapa fedha zozote bali atatoa mafunzo kama atakuwa na uwezo huo na kama
hatakuwa nao vikundi vitawajibika kumgharamia mwezeshaji wakati wa ushauri wa
namna ya kuanzisha na kusimamia vikundi vitakavyo kuwa chini yake.
11
Katika mkutano huu mada zifuatazo zinatakiwa kufafanuliwa kwa undani:
• Nini maana ya VICOBA
• Jinsi mfumo wa VICOBA unavyofanya kazi
• Mifumo ya uwekaji wa fedha
• Taratibu za uwekaji wa fedha
• Taratibu za urejeshaji wa mikopo
• Tofauti kati ya mfumo wa VICOBA na mifumo mingine
Nini maana ya kikundi.
Kikundi ni ni kundi la watu waliokubaliana kukusanya rasilimali zao kwa pamoja ili
kufikia lengo walilo kusudia.
Umililiki wa Kikundi. Wanakikundi ndio wataendesha shughuli zote za kikundi kwa
kupitia mikutano ya kila wiki na mkutano mkuu. Wanakikundi watachagua kamati ya
uongozi na kuanzisha sheria za kikundi zitakazo waongoza. Mali zote za kikundi
zitaendelea kumilikiwa na wanakikundi wenyewe na nivyema wawezeshaji
wakajiepusha kuchukua fedha za kikundi kuzipeleka kwenye asasi nyingine au sehemu
yeyote bila ya kupata ushauri wa kina.
Muda wa kuweka fedha. Wanakikundi wataamua ni mara ngapi kwa mwezi watakuwa
wanakutana na taratibu za utoaji wa mikopo ya hisa na jamii. Ni vyema pia
kukubaliana matukio mbalimbali yanayo weza kuchangiwa na wanakikundi
ilikuepusha lawama na manughuniko. Hata hivyo inashauriwa vikundi kukutana kila wiki
ili kuongeza ukaribu na kusaidia kukua kwa mfuko wa kukopeshana kwa haraka.
Uzoefu unaonyesha ukuaji wa mfuko wa kikundi kinacho kutana kila wiki ni tofauti na
ukuaji wa kikundi kinacho kutana mara moja kwa mwezi maana uwezo wa
wanakikundi kuhifadhi fedha nyingi na kuziwasilisha kwenye kikundi inakuwa shida.
Kukutana kila wiki kunasaidia watu kulipa mikopo yao kwa wakati na kuufanya
mzunguko wa fedha ndani ya kikundi kuwa imara.
Dhana ya Riba. Dhana ya mikopo huleta mjadala wa riba ya mkopo, ambayo
inapingana na maadili ya Imani za kidini mbalimbali. Mwezeshaji ni vyema ajiandae na
atoe ufafanue wa kina na kueleza kwa uwazi tofauti kati ya Riba na Ziada ya mikopo
ambayo inatozwa na vikundi vya VICOBA.
Uanzishaji wa Kikundi. Baada ya mkutano huu washiriki watapewa nafasi ya kujadiliana
na kutoa maamuzi kama wapo tayari kuanzisha kikundi au bado wanafikiria. Kama
kutakuwa na walio tayari kuanzisha kikundi basi ni mwezeshaji atawasaidia kuanzisha
na kuwaongoza katika mambo ya msingi ya kukubaliana. Wajumbe walio tayari
watachagua viongozi wa muda, wataandaa sheria za muda, watakubaliana siku ya
kukutana, sehemu ya kukutana na jinsi ya kuchangia vifaa vya zoezi la kibenki.
12
MADA YA PILI: KUUNDWA KWA VIKUNDI
Mwezeshaji atawaomba washiriki mbao wamehudhuria kwenye mkutano wa
uhamasishaji na ambao wapo tayari kuanza kikundi kubaki na wale ambao wanao
kwenda kutafakari na familia zao watatakiwa kuondoka ilikuwapa uhuru walio baki
kupanga mambo yao.
Hatua ya kwanza katika uundaji wa kikundi ni kuundwa kwa vikundi vidogo vya watu
watano na ambao watatengeneza kundi kubwa la watu wasio pungua kumi na tano
na wasio zidi thelathini. Lengo vikundi vidogo vya watu watano ni kudhaminiana wakati
wa kukopa na endapo mjumbe kati yao atashindwa kurejesha mkopo kama kanuni na
taratibu zinavyo jieleza wadhamini watawajibika kulipia deni au kiasi kilicho salia.
Vikundi vinatakiwa kutoelemea upande wowote wa kisiasa au wa kidini kwa sababu
wanachama wake wanatakiwa kuwa mchanganyiko. Kuegemea kwa upande mmoja
kutasababisha wanachama wengine kujitoa au kupunguza hari ya watu. Mfumo wa
VICOBA haubagui jinsia ambapo wanawake na wanaume wanaruhusiwa kuwa
wanachama katika vikundi hivi na kupata haki zote zinazo stahili.
Mtu mwenye madeni mengi kwenye vikundi vingine haruhusiwa kujiunga katika
kikundi kwani anaweza kudhorotesha maendeleo ya kikundi kwa kukopa fedha na
kutozirejesha kwa wakati. Umeibuka pia mtindo wa vikundi kuwa na walezi na nijambo
ambalo limerudisha nyuma maendeleo ya vikundi na mfumo wa VICOBA. Jambo hili
nilazima liepukwe na wanakikundi maana fedha za kikundi ni mali ya wanachama na
hakuna umuhimu wa vikundi kuwa chini ya walezi. Uzoefu unaonyesha walezi wa
kikundi huingilia maamuzi ya kikundi na mwisho kudumaza maendeleo ya kikundi.
Viongozi wa vikundi hivi ni Mwenyekiti, Katibu, Mwekahazina na Wahesabu fedha
wawili. Iwapo kiongozi mmoja hajaudhuria katika mkutano nafasi yake itashikwa na
mwanakikundi yeyote atakayechaguliwa siku hiyo na kusimamia au kutekeleza
shughuli zote zinazohitajika kama utaratibu unavyoeleza. Kikundi kitakuwa na wajibu
wa kumtafuta mwezeshaji kusaidia kutatua tatizo au kupata ufafanuzi wa jambo fulani
ndani ya kikundi. Mwezeshaji ni vyema ashirikishwe mara kwa mara na ni vyema
akajiepusha na jambo lolote ambalo litaweza kuathiri fedha za wanachama na kama
kuna jambo litakuwa juu ya uwezo wake ni vyema na yeyé akaomba ushauri kwa
wataalam zaidi.
Watiaji saini kwenye hundi ya kikundi ni Katibu, Mweka hazina na mjumbe mmoja
ambaye ni mwanakikundi lakini siyo kiongozi na wanakikundi watampendekeza
kutokana na uadilifu na uaminifu wake katika jamii.
Mwezeshaji atawasaidia washiriki kuchagua uongozi wa muda, kuanzisha sheria za
muda, kukubaliana siku ya kukutana, sehemu ya kukutana na thamani ya Hisa pamoja
na mchango wa mfuko wa jamii. Majengo ya kisiasa au ya kidini yatatumika tu iwapo
13
wanakikundi wote watakubaliana na kuridhia na endapo baadhi ya wanachama
hawatakuwa tayari kutumia majengo hayo basi sehemu ya kukutana itatakiwa
kubadilishwa.
Mafanikio ya kikundi yanategemea sana jinsi wanachama wanavyojihusisha kikamilifu
katika kushiriki mikutano ya kila wiki na jinsi wanavyo zifuata sheria na kanuni walizo
jipangia. Mahudhurio ya wanakikundi yanasaidia kufanya mahesabu kuwa sahihi na
kupunguza minongono na malalamiko ya wajumbe wengine.
Vikundi vya VICOBA hutunga sheria zao za kujiongoza na vikundi hivi hujitegemea
vyenyewe. Kila kikundi huwa na sheria zake na sheria hizo hutoa mamlaka kwa
uongozi wa kikundi kuonyesha mwelekeo wa uendeshaji wa shughuli za kikundi. Kila
mshiriki hutakiwa kuzijua sheria zote za kikundi na kuzifuata ipasavyo.
Wajumbe wa kamati ya uongozi watachaguliwa kila baada ya mwaka mmoja na
wanaweza kuondolewa wakati wowote iwapo 2/3 ya wanakikundi wa tapiga kura ya
kuwaondoa na kuto kuwa na imani nao kutowajibika katika shughuli za kikundi
ipasavyo. Kila mwaka kati ya viongozi watano wawili au watatu watapumzika na nafasi
zao zitajazwa na wanachama wengine. Sababu za kupumishwa baadhi na baadhi
kuendelea ni kujengeana uwezo na uzoefu na kati ya wajumbe watako ondoka ni
lazima kati ya mwneyekiti, Katibu na mweka hazina mmoja aweze kupumzika. Mwaka
utakao fuata wale walio baki wataondoka na nafasi yao kujazwa na wajumbe wapya
watakao chaguliwa.
MADA YA TATU: AWAMU ZA KIKUNDI KUPITIA
Kuanzishwa kwa kikundi cha VICOBA hufuata awamu kuu nne ambazo ni awamu ya
uhamasishaji, awamu ya mafunzo ya kina, maendeleo na awamu ya kupevuka na
kukomaa kwa kikundi.
Japo awamu hizi nne zinatoa taswira ya jinsi kikundi cha VICOBA kinavyoweza kukua,
inawezekana kabisa kikundi kuamua kuingiza mfumo wa mafunzo mengine ya ziada
hata katika hatua ya Mwisho ya ukuaji.
Hatua za kuanzisha na kukua kwa kikundi cha VICOBA inaweza kuwasilishwa kama
inavyo onyesha katika mchoro ufuatao.
14
1- AWAMU YA UHAMASISHAJI: Hii ni awamu ya kwanza kwa uanzishwaji wa kikundi
cha VICOBA ambapo mhamasishaji ataelezea mfumo mzima wa VICOBA unavyo
fanya kazi, faida zake, hasara zake na huduma zingine zitokanazo na mfumo wa
VICOBA. Viongozi wa eneo husika hualikwa na kukaribishwa kama wahamasishaji
wakuu kutokana na nafasi zao katika jamii.
Baada ya wajumbe kuelimishwa juu ya mfumo wa VICOBA unavyofanya kazi,
wajumbe walioshiriki kwenye mkutano watakuwa na hiari ya kuanzisha kikundi au
wataomba nafasi ya kufikiria na kutafakari maelezo yaliyotolewa. Kama wajumbe
watakuwa tayari kuanzisha kikundi, viongozi wa muda watachaguliwa ambao
watakaa madarakani kwa muda wa wiki nne hadi kumi na mbili na ndipo uongozi wa
kudumu utafanyika.
2- AWAMU YA MAFUNZO: Awamu hii ni awamu ya muhimu sana maana ndio msingi
wa kikundi hujengwa na ambapo mada mbalimbali kuhusu mfumo wa VICOBA
huwasilishwa. Kwa mfano katika awamu hii, sifa na kazi za viongozi hujadiliwa, sheria za
kikundi hutengenezwa, malengo ya kikundi huanishwa, taratibu za kununua hisa na
uwekezaji mwingine ndani ya kikundi huanza, viongozi wa kudumu huchaguliwa na
mafunzo ya uendeshaji wa miradi hutolewa. Awamu hii ni lazima kuhudhuriwa na
wanakikundi wote na baada ya awamu hii kikundi kinashauriwa kutoongeza
mwanakikundi wapya hadi mwisho wa mwaka.
3. AWAMU YA
UATAMIZI
Miezi 4
4. AWAMU YA
UANGALIZI NA
KUPEA
Miezi 4
1. AWAMU YA
UHAMASISHAJI
Wiki 4
2. AWAMU YA
MAFUNZO YA
KINA
Mwezi 3
15
3- AWAMU YA UANGALIZI WA KINA: Hiki ni kipindi ambacho kikundi huwekwa kwenye
uangalizi wa karibu na kikipewa nafasi ya kuanza kujiendesha chenyewe. Katika
awamu hii mwezeshaji atakitembelea kikundi kila baada ya wiki mbili kwa mwezi wa
kwanza na mara moja kwa mwezi kwa muda wa miezi mitatu mfululizo.
Katika awamu hii kikundi kinapita katika wakati mgumu kwani ni awamu ambayo
mikopo huanza kutolewa, uvunjifu wa sheria za kikundi hujitokeza, malalamiko ya
baadhi ya wanakikundi kwa kutopewa huduma pia huibuka na mambo haya
yanatakiwa kushughulikiwa haraka kabla hayaja sababisha madhara makubwa ndani
ya kikundi. Mwisho wa awamu hii mwezeshaji huchambua udhaifu wa kikundi na
kubaini kama kikundi kinaweza kujiendesha au bado kinahitaji huduma ya Karibu.
Mwezeshaji atawasilisha fomu ya kipimo cha tathimini ambayo itajadiliwa na
wanakikundi wote.
4- AWAMU YA KUPEVUKA: Awamu hii ni awamu ambayo mwezeshaji atakitembelea
kikundi bila ya taarifa ilikufanya tathimini ya kikundi kinavyo jiendesha. Mwezeshaji
atakitembelea kikundi baada ya miezi mitatu au minne au mara nyingi zaidi kama
ataombwa na wanakikundi husika. Baada ya awamu hii vikundi ambavyo vinauwezo
wa kujiendesha vyenyewe vitapewa vyeti baada ya kufanyiwa tathimini ya kina na
watu wenye ujuzi na uzoefu wa vikundi vya VICOBA na vitapewa utambulisho wa kuwa
huru baada ya kukamilisha awamu zote muhimu.
Jukumu la mwezeshaji wa vikundi vya VICOBA ni kuwawezesha wanavikundi jinsi ya
kukiendesha na kukisimamia kikundi chao. Mwezeshaji hapaswi kufanya maamuzi kwa
niaba ya kikundi, bali awaelimishe wanakikundi ili waweze kukimiliki kikundi chao na
kufanya maamuzi yao. Mwezeshaji haruhusiwi kukitawala kikundi maana jukumu lake ni
la muda tu na baada ya kukamilika kwa mafunzo wanakikundi watajiendesha
wenyewe na mwezeshaji atabaki kuwa mshauri. Fedha na mali za kikundi zitakuwa
chini ya kikundi husika kwa hiyo hairuhusiwa taasisi yoyote kumiliki au kutumia fedha za
kikundi maana hurejeshewa wanakikundi pale wanapo jitoa au kufariki.
16
SEHEMU YA PILI
NAMNA YA KUENDESHA MIKUTANO
Lengo:
• Kuelezea aina ya mikutano ya kikundi
• Jinsi ya kuendesha mkutano ya kikundi
VIFAA
• Bango kitita
• Kalamu au chaki
• Ubao
MUDA: Dk 45
MBINU ZA KUFUNDISHIA:
• Kuwasilisha mada.
• Majadiliano.
• Maswali na majibu.
• Mifano.
MADA YA KWANZA: AINA ZA MIKUTANO
Kutakuwa na mikutano aina tatu ya vikundi vya VICOBA. Kutakuwa na mkutano wa
kawaida, mkutano wa Dharura na mkutano mkuu.
Mkutano wa Kawaida.
Mkutano wa kawaida ni mkutano unaofanyika kwa wiki mara moja kwa lengo la
manunuzi ya hisa, urejeshaji wa mikopo, ukopaji wa fedha na pia mkutano huu
hutumika kama jukwaa la kuelezea mambo mbalimbali ya kimaendeleo yanayo
wahusu wanakikundi. Katika mikutano hii wanachama wanaruhusiwa kuwaalika watu
mbalimbali wenye ujuzi na kutoa mafunzo kutokana na mahitaji ya kundi husika.
Mkutano wa Dharura.
Huu ni ule mkutano maalum ambao huitishwa kwa sababu mbalimbali za maamuzi
ambayo yatahitaji wanakikundi wote kushiriki katika jambo husika. Mambo mbalimbali
yanaweza kusababisha kuitishwa kwa mkutano wa dharura na ambao ni pamoja na
mabadiliko ya uongozi, uboreshaji wa sheria za kikundi, kutatua migogoro ya ndani ya
kikundi na jambo lolote litakalo hitaji ushiriki wa wanakikundi wote. Tangazo la mkutano
hutolewa siku 7 kabla ya mkutano ili kuwezesha wanakikundi wote kuhudhuria
kikamilifu.
17
Mkutano mkuu.
Mkutano huu hufanyika mara moja kwa mwaka na mambo mbalimbali hujadiliwa na
kuamuliwa kwa maendeleo ya kikundi. Mambo hayo ni pamoja na kuwasilishwa kwa
tarifa ya fedha ya kikundi ya mwaka, kupata taarifa na mchanganuo wa makusanyo
yote ya kikundi, kuchagua viongozi wapya, kuboresha sheria, kuongeza au kupunguza
thamani ya hisa na kugawana faida.
Mkutano mkuu unatakiwa uandaliwe mapema na siku ambayo wanachama
wanatakiwa kupongezana kwa kufanya tafrija fupi. Mfuko wa faini au michango
kutoka kwa wanachama hutumika kwa ajili ya kugharamia sherehe. Inashauriwa katika
sherehe hii wageni mbalimbali waalikwe na kipaumbele kitolewe kwa viongozi wa
serikali waliopo katika eneo la kikundi na viongozi wa dini
MADA YA PILI: UENDESHAJI WA MKUTANO
Mfumo wa uendeshaji wa vikundi vya VICOBA unatofautiana na mifumo mingine hasa
katika uendeshaji wa mikutano na shughuli zote. Mfumo wa VICOBA wanachama
wanakutana mara moja kwa muda maalum na maamuzi yote hufanywa mbele ya
wanachama.
Jinsi ya uendeshaji
Muda wa kuanza kufanya mkutano, kamati ya uongozi yenye wajumbe watano
ambao ni Mwenyekiti, Katibu, Mwekahazina na Wahesabu fedha wawili wanakaa
mbele wakitazamana na wajumbe wengine. Mwenyekiti atafungua kikao kwa
kuwaomba washiriki kila mmoja kwa imani yake kuomba dua au sala ya kimya kimya
angalau nusu dakika.
Utaratibu wa kukaa wakati wa uendeshaji wa mikutano ya kikundi.
Wahesabuji
Katibu Mhazini
Mwenyekiti
Wanakikundi
18
1- KUANZA MKUTANO
Mwenyekiti atatangaza mbele ya wanakikundi kuwa mkutano umefunguliwa na
atawaomba washika funguo kufungua sanduku na mwekahazina kutoa ndani
ya sanduku vitabu vya hisa, leja na bakuli tatu kwa ajili ya maandalizi ya shughuli
za kibenki ndani ya sanduku. Bakuli kubwa ni kwa ajili ya kukusanyia Hisa, bakuli
inayo fuata ni kwa ajili ya kukusanyia fedha za mfuko wa jamii na marejesho na
bakuli dogo kuliko zote litatumika kukusanyia faini.
Baada ya sanduku kufunguliwa na bakuli kutolewa Mwenyekiti atamwomba
Katibu kuita mahudhurio na kukusanya faini kwa watu wote ambao wamekiuka
kanuni na taratibu za kikundi.
2- AGENDA
Mara baada ya kikao kufunguliwa mwenyekiti atatoa taarifa fupi ya makusanyo
kwa wiki iliyopita iliyoandikwa kwenye leja au daftari kubwa na kutangaza salió
la pesa zilizobaki kwenye sanduku baada ya wanakikundi kukopa kwenye
mkutano uliopita. Mwenyekiti ataainisha agenda kuu ya mkutano na kuwauliza
wanakikundi kama wanakubaliana na agenda hiyo na kama kuna pendekezo
la agenda nyingine ya kujadiliwa. Mikutano ya kawaida agenda kuu itakuwa ni
kununua hisa, mfuko wa jamii, kutoa marejesho, kupata mafunzo, kutoa mikopo
na kujadili mengineyo kama yatakuwepo.
3- UWEKAJI WA FEDHA
Mwenyekiti atamwomba katibu aendeshe shughuli za kibenki na uwekaji wa
fedha za kikundi kwa kumtaka katibu kuwaita washiriki namba zao na kununua
hisa kwa kila mmoja kutaja kwa sauti idadi ya hisa anazo nunua na kiasi cha
mfuko wa jamii anachowekeza. Mwanachama atawasilisha fedha kwa
wahesabuji na kitabu anakabidhiwa mwekahazina kwa ajili ya kujaza hisa na
jamii alizo wekeza mwanachama.
Baada ya makusanyo ya hisa Katibu ataongoza zoezi la urejeshaji wa mikopo na
kila mwanachama anayerejesha atawasilisha mbele kiasi mbele na katibu
atajaza kwenye daftari kubwa mwekahazina atajaza kwenye kitabu kidogo.
Wahesabu fedha watapokea fedha na kuziweka kwenye bakuli husika wakati
huo huo wajumbe wawili watapewa jukumu la kujaza leja.
Mwisho Katibu atapiga mahesabu kwenye Daftari kubwa na Mwekahazina
atapiga mahesabu kwenye vitabu vya wanakikundi na leja. Wahesabu fedha
watatoa tarifa ya fedha taslimu zilizokusanywa na mwenyekiti atatangaza tarifa
kwa wajumbe.
19
4- MAREJESHO
Baada ya makusanyo Katibu atawaongoza wajumbe kwenye awamu ya kutoa
marejesho ya mikopo. Katibu ataanza kuwaita majina wanakikundi ambao
tayari muda wao wa kurejesha umewadia. Katibu ataandika idadi
inayorejeshwa kwenye kaunta book, mwekahazina kwenye kitabu cha
mwanakikundi na wajumbe wengine kwenye leja ya mikopo na wahesabu
fedha watapokea fedha inayorejeshwa toka kwa mawanakikundi husika.
Fedha zikikusanywa na kuhesabiwa na wahesabu fedha zitakabidhiwa kwa
mhazina kwa uhakiki zaidi na takwimu sahihi kupelekwa kwa mwenyekiti na
kutangaza jumla ya makusanyo yote.
5- MIKOPO
Baada ya kukamilika kwa shughuli ya marejesho Katibu atazisoma fomu zilizo
wasilishwa mbele na wakopaji. Kila fomu itajadiliwa na kupitishwa au kukatialiwa
kwa sababu ambazo zitatajwa na mtoa hoja. Sababu zinaweza kuwa nyingi
kiwa ni pamoja na kuto rejesha mikopo ya nyuma aliyo kopa kwa wakati,
kutohudhuria kikamilifu, na kutokidhi masharti yaliyopangwa na wanakikundi.
Wajumbe watamjadili na kupitisha au kukataa maombi ya mwanakikundi husika
na kama watamkubalia basi fomu itapokelewa na mjumbe atakabidhiwa
mkopo wake baada ya kutoa Bima ya mkopo.
Katibu atasoma taarifa ya fedha zilizosalia baada ya kutoa mikopo kwa
kuainisha fedha zitakazo baki sandukuni au benki.
6- KUTHIBITI FEDHA
Makusanyo ya fedha ni lazima yatangazwe kwa wajumbe baada ya kukamika
kwa zoezi la kibenki. Baada ya matangazo wahesabu fedha watamkabidhi
mwekahazina na atazihakiki na kuziweka ndani ya sanduku au kuzipeleka benki
na kipindi hicho takwimu itatolewa kwa mwenyekiti ya kuonyesha jumla ya
makusanyo yote na atatangaza kwa wanakikundi.
Iwapo kikundi kitafungua akaunti basi kiongozi au mwanakikundi yeyote
atachaguliwa na kuombwa kuwasilisha fedha hizo katika benki husika. Ili
kuhakikisha uhifadhi wa fedha ni salama yafuatayo yanapendekezwa
yafanyike:
20
• Risiti ya kuweka fedha iwasilishwe katika kikao kinachofuata na
mwanakikundi aliyepeleka fedha Benki, ikionyesha mhuri wa benki husika na
tarehe fedha zilipopelekwa benki.
• Kikundi kiombe taarifa fupi ya fedha toka katika Benki husika, kila mwezi.
• Iwapo wanakikundi hawana ufahamu au uelewa juu ya taarifa za Benki basi
mafunzo maalum yatolewe kwa wanakikundi kujenga uwezo wao.
Angalizo. Kwa muda mrefu sana vikundi vya VICOBA vinatumia masunduku
kuhifadhia fedha na kwasasa jambo hili limeonekana kuwa ni la hatari hasa
baada ya watu wengi kubaini njia hiyo ya uwekaji wa fedha. Kutokana na
kupungua kwa usalama na matukio kadhaa kutokea maeneo mbalimbali ya
Tanzania kwa watu kuiba masanduku yakiwa na hela na mengine wakihisi
kuwepo kwa hela.
Kutokana na matukio kuendelea kukithiri vikundi vinashauriwa kutoweka fedha
ndani ya masanduku zaidi ya Laki mbili na vikundi vinavyo bakiza fedha nyingi
vifanye jitihada za kufungua akaunti benki za kuhifadhia fedha za ziada. Vikundi
vinashauriwa pia kuhakikisha kila baada ya makusanyo mikopo inatolewa kwa
wanachama wenye uhitaji na wakati wa kufunga hesabu za mwaka vikundi
haviruhusiwi kukusanya fedha zote na kuanza upya bali vitafunga hesabu
wakati mikopo ikiwa mikononi mwa wanachama.
Kikundi kitatakiwa kufanya makisio ya faida itakayo gawanywa kwa
wanachama mwisho wa mwaka na fedha hizo ndizo zitatakiwa kuhifadhiwa ili
kutoa mgao na kipindi hicho fedha zingine zikiwa kwenye mzunguko wa
wanachama. Matukio mengine yaliyojitokeza ni pamoja na fedha za kikundi
kihifadhiwa kwenye akaunti za viongozi, watu binafsi au za wawezeshaji na
mchezo huo pia hauruhusiwi maana unahatarisha fedha za kikundi.
7- KUFUNGA KIKAO
Mwenyekiti atawauliza wanakikundi kama kuna mengineyo na baada ya zoezi
hilo atawashukuru wanakikundi kwa kufika na kutoa matangazo kwa ufupi kama
yapo kabla ya kuahirisha kikao hicho.
21
SEHEMU YA TATU
UENDESHAJI WA SHUGHULI ZA KIBENKI
Lengo:
• Kufanunua maana na faida za kununua hisa.
• Kutoa mwongozo wa jinsi ya kusimamia fedha za wanakikundi.
• Kutoa ufafanuzi na taratibu za kutoa na kurejesha mikopo kwa wanakikundi.
• Kufahamu viwango vya ziada ya mikopo
• Kufahamu umuhimu wa uwekaji wa bima
Vifaa:
• Bango kitita
• Karamu au chaki ya kuandikia
• Ubao wa kuandikia
Muda: saa Moja
Mbinu za kufundishia:
• Kuwasilisha mada
• Majadiliano
• Maswali na majibu.
• Mifano na mengineyo
Mada hii itaongelea mambo yote ya muhimu maana inajikita kwenye uendeshaji wa
mifuko yote ya kikundi. Washiriki wanatakiwa kuelewa kwa undani mambo yote
yanayo husu Hisa, Jamii, Mikopo, Marejesho, Bima, Ziada ya Mikopo na mfuko wa
adhabu. Mwezeshaji na wanavikundi nilazima wakatenga muda wa kutosha kuyajadili
mambo haya ya muhimu. Nimuhimu mwanachama mpya ndani ya kikundi wajumbe
wengine wakatoa mafunzo kwa mjumbe mpya ili aweze kuyaelewa mambo ya msingi
ya kuzingatia.
MADA YA KWANZA: HISA
1. Mwezeshaji anza kwa kuwauliza washiriki hisa ninini?
2. Je nani amewahi kununua hisa sehemu yoyote na ananufaikaje na ununuaji huo?
3. Kunafaida gani ya kunua Hisa?
22
4. Kuna tofauti gani kati ya hisa na akiba
Maelezo ya mwezeshaji. Hisa ni fedha inayowekezwa na mwanakikundi katika kikundi
kwa lengo la kupata faida na kuwa mmiliki wa kikundi husika.
Mwanakikundi anaweza kununua hisa kati ya moja hadi tano kila wiki. Thamani ya hisa
moja itatokana na makubaliano ya wanakikundi wa kikundi husika na inashauriwa
kiwango hicho kizingatie uwezo wa kiuchumi wa wanakikundi wake.
Mfano kama thamani ya hisa moja ni shiling 2,000/- hisa tano thamani yake itakuwa ni
shilingi 10,000/- kwa wiki na mwanakikundi anahiari ya kuwekeza kiwango anachoweza
lakini isipungue hisa moja na isizidi hisa tano.
Mwanakikundi anaruhusiwa kununua hisa moja hadi tano kila mkutano unapo fanyika,
na lengo la kuweka uwiano huu ni kuepusha watu wachache wasiweze kukimiliki
kikundi na kuwawafanya wengine kuwa wanyonge kwa upande wa kipato na sauti
ndani ya kikundi. Pia husaidia kuleta uwiano wa karibu kwa upande wa mikopo
wanayostahili pamoja na mafao ya mgao mwishoni mwa mwaka. Kuweka kikomo
cha hisa tano ni kuondoa uwezekano wa baadhi ya washiriki kutumia uwezo wao
kukitawala na kukiyumbisha kikundi kama wapendavyo.
Hisa huwakilishwa katika kikundi na kupigwa muhuri au kuandikwa kwa tarakimu katika
kitabu cha mwanakikundi husika na kwenye leja ya kikundi. Thamani huandikwa ndani
ya leja ya kikundi na fedha zikisha kusanywa huwekwa ndani ya sanduku la fedha au
hupelekwa benki. Ikumbukwe kuwa mwanakikundi akishindwa kutoa hisa zake basi wiki
hiyo haitawezekana kufidiwa tena.
Hisa ni mali ya mwanakikundi na mwanakikundi atakapo jiondoa, kikundi kitawajibika
kumrejeshea hisa zake zote, mfuko wa jamii na malimbikizo mengine kama yapo
ambayo mwanakikundi aliye jitoa katika kikundi anastahili lakini faida hataweza
kupewa hadi kikundi kifunge hesabu za mwaka.
MADA YA PILI: MIKOPO
Anza na maswali haya
1. Kwa nini tunakopa
2. Wangapi wamewahi kukopa
3. Kluna faida gani ya kukopa
4. Kunahasara gani ya kukopa
23
5. Masharti gani nimuhimu kuyaweka kwa wakopaji
Ni fedha au mali ambazo mkopeshaji anamtaka mkopaji azirejeshe kwa makubaliano
maalumu. Katika mfumo huu kutakuwa na mikopo ya aina kuu mbili. Kutakuwa na
mikopo itakayo kopwa kutokana na mfuko wa Hisa na kutakuwa na mikopo itakayo
kopwa kutokana na mfuko wa jamii. Mikopo ya hisa, mwanachama ataruhusiwa
kukopa mara tatu ya hisa alizo wekeza ndani ya kikundi na kurejesha na faida ambayo
itatumika kuwagawia wanachama mwisho wa mwaka na mikopo ya jamii itarejeshwa
bila ya faida.
Kila mkopaji atajaza fomu ya mkopo na kubainisha dhamana ya mkopo wake.
Dhamana ya mikopo itathibitishwa na wajumbe wa vikundi vidogo na dhamana hizo
zitatakiwa kulingana au kuzidi kiasi cha mkopo anacho daiwa mwanachama husika.
Mikopo yote katika vikundi vya VICOBA itatakiwa kulipwa kila mwezi na muda wa
kurejesha mikopo ni kati ya miezi mitatu hadi mwaka mmoja. Mkopo wa kwanza
mkopaji ni lazima aurejeshe ndani ya muda wa miezi mitatu, mkopo wa pili ndani ya
miezi sita na mkopo wa tatu kikundi kinaweza kuamua wanachama akarejesha mkopo
ndani ya mwaka mmoja.
Mfumo haumkatazi mkopaji kutoa marejesho ya mkopo wake kila wiki na cha msingi
anatakiwa kuzingatia kuwa ndani ya mwezi mmoja awe amekamilisha kiwango
alichokuwa anatakiwa kukirejesha. Kikundi kinashauriwa kutunga sheria ambazo
zitaainisha taratibu za kuchukua mkopo na hatua zitakazo chukuliwa iwapo mkopaji
atashindwa kurejesha mkopo wake kwa wakati. Kikundi kinatakiwa kuhakikisha sheria
zinasimamiwa na zinafuatwa na kila mwanakikundi ili kuweka nidhamu katika utoaji na
urejeshaji wa mikopo kwa wakati.
MADA YA TATU: MAREJESHO YA MKOPO
• Je wangapi wamewahi kukopa.
• Mikopo mnayokopa mnarejesha kwa muda gani
Katika mfumo wa VICOBA mwanakikundi anatakiwa kutoa marejesho mara moja kwa
mwezi na anaruhusiwa kulipa kidogo kidogo kila wiki kama taratibu za vikao vya kikundi
vitakavyo bainisha na kama biashara yake inamruhusu kufanya hivyo.
Wanakikundi wote watakao shindwa kurejesha mkopo kwa wakati kama ilivyo
kubaliwa na alivyo jaza kwenye fomu yake ya mkopo basi atatakiwa kutozwa faini ya
asilimia mbili ya mkopo aliotakiwa kuurejesha kwa mantiki kwamba kama angerejesha
fedha hizo zingekopwa na mwanakikundi mwingine na kikundi kingepata faida.
24
Mfumo huu pia unamruhusu mwanakikundi kumaliza deni lake kabla ya muda wake na
kumwezesha kuomba mkopo mwingine ndani ya kikundi bila kusubiliana. Nidhamu
kubwa inatakiwa kuhakikisha kila mkopaji anatoa marejesho yake kama inavyo takiwa
ili kuwawezesha wengine kukopa.
Katika mazingira yasiyotarajiwa mwanakikundi akishindwa kurejesha mkopo kwa muda
uliopangwa kikundi kitakuwa na uwezo wa kumuongezea muda au kuchukua
dhamana zake na kama hazitoshi basi wadhamini wake wa kikundi kidogo
watawajibika kulipa deni lililo salio.
Mfumo wa VICOBA unaonyesha mafanikio makubwa kutokana na mfumo wa
urejeshaji mikopo kila mwezi. Kurejesha mkopo kila mwezi kuna msaaidia mkopaji
kupunguza hatari ya fedha za kikundi kupotea na marejesho ya kila wiki huwasaidia
wanakikundi wengine kukopa. Kitendo cha kukaa na fedha muda mrefu bila kurejesha
kina athiri maendeleo ya kikundi hasa kutokana na kutopatikana kwa mikopo kwa
wakati na matokeo yake baadhi ya wanachama kusubiri muda mrefu bila kukopa na
mwisho kukata tamaa na kujitoa.
MADA YA NNE: ZIADA YA MKOPO
1. Tunaposema ziada ya mikopo tunamaanisha nini
2. Wangapi wanafahamu riba
3. Riba ni mali ya nani
4. Je kama kuna wakopaji wape nafasi ya kueleza ni asilimia ngapi ya riba hutozwa
kwenye taasisi zingine.
Tofauti kati ya ziada ya mkopo na riba
Ziada ya Mkopo ni asilimia ya mkopo ambayo mkopaji anatakiwa kurejesha kwenye
kikundi na mwisho wa mwaka fedha hizo humrudia mwenyewe kwa njia ya gawio la
faida na,
Riba ni fedha ambazo mkopeshaji amemtaka mkopaji kurejesha fedha alizo kopa na
kiasi fulani na ambacho ni mali ya mkopeshaji. Kwa mfano mtu anapokopa benki faida
inakuwa mali ya benki.
1.1. Umuhimu wa ziada ya mkopo.
Hutengeneza mfuko wa faida ambayo wanakikundi hugawana mwisho wa mwaka
kama gawio la hisa walizo wekeza. Katika kikundi siyo wanachama wote wanakopa
fedha na kutokopa fedha kwao kunawasaidia wengine kukopa mara tatu ya hisa
25
walizo wekeza ndani ya kikundi. Uzoefu unaonyesha mwanachama anayewekeza hisa
zake ndani ya kikundi anauhakika wa kupata faida kati ya asilimia kumi na mbili hadi
kumi na tisa kwa mwaka na kiwango hiki cha fedha ni vigumu kupata kama
umewekeza kwenye makampuni au taasisi nyingine za fedha.
Mfuko huu pia husaidia kugharamia madeni mabaya ambayo mfuko wa bima
umeshindwa kuyalipa. Kutofidiwa kwa mfuko wa bima kunasababisha hisa za
wanakikundi wote kuwa kwenye hatari ya kufilisika.
Mfuko huu pia unasaidia kukabiliana na majanga mbalimbali yanayoweza kujitokeza
dhidi ya mali za wanakikundi. Viwango vya ziada ya mikopo vikiwa vidogo huathiri
ukuaji wa mtaji wa kikundi na mgao wa faida mwisho wa mwaka na Wakati Viwango
vya riba vikiwa vikubwa huathiri utashi wa mkopaji kuchukua mikopo.
Mapendekezo:
Inashauriwa Ziada ya Mkopo itozwe kwa asilimia tano (5%) kwa mkopo unaolipwa kwa
miezi 3; asilimia kumi (10%) kwa mkopo unaolipwa kwa miezi sita; na asilimia kumi na
tano (15%) kwa mkopo unaolipwa miezi kumi na mbili.
Viwango hivi vinavyotozwa kama nyongeza ya mkopo vinaweza kupungua au
kuongezwa baada ya wanakikundi kufanya tathmini ya kikundi chao mwisho wa
mwaka na kukubaliana juu ya kubadilisha viwango hivi.
MADA YA TANO: MFUKO WA JAMII
1. Je tunapo pata matatizo ya dharura tunapata wapi msaada
2. Je inaruhusiwa mwanachama kuchukua mtaji na kwenda kujitibia au kulipia ada
ya Mtoto shule.
Mfuko wa jamii una lengo la kutoa mkopo kwa wanakikundi ili kusaidia mahitaji ya afya
na elimu yanayo jitokeza bila ya kujiandaa. Mfuko huu unatolewa kama mkopo usio
na riba na ni mkopo unaomsaidia mwanakikundi moja kwa moja na wanafamilia wake
pale wanapopata tatizo la dharura. Mfuko wa jamii hujengwa kwa kila mwanakikundi
kuchangia kiasi cha fedha katika kikundi kila wiki wanapo kutana.
Mfano: Kikundi kinaweza kuamua kila mwanakikundi kutoa shilingi elfu moja (1000/-)
kwa wiki katika mfuko huu. Kama kila mwanachama atachangia kiasi hicho basi
mwanachama ndani ya kikundi ataruhusiwa kukopa mkopo ambao hautazidi shilingi
laki moja na hii itasaidia wanakikundi wenye matatizo mbalimbali kuweza kunufaika na
mfuko huu.
26
Mkopaji atatakiwa kurejesha mkopo wa mfuko wa jamii ndani ya miezi mitatu naakilazi
mika kurejesha moja ya tatu kila mwezi. Mkopaji akishindwa kurejesha mkopo ndani ya
miezi mitatu bila sababu maalumu mwanachama huyo atatakiwa kulipa ziada ya
mkopo kama mkopo wa kawaida. Iwapo pia mwanachama atafariki na deni la mfuko
wa jamii kikundi kitakata kiasi kwenye mafao yake kulipia deni analo daiwa na kiasi
kitakacho salia atakabidhiwa mrithi wake.
Kila mwanachama anawajibika kuhakikisha kiwango alicho changia kwenye kikundi
katika mfuko wa jamii kinalingana na idadi ya wiki. Iwapo mwisho wa mwaka itabainika
miongoni mwa wanakikundi walichangia kiasi pungufu basi fedha zao za mgao wa
faida zitakatwa ilikuweka ulinganisho kati yake na wanachama wengine ndani ya
kikundi.
MADA YA SITA: MFUKO WA BIMA
1. Je kunamwanachama ambaye amewahi kukatia bima
2. Je huduma gani ambazo hukatia Bima
3. Kuna faida gani ya kukatia bima
4. Matukio gani mngependa kukatiwa Bima
Mfuko wa Bima ni mfuko ambao umeanzishwa kwa lengo la kulinda mikopo yote
itakayo kopwa endepo wakopaji watafariki. Mfuko huu utakuwa na wajibu wa kuweka
usalama kwa mtaji wa kikundi hasa pale mmoja wa wanakikundi anapofariki akiwa
hajamaliza kulipa mkopo wake ndani ya kikundi. Mfuko wa bima utachangiwa na kila
mwanakikundi atakayekopa mkopo katika kikundi husika.
Mwanakikundi atachangia asilimia mbili ya mkopo wake kwenye mfuko wa bima ya
kikundi. Fedha hizo hazitarudishwa kwa mwanakikundi baada ya kumaliza deni lake
bali mfuko huu utaendelea kujengwa ilikuuwezesha kukabiliana na majanga makubwa
yanayoweza kujitokeza. Mwanakikundi akijitoa katika kikundi hataruhusiwa kudai na
hatarejeshewa fedha za mfuko wa bima maana mikopo bado itaendelea kukopwa
kwa wale watakao baki katika kikundi. Fedha za bima ni mali ya kikundi na iwapo
kikundi kitasambaratika fedha zote za Bima zitachanganywa na mfuko wa ziada ya
mkopo na kugawanywa kama faida.
27
2. Faini
Kutakuwa na mfuko wa faini ambao utakuwa unajitegema katika kikundi na ukiwa na
majukumu ya kugharamia shughuli zote za uendeshaji ikiwemo kutoa nakala za fomu,
kununua vinywaji kwa wageni na wanakikundi wenyewe pale inapo hitajika na
kununua vifaa vinapo kwisha.
Faini ni fedha zitakazo kuwa zinalipwa na mwanakikundi anayekiuka kanuni na taratibu
za kikundi walizojiwekea. Kanuni za kikundi hutungwa na wanakikundi husika na
zikiainisha malengo ya kikundi, taratibu za kuendesha kikundi, vitendo visivyokubalika
katika kuendesha kikundi na iwapo mwanakikundi atakwenda kinyume na
makubaliano ya wanakikundi. .
Fedha za faini zitatumika katika kugharamia shughuli za kikundi na muda mwingine
wanakikundi husika wanaweza kujipongeza kwa kunywa vinywaji au matumizi
mengine yoyote yatakayo pitishwa na wanakikundi. Mfuko huu pia unawajibu wa
kugharamia safari za viongozi, gharama za mafunzo na kuandaa tafrija mwisho wa
mwaka.
Vikundi vingi vya VICOBA havioni umuhimu wa kufanya tafrija. Tafrija ni muhimu sana
kwenye vikundi hasa baada ya kutimiza mwaka maana kwenye tafrija wageni
mbalimbali hualikwa na mara nyingi tafrija huleta hamasa hasa kwa wengine kuja
kujifunza. Wakati umefika sasa vikundi viwili hadi kumi kuunganisha kufanya tafrija
sehemu moja na ambayo wanaweza kuwaalika wageni mbalimbali badala ya kila
kikundi kualika wageni wao.
MADA YA SABA: KUFUNGA MAHESABU MWISHO WA MWAKA
Kila kikundi kitakuwa kinafunga hesabu zake kila mwaka baada ya kutimiza wiki 52 za
uwekaji wa fedha na uchukuaji wa mikopo. Hesabu zitatakiwa kufungwa na ripoti ya
jumla ya makusanyo ya hisa, mikopo, bima, mfuko wa jamii, faini na michango mingine
kama itakuwepo itatolewa.
Kikundi kitafunga hesabu za mwaka mzima kwa kutambua fedha zilizowekezwa ndani
ya kikundi na kila mwanakikundi kwa mwaka mzima. Mwisho wa mwaka kila kikundi
kinatakiwa kuhakikisha hesabu zinabainisha wazi kiasi cha fedha taslimu kilichopo
ndani ya kikundi na kiasi cha fedha kilichopo mikononi mwa wanachama kwa njia ya
mikopo. Fedha taslimu zinajumlisha fedha zote zilizopo kwenye kisanduku na zilizo
hifadhiwa benki au katika taasisi yoyote ya fedha iliyoruhusiwa kwa mujibu wa Benki
kuu ya Tanzania.
Wakati wa mahesabu viongozi pamoja na wanakikundi watahakikisha takwimu za
fedha zimetengwa kwenye makundi kama ilivyo kuwa inachangiwa na kikundi husika.
28
Viongozi watajumlisha mifuko yote na kupata jumla yake kama inavyo onyesha
kwenye mfano hapo chini.
S/N IDADI
YA HISA
THAMANI
YA HISA
MFUKO
WA
JAMII
BIMA YA
MKOPO
ZIADA
YA
MIKOPO
MADENI
YA HISA
MADENI
YA
JAMII
1 1000 5,000,000 104,000 2,000,000 8,000,000 0
2 1500 7,500,000 104,000 3,000,000 5,000,000 0
3 750 3,750,000 104,000 375,000 3,000,000 0
4 900 4,500,000 104,000 0 0 0
5 850 4,250,000 104,000 2,625,000 2,000,000 0
JUMLA 5,000 25,000,000 520,000 2,300,000 7,500,000 18,000,000
Hisa 25,000,000
Jamii 520,000
Bima 2,300,000
Ziada ya Mkopo 7,500,000
JUMLA ya fedha zote 35,320,000
Madeni ya Hisa 18,000,000
Taslim kwenye sanduku 17320,000
JUMLA KUU madeni na tslimu 35,320,000
Baada ya kukamilisha zoezi la kujua kikundi kinathamani ya shilingi ngapi kama inavyo
onyesha hapo juu wanakikundi watakwenda kwenye zoezi la mwisho la kuhakikisha
kama fedha tajwa hapo juu zipo au hazipo. Baada ya mahesabu kuwiana zoezi la
mwisho litakuwa ni kugawana fedha za Ziada ya mkopo kama gawio la mwisho wa
mwaka na kutoa fedha za wanachama wanajiondoa katika kikundi.
3. Jinsi ya kugawana faida mwisho wa mwaka.
Mgao wa faida utafanyika kwa kutumia fedha za faida zilizo patikana na idadi ya hisa
zilizo changiwa na wanachama kwa muda wote wa uhai wa kikundi. Baada ya
kufunga hesabu mgao wa faida utafanyika kwa kuchukua faida iliyopatikana na
kugawanya na idadi ya hisa zilizowekezwa ndani ya kikundi. Lengo la zoezi hili ni
kubaini hisa moja imepata faida ya shilingi ngapi kabla ya kuigawa faida hiyo kwa kila
hisa za mwanakikundi.
29
Kama inavyo onyesha jedwali hapo juu, kikundi kwa mwaka mzima kiliweza kununua
hisa 5000 zenye thamani ya Tsh ml 25, 000,000 na mwaka kilipata faida ya Tsh milioni 7,
500,000. Kutokana na mfumo wa kupata faida ya kila hisa moja zitachukuliwa shilingi 7,
500,000 ambazo ni ziada ya mikopo na zitagawanywa na idadi ya hisa zilizo nunuliwa
kwa kipindi chote ambacho ni hisa 5000. Baada ya kuzigawanya kila hisa itapata faida
ya shilingi 1500. Baada ya kupata faida hiyo kila manachama atazidishiwa hisa zake na
faida ya hisa moja iliyopatikana kama inavyo onyesha kwenye jedwali hapo chini.
S/N IDADI YA HISA FAIDA YA HISA MOJA MGAO SAINI YA MPOKEAJI
1 1000 1500 1,500,000
2 1500 1500 2,250,000
3 750 1500 1,125,000
4 900 1500 1,350,000
5 850 1500 1,275,000
JUMLA 5000 7,500,000
Baada ya kuandaliwa kwa jedwali hili mgao wa faida utatolewa kwa wanakikundi
wote ndani ya kikundi bila ya kujali kama walikopa au hawakukopa na kila mpokeaji
atatia saini yake. Ikumbukwe kuwa mgao wafaida hautakuwa sawa bali mwenye hisa
nyingi atapata faida kubwa na mwenye hisa ndogo atapata gawio dogo.
30
SEHEMU YA NNE
UONGOZI WA KIKUNDI
Lengo:
♦ Kuwasaidia washiriki kufahamu umuhimu wa kuwa na Kamati ya uongozi
♦ Kuwasaidia kutambua majukumu ya kamati ya uongozi na nafasi tofauti zilizomo
kwenye kamati.
♦ Kuwawezesha washiriki kueleza majukumu, sifa na mamlaka ya wote ambao
watashika nafasi za uongozi, pamoja na kuendesha vikao
Vifaa:
• Bango kitita
• Kalamu
• Ubao
Muda: 1.00
Mbinu za kufundishia
• Kuwasilisha mada
• Majadiliano
• Maswali na majibu.
• Mifano
MADA YA KWANZA: KAMATI YA UONGOZI
Kamati ya uongozi itaundwa na wajumbe watano. Wajumbe hawa ni mwenyekiti,
Katibu, mwekahazina na wahesabufedha wawili. Wajumbe hawa watachaguliwa
miongoni mwa wanakikundi wenzao katika mkutano mkuu wa wanachama. Kamati hii
ndiyo yenye dhamana ya kuongoza na kusimamia shughuli na rasilimali za kikundi.
Wajumbe wa kamati watachaguliwa kwa mujibu wa sifa, uwezo na weredi wao katika
jamii.
Nafasi za viongozi kama watakuwa hawapo zitajazwa na mwanakikundi yoyote
atakaye pendekezwa siku ya mkutano na atakuwa na madaraka ya kufanya shughuli
zote ambazo kiongozi husika alitakiwa kuzitekeleza.
31
Hadithi.
Hadithi hii ni ya kikundi cha maendeleo, kikundi kilianzishwa na washiriki 27 na baada
ya wiki moja wakajikuta wameongezeka hadi wanakikundi 45. Washirki waliamua
kujigawa katika makundi mawili. Katika kikundi cha pili wanakikundi walimchagua mke
wa Kiongozi wa serikali na kuwa mwenyekiti wa kikundi. Mwezeshaji alijaribu bila
mafanikio kuwaelimisha wanakikundi sifa za mwenyekiti wa kikundi lakini wanakikundi
waliendelea kung’ang’ania awe mwenyekiti wao kwa sababu watapatiwa misaada
na matokeo yake alishindwa kuendesha kikundi na kikundi kushuka kimaendelea siku
hadi siku. Baadae wanakikundi waliamua kumbadilisha mwenyekiti lakini tayari
wanachama wengi walikuwa wamejitoa na baadhi ya wanakikundi walikimbia bila
kurejesha mikopo.
A. Je mmejifunza nini kutokana na hadithi hii?
B. Mnafikiri ingekuwa ni nyinyi mngefanya nini?
4.3. MAELEZO YA MAJUKUMU NA SIFA ZA KILA MJUMBE WA KAMATI YA UONGOZI.
MWENYEKITI
SIFA
• Awe mwenye uwezo wa kuendesha
mikutano
• Mwenye tabia njema katika jamii
• Mwenye kukubalika mbele ya jamii na
kusikilizwa
• Mwaminifu, mwenye heshima,
mwenye hekima na busara.
• Mwenye uwezo wa kutatua migogoro
ndani ya kikundi.
• Mvumilivu, mwenye kupatikana katika
vikao vya kikundi na mwenye uwezo
wa kusimama mbele ya watu.
• Asiwe mlevi
• Mwenye hamasa nzuri katika jamii.
• Mwajibikaji na mfano wa kuigwa na
wanakikundi wengine katika kikundi.
• Mwenye ushawishi na utetezi mzuri
katika maendeleo ya kikundi.
MAJUKUMU
• Kuongoza kikundi
• Kuwakilisha kikundi kwa watu wa nje
na wasio wanakikundi
• Kuhakikisha sheria za kikundi za
zinafuatwa na kuheshimiwa
• Kuwashauri wanakikundi
• Kutafuta suluhisho la ugomvi miongoni
mwa wanakikundi
• Kuhitimisha mikutano
• Kufungua mikutano na kutangaza
agenda
• Kutangaza makusanyo yaliyo pita
(uwekaji fedha) na baadae kutoa
mikopo.
• Kuhakikisha usalama wa mali zote za
kikundi.
• Kushirikiana na wajumbe wengine wa
kamati ya uongozi kulipa mali pale
inapobainika kuwa wao ndio wahusika
wa upotevu wa mali hizo.
KATIBU
32
SIFA
• Ajue kusoma, kuandika na kuhesabu
kwa ufasaha
• Awe ni mwenye uwezo wa kutoa
taarifa sahihi kuhusiana na mwenendo
wa shughuli za kikundi.
• Awe na mahudhurio mazuri kwenye
kikundi.
• Mwenye kuwajibika, hodari, mwaminifu
na mwenye busara
• Mwenye kuheshimu wenzake
• Asiwe mlevi.
• Asiwe na upendeleo
MAJUKUMU
• Kuandika na kukumbuka shughuli zote
zinazofanywa na kikundi katika kila
mkutano.
• Kuita wanakikundi wakati wa kununua
hisa na uwekaji wa mfuko wa jamii.
• Kutoa taarifa na shughuli za kikundi
kwa mwezeshaji wakati wa ufuatiliaji.
• Kulipa fedha zinazo potea ikibainika
kuwa kamati ya uongozi wa kikundi
imehusika.
MHAZINA
SIFA ZAKE
• Mwenye maudhuria mazuri kwenye
kikundi.
• Mwenye kujua kusoma kuandika na
kuhesabu kwa ufasaha
• Mwenye nyumba yenye usalama wa
uhakika na inayoheshimika
• Mwanifu katika jamii na mwenye
busara
• Inashauriwa awe mwanamke
• Mwenye mahusiano mazuri katika
familia yake
• Mwenye familia na asiyehamishika
kirahisi.
MAJUKUMU YAKE
• Kuweka fedha za kikundi
• Kuhakikisha usalama wa fedha na mali
za kikundi
• Kutayarisha mahesabu katika sanduku
la fedha na kusimamia mienendo yote
ya shughuli za kibenki.
• Kuhakikisha sanduku limefungwa
baada ya mkutano wa kikundi
• Kuhakikisha marejesho yanatolewa.
• Kutunza kumbukumbu zote za fedha
za kikundi
• Kugonga mihuri kwenye vitabu vya
Hisa.
• Kutoa taarifa ya mapato na matumizi
mwisho wa kufunga mwaka wa
kikundi.
• Kulipa fedha zinazo potea ikibainika
kuwa kamati ya uongozi wa kikundi
imehusika.
WAHESABU FEDHA
SIFA
• Mwenye kupatikana kila wiki kwenye
vikao vya kikundi
• Awe mwaminifu
• Awe menye busara na kauli nzuri
• Mwenye kujua kusoma, kuandika na
kuhesabu kwa ufasaha.
• Asiwe mdokozi na ambaye amewahi
kuhusishwa na mambo ya utapeli.
MAJUKUMU
• Kuhesabu na kuthibitisha fedha zinazo
ingia na zinazotoka kwenye sanduku
kabla na baada ya kukusanya fedha
• Kutoa taarifa ya jumla ya fedha zote
kwa mwenyekiti kabla ya makusanyo
na baada ya makusanyo.
• Kupokea fedha zote zinazo wekwa
katika kikundi kuanzia hisa, mikopo na
marejesho na ziada ya mikopo.
33
• Kulipa fedha zinazo potea ikibainika
kuwa kamati ya uongozi wa kikundi
imehusika.
Kikundi kitakuwa na wajumbe wanne wenye dhamana maalumu na ambao ni washika
funguo watatu na mjumbe mmoja mtiaji saini kwenye hundi ya kikundi wakati wa
kuchukua fedha benki. Wajumbe hawa hawatakuwa viongozi na watakuwa na
dhamana maalumu na inashauriwa wawe na sifa zifuatazo:
WASHIKA FUNGUO
WASHIKA FUNGUO
SIFA
Mwanakikundi mwenye uwezo wa
kuhudhuria mikutano kila wiki
Mwenye nyumba yenye usalama
na uaminifu.
Mwenye kumbukumbu nzuri
Mwaminifu na mnyenyekevu
MAJUKUMU YAO
Kuwa mdhamini wa funguo
Kuwasilisha funguo katika kila
mkutano
Kuhakikisha sanduku linafunguliwa
na kufungwa kila siku ya mkutano.
Kulipa gharama ya kufuli na
nyinginezo iwapo atapoteza
funguo za kikundi
MTIAJI SAINI
SIFA
Awe mwaminifu.
Mwenye hekima, busara na mcha
mungu
Asiwe mwenye dhiki
Awe mkweli, mwazi na mpenda
haki
Awe mwenye msimamo
Majukumu yake
Kuchukua fedha kwa kushirikiana na
wajumbe wengine benki au kusaini
kwenye hundi ya kikundi inapobidi.
34
MADA YA PILI: UCHAGUZI WA KAMATI YA KUDUMU YA UONGOZI WA KIKUNDI
Baada ya kujifunza na kutambua sifa na majukumu ya kila kiongozi uchaguzi wa
kamati ya uongozi ya kudumu utafanyika.
• Wanakikundi watajikumbusha sifa, na majukumu ya kila mjumbe wa kamati ya
uongozi
Kwa kawaida kwenye vikundi vingi washiriki hupenda kukwepa majukumu kwa
kutokubali kuchaguliwa na vyema ikaelezwa wazi kwamba mtu ambaye atajiona yeyé
apendi kuwa kiongozi kwa sababu zake binafsi basi hatastahili kuwa mwanakikundi
katika kikundi. Kila mwanachama anadhamana ya kuhakikisha kikundi kinatimiza
malengo yake na nivyema kila mjumbe akafahamu kuwa siku itakapo wadia
atawajibika kukiongoza kikundi.
Wakati mwingine pia washiriki huchagua viongozi mapema kabla ya kutambua sifa
zao au wakati mwingine viongozi kujishinikiza wao wenyewe kutokana na maslahi yao
binafsi.
Mwezeshaji ni lazima ahakikishe uchaguzi unafanyika tena na wajumbe wenye sifa
kuchaguliwa kushika nafasi zinazo takiwa na nivyema suala la kuchagua viongozi
lisiingiliane na masuala ya siasa na dini maana kuviingiza vitu hivyo kutaathiri kama siyo
kuvunja kabisa kikundi.
Uchaguzi utafanyika kwa washiriki
• kupendekeza majina ya wagombea kwa kila nafasi
Washirika watapiga Kura kwa kila nafasi na kura zitapigwa kwa nafasi moja na baada
ya kukamilika wajumbe watapendekeza majina ya nafasi inayofuata na inashauriwa
uchaguzi uanze wa mwenyekiti wa kikundi.
Mwezeshaji ahakikishe wajumbe waliochaguliwa wanaweza kufanya kazi na kama
sivyo ni vyema aingilie kati na kueleza umuhimu wa kazi na sifa zinazohitajika.
Mwezeshaji wapongeze wanakikundi waliochaguliwa kushika nafasi mbalimbali katika
kikundi na watakie mafanikio mema katika kazi zao na wanakikundi wote wajipongeze
kwa kukamilisha zoezi hilo kwa amani na upendo
35
MADA YA TATU: MAMLAKA
Kipindi cha uongozi ni mwaka mmoja ambapo kikundi kitafanya tena uchaguzi mkuu
wa kubadilisha wajumbe wa kamati ya uongozi.
Kiongozi haruhusiwi kukaa madarakani zaidi ya awamu mbili za uongozi na hii ni
kuonyesha kwamba mfumo huu unahitaji kila mwanakikundi ashike nafasi ya uongozi
ndani ya kikundi. Katika mkutano mkuu ndio uchaguzi wa viongozi wapya na ambao
wanamajukumu ya kuongoza, kuendesha na kusimamia fedha pamoja na shughuli
zote za kikundi watapatikana.
Lengo la mamlaka ni kuwaidhinisha wajumbe wa kamati ya uongozi kufanya kazi zao
zilizoamuliwa na kukabidhiwa. Pia inasaidia kuweka mipaka kwa baadhi ya viongozi
wanaofikiri kuwa wenye uwezo wa maamuzi ya kupindukia katika jamii ni wao.
4.3.1. Taratibu za kuachia madaraka
Kama ilivyo elezwa hapo awali viongozi wa kikundi watakuwa wanabadilishwa kila
mwaka ili kuonyesha ufanisi wa kikundi. Katika mkutano mkuu wa mwaka baada ya
kutangaza hesabu za kikundi na wajumbe wote kuridhia taarifa iliyotolewa na uongozi
ulio pita hatua itakayo fuata ni kufanya uchaguzi wa viongozi kwa kuwapigia kura
wajumbe walio kuwa madarakani maana inashauriwa kila mwaka viongozi watatu
lazima wapunguzwe na nafasi zao zijazwe na wajumbe wapya watakao chaguliwa.
Wajumbe watapiga kura kwa kuandika majina ya viongozi gani wangependa
wapumzishwe na viongozi gani wangependa wabaki. Kati ya viongozi watakao takiwa
kutoka ni lazima kuwe na wajumbe kwenye nafasi ya mwenyekiti, au Katibu au
mwekahazina atakaye ondolewa. Lengo la kufanya mabadiliko haya ni kuongeza
ufanisi katika kikundi na kuleta hali ya uwajibikaji miongoni mwa wanachama maana
kikundi ni mali ya wanachama wote. Mwaka utakao fuata wale viongozi walio baki
wataondoka na nafasi zao zitajazwa na wajumbe wengine watakao chaguliwa.
36
SEHEMU YA TANO
SHERIA ZA KIKUNDI
Lengo:
• Kuelezea umuhimu wa sheria katika kikundi.
• Kuwasaidia wanakikundi kuandaa sheria zao
VIFAA
• Bango kitita
• Kalamu
• Ubao
MUDA: 1.30
MBINU ZA KUFUNDISHIA:
• Kuwasilisha mada
• Majadiliano
• Maswali na majibu.
• Mifano
1. MAANA YA SHERIA
Sheria ni mustakabali, taratibu na kanuni zilizokubalika na wanachama ili kuongoza
kikundi. Kuheshimu sheria hizo ni muhimu kwani ndio muhimili wa kufikia malengo ya
kikundi.
Wanakikundi ni vyema wakatambua kuwa sheria walizozitunga ni zao kwa hiyo
wanaweza kuzibadilisha kulingana na mahitaji au kuongeza wakati itakapobidi, ila
sheria hizo zisiwe kinyume na taratibu za uendeshaji wa mfumo wa vikundi vya VICOBA.
Baada ya sheria kuanzishwa ni lazima sheria hizo ziandikwe kwa lugha ambayo kila
mwanakikundi ataweza kuzisoma na kuzifuata. Hivyo ni muhimu kila mwanakikundi
kupata nakala na zingine zihifadhiwe kwenye faili la kikundi ambapo zitapatikana
muda wowote zitakapohitajika. Ni vyema kila kikundi kikawasilisha nakala ya sheria
katika ofisi za serikali za mitaa au katika ofisi za watendaji wa vijiji ili vikundi viweze
kutambulika. Mfumo wa VICOBA hadi sasa hautambuliki kisheria na matokeo yake
37
baadhi ya vikundi vimesajiliwa chini ya mamlaka ya biashara yaani Brela, wengine
Ushirika, wengine mambo ya ndani na matokeo yake kujiingiza katika sheria hizo
baadhi ya vikundi vimepoteza mueleko vingine vingi vimesambaratika kabisa. Serikali
inawajibu wa kuandaa sheria itakayo weza kuandaa utaratibu wa vikundi vya VICOBA
kutambulika na hii itasaidia kulinda uhalisia wake. Ikumbukwe kuwa vikundi vya
VICOBA vimeenea na vinaongezeka na tathimini iliyo fanyika mwaka jana mwezi
decemba jumla ya shilingi bilioni 24 zinazunguka ndani ya vikundi.
Hadithi.
Juma ni mwanakikundi katika kikundi cha Sonaka na huudhuria mara chache kwenye
vikao, lakini kwa kawaida hupeleka fedha za michango kwenye kikundi kwa
kumuagiza mwanakikundi mwenzake. Siku ya Ijumaa Juma alikuwa na shughuli ya
jamaa yake ambayo ilikuwa ni siku ya mkutano wa kikundi. Kama kawaida Juma
alipeleka hisa yake yenye thamani ya shilingi 1000/= kwa kumpa jirani yake na
akamtaka amwombee na mkopo wa shilingi 100,000/= katika kikundi ilikuchangia
shughuli ya rafiki yake.
Kwa kuwa Juma alikuwa hahudhurii kwenye kikundi mara kwa mara, wiki iliyopita
wanakikundi walifanya mabadiliko ya sheria za kikundi ambazo zilikuwa hazifanyi kazi
na hazikidhi kwa wakati huo. Kutokana na mabadiliko hayo wanachama walimkatalia
mjumbe aliyetumwa na Juma ombi la mkopo na kumrudishia hisa yake ya shilingi
1000/=.
Mwezeshaji au kiongozi wa kikundi wape nafasi wanakikundi kujadili kwa dakika tano
na maswali yafuatayo yanaweza kuwaongoza.
• Je unadhani ni kwanini walimrudishia ?
• Je unahisi nini kilitokea ?
38
VIPENGELE VYA SHERIA ZA KIKUNDI
1. Jina na anuani
2. Malengo ya ya kikundi
3. Mamlaka ya kikundi.
4. Sifa za mwanakikundi
4.1. Jinsia
4.2. Umri
4.3. Makazi
4.4. Afya
5. Taratibu za kujiunga katika kikundi
6. Wajibu wa mwanakikundi
7. Mrithi
7.1. Taarifa za mrithi
7.2. Taratibu za kubadilisha mrithi
7.3. Idadi ya warithi wanaoruhusiwa kuandikwa kwenye daftari la kikundi
7.4. Mafao anayo stahili mrithi
8. Kufukuzwa/kusimamishwa ndani ya kikundi
8.1. Matukio yatakayo msimamisha/kufukuzwa mwanakikundi
8.2. Haki za mwanakikundi aliyefukuzwa
8.3. Muda wa kuzilipa haki za mwanakikundi aliyefukuzwa
8.4. Mwanachama asipo hudhuria mara ngapi mfululizo bila taarifa atakuwa
amejifukuzisha ndani ya kikundi.
9. Ukomo wa mwanakikundi
9.1. Taratibu za kufuata iwapo mwanakikundi atajitoa katika kikundi.
9.2. Taratibu za kupata haki za mwanakikundi aliyejitoa
9.3. Muda wa kupewa mafao anayostahili
10. Uwanakikundi utasitishwa kwa:
10.1. Kutohudhuria mara nne mfululizo
10.2. Kutoa siri za kikundi
39
10.3. Kuchonganisha
10.4. Kutonunua hisa mara nne mfululizo
11. Taratibu za mfuko wa Hisa
11.1. Idadi ya hisa ambazo mwanakikundi anaruhusiwa kununua ni hisa moja
hadi hisa Tano.
11.2. Thamani ya hisa moja ni tsh?.
11.3. Kiasi cha faini kwa watakao shindwa kununua hisa?
12. Mikopo ya Hisa
12.1. Taratibu za kurejesha mkopo
12.2. Viwango vya Riba/ziada ya mkopo
12.3. Taratibu za kufuata kwa wanakikundi watakao shindwa kurejesha mkopo.
12.4. Wajibu wa wadhamini (5) wa kikundi kidogo iwapo mkopaji ameshindwa
kurejesha mkopo.
12.5. Vigezo vitakavyo weza kuchuja wakopaji iwapo fedha hazitoshi
sandukuni
12.6. Jinsi ya kutathimini uwezo wa mkopaji
12.7. makosa gani yatamwezesha mwanachama kupewa mkopo kiasi kinacho
lingana na hisa zake au mara mbili ya hisa zake.
13. Bima ya mkopo.
13.1. Kiwango cha kuchangia katika mfuko wa bima inashauri aslimia mbili
13.2. Mfuko wa Bima utafanya kazi iwapo mwanakikundi amefariki na deni la
Mkopo wa Hisa.
13.3. Iwapo bima haitatosha kufidia deni kiasi cha fedha kitakatwa kutoka
kwenye mfuko wa Ziada ya mikopo kabla ya kugawana mwisho wa
mwaka.
14. Mfuko wa jamii (ELIMU NA AFYA)
14.1. Kila mwanakikundi atachangia shilingi …… katika mfuko wa jamiii
14.2. Mwanakikundi ataruhusiwa kukopa mkopo usiozidi shilingi …. Katika mfuko
wa jamii na atazirudisha bila ziada ya mkopo.
14.3. Kiwango cha chini kinachotegemewa kiwepo kwenye mfuko wa jamii
ndani ya kikundi kwa wakati wowote kwa dharula ni shilingi………….
14.4. Mwanakikundi ataruhusiwa kukopa kwa ajili ya matatizo ya elimu na afya.
14.5. Muda wa kurejesha mkopo wa jamii
14.6. Hatua zitakazo chukuliwa iwapo mwanakikundi ameshindwa kurejesha
mkopo wa jamii kwa wakati.
14.7. Hatua zitakazo chukuliwa iwapo mwanakikundi atafariki na deni la mfuko
wa jamii.
40
15. Majukumu ya Viongozi wa kikundi
16. Mambo ya kufanya katika mkutano mkuu
17. Makosa yatakayo tozwa faini.
17.1. Kutohudhuria mkutano wa kikundi bila ya taarifa mwanakikundi atatozwa
shilingi………………………..
17.2. Uchelewaji kwenye mkutano wa kikundi bila ya taarifa ni shilingi …
17.3. Mwanakikundi aliyeomba udhuru tofauti na kuuguliwa au kufiwa
atachangia shilingi ngapi kwenye mfuko wa faini?
17.4. Kuonyesha dharau kwenye kikundi
17.5. Kupoteza Kitabu
17.6. Kuzungumza kwenye mkutano bila ya ruhusa ya mwenyekiti…….
17.7. Kamati isipotekeleza majukumu yake sawasawa
17.8. Simu kuita kwa sauti kwenye mkutano
18. MENGINEYO
18.1. Mwanakikundi atakaye ugua muda mrefu ndani ya kikundi wanakikundi
watachukua hatua gani …………………..
18.2. Mwanakikundi aliye fariki mafao yake yatatolewa ndani ya siku tisini.
18.3. Iwapo mwanakikundi atafiwa atachangiwa Tsh ….. na kila mwanakikundi
wa kikundi.
18.4. Kiasi gani kitachangiwa iwapo mwanakikundi atakuwa amefariki
19. Mwanakikundi aliye fariki
19.1. Hatua zitakazochukuliwa kwa mwanakikundi aliyefariki
19.2. Haki za mwanakikundi aliyefariki
19.3. Lini haki hizo zitalipwa
19.4. Ikiwa amefariki na mkopo wa kikundi hatua zipi zitachukuliwa
20. VYANZO VYA MAPATO YA KIKUNDI
o Faini
o Ziada ya mikopo
o Na mikopo kutoka katika taasisi za fedha
o Mfuko wa Hisa
o Bima ya kikundi
41
SEHEMU YA SITA
UTUNZAJI WA KUMBUKUMBU
Lengo:
1. Kuelezea umuhimu wa kuweka na kutunza kumbukumbu za kikundi
Vifaa:
• Bango kitita
• Karamu au chaki
• Ubao wa kuandikia
Muda: 45
Mbinu za Kufundisha:
• Kuwasilisha mada
• Majadiliano
• Maswali na majibu.
• Mifano
MADA YA KWANZA: MFUMO WA UTUNZAJI WA KUMBUKUMBU
Mfumo wa VICOBA ni kama mifumo mingine ya kifedha ambayo inahitaji umakini sana
katika utunzaji wa kumumbuku na mali ya wanachama. Mfumo wa VICOBA
unahamasisha kumbukumbu kutunzwa katika makundi tofauti na hii ni kurahisha na
kuwa na uhakika pale moja ya kumbukumbu inapo someka tofauti au inapo leta utata
wa maamuzi. Katika mfumo wa VICOBA kumbukumbu zitatuzwa kwenye kitabu cha
mwanachama, Daftrai kubwa, leja ya kikundi na kutakuwa na fomu za mikopo. Kila
kundi lina umuhimu wake kama inavyo onyesha hapo chini.
KITABU CHA KUMBUKUMBU ZA MWANAKIKUNDI.
Kitabu cha kumbukumbu za mwanachama ni kitabu kinachotunza kumbukumbu za
mwanakikundi ambapo hisa, mfuko wa jamii, Bima, ziada ya Mkopo na mikopo
hujazwa ilikumrahisishia mwanakikundi kufuatilia kwa karibu mwenendo wa fedha zake
ndani ya kikundi.
Ni muhimu kwa kila mwanakikundi kuwa na kitabu kwa ajili ya kumbukumbu zake
zinazohusu hisa zake, mfuko wa jamii na mikopo. Kitabu hiki ambacho kitaandikwa
42
namba ya mwanakikundi ilikumwezesha kufuatilia mwenendo wa uwekaji wake na
mikopo yake yote.
MKUTANO WA MFUKO WA JAMII HISA
01
Kitabu hiki kinasehemu kuu mbili. Sehemu ya kwanza inatunza kumbukumbu za
makusanyo na akiba za mwanachama na sehemu ya pili inaonyesha mikopo na
kwenye mikopo kumegawanyika katika makundi Mawili. Kundi la kwanza mikopo ya
hisa na kundi la pili mikopo ya jamii. Mikopo ya hisa taarifa zifuatazo zinapatikana:
Tarehe aliyokopa mkopo, bima ya mkopo, kiasi kilichokopwa, ziada ya mkopo, kiasi
alichorejesha, salio la mkopo na sahihi ya mhazina wa kikundi husika maana ndiye
anayetakiwa kujaza katika kitabu hiki.
TAREHE BIMA KIASI CHA
MKOPO
ZIADA YA
MKOPO
KIASI KILICHO
REJESHWA
SALIO SAHIHI YA
MWEKA HAZINA
Sehemu ya pili ni mikopo ya jamii na taarifa zifuatazo hujazwa: tarehe aliyokopa, kiasi
alichokopa, kiasi alichorejesha, salio la mkopo na saini ya mweka hazina. Kitabu hiki ni
lazimia kionyeshwe wakati wa kununua hisa, kukopa mkopo na kutoa marejesho.
Wakati wa mikopo inashauriwa kitabu cha mwanachama anaye taka mkopo kiwasili
mbele au apewe mwanachama mwingine na azihesabu hisa za mkopaji husika.
TAREHE KIASI CHA
MKOPO
KIASI
KILICHOREJESWA
SALIO SAHIHI YA MWEKA
HAZINA
1. LEJA YA KIKUNDI.
Kikundi kitakuwa na Leja mbili za kumbukumbu za wanakikundi wote ambapo taarifa
mbalimbali zitaingizwa kwenye ukurasa husika. Leja ya kwanza itahusika na makusanyo
yote ya siku na taarifa zifuatazo zitapatikana kwenye leja ya kikundi nazo ni: majina ya
wanakikundi, mahudhurio ya kila wiki, kitabu cha mahesabu, hisa za wanakikundi,
mfuko wa jamii, fomu ya warithi wa mali za wanakikundi, faini inayokusanywa na leja
ya pili itajishughulisha na mikopo ya hisa na jamii ambapo kila mwanachama atakuwa
43
na ukurasa wake na taarifa mbalimbali zitaainishwa kama zinavyo onyeshwa kwenye
jedwali hapo chini.
MIKOPO YA HISA
TAREHE MUDA
WA
MKOPO
BIMA
YA
MKOPO
KIASI
CHA
MKOPO
ZIADA
YA
MKOPO
SAINI
YA
MKOPAJI
MKOPO
ULIO
REJESHWA
FAINI YA
KUCHELEWESHA
MKOPO
MKOPO
ULIo
SALIA
SAINI
YA
KATIBU
MIKOPO YA JAMII
TAREHE KIASI CHA
MKOPO
SAINI
YA MKOPAJI
MKOPO ULIO
REJESHWA
MKOPO ULIo
SALIA
SAINI YA KATIBU
2. DAFTARI KUBWA
Kufanya kazi ya kurekodi makusanyo yote ambayo yanafanyika kwa wiki husika Kikundi
kitakuwa na daftari kubwa moja ambalo litahifadhi taarifa zote za kila wiki kwa mujibu
wa makusanyo yatakavyokuwa yanafanyika. Daftari kubwa litahifadhi taarifa zote kwa
undani zaidi na hii itasaidia kuwa na usalama wa utunzaji wa taarifa nyingi ndani ya
kikundi. Daftari kubwa litahifadhi taarifa za hisa, jamii, marejesho, mikopo, faini na kutoa
taarifa ya salió la kila wiki katika kikundi.
Ushauri: Inashauriwa daftari kubwa lisihifadhiwe kwenye sanduku au kama kikundi
hakina sanduku basi aliyehifadhi vitabu pamoja na reja asihifadhi daftari kubwa.
JINSI YA KUCHORA
NAMBA JINA LA MWANACHAMA IDADI YA
HISA
THAMANI
YA HISA
MFUKO
WA JAMII
FAINI
FOMU ZA MIKOPO
Kikundi kitakuwa na fomu mbili tofauti za mikopo. Fomu moja itahusika na mikopo ya
hisa na fomu nyingine itajihusisha na mikopo ya jamii. Ni vyema mkopaji ajaze fomu
kabla ya kupewa mkopo wake kwa ajili ya kumbukumbu
44
Kutakuwa na aina kuu mbili za fomu za mikopo ambazo ni:
Fomu ya mfuko wa Hisa ambao utaeleza kwa kina jina la mkopaji, kiwango anacho
kopa, majina na saini za wadhamini na dhamana juu ya mkopo alio uomba. Fomu zote
zitakuwa kwenye faili moja.
Kutakuwa na fomu nyingine ya mfuko wa jamii ambayo itaonyesha jina la mkopaji na
wadhamini wake pia. Hii inasaidia kuonyesha kumbukumbu za kikundi na iwapo
kunatokea jambo lolote basi taarifa zisikosekane. Utaratibu utaandaliwa na kikundi juu
ya upatikanaji wa fomu na kumwezesha mwanakikundi kupata fomu pale anapohitaji
mkopo.
Kikundi kinashauriwa kutumia mfumo huu na kuepusha kuwa na makaratasi mengi au
daftari kubwa nyingi ndani ya kikundi maana karatasi nyingi huleta shida wakati wa
kufunga hesabu na muda mwingine kujaza sanduku bila sababu.
MADA YA PILI: MFUMO WA UHIFADHI WA FEDHA
BENKI.
Kutokana na hali halisi ya ukuaji wa fedha za kikundi maeneo mbalimbali na kwa
kuzingatia kanuni za fedha kila kikundi kitashauriwa kufungua benki akaunti ambayo
itawezesha kutunza fedha zake. Hatahivyo fedha hizo zitatunzwa pale tu iwapo
hapatakuwa na wakopaji ndani ya kikundi. Vikundi pia vitaendelea kuangalia umbali
wa kutoka kwenye eneo la kikundi na eneo ambalo benki ilipo na hii itasaidia
kuepusha matumizi makubwa ya nauli wakati fedha zinapopelekwa.
Hasara ya kupeleka fedha benki ni kukatwa kila mwezi na kutotolewa kwa mikopo kwa
wakati ndani ya kikundi. Hata hivyo mafunzo maalumu yatatakiwa kutolewa jinsi ya
kutunza kumbukumbu za fedha zilizopo benki na wanazozungusha mkononi.
SANDUKU
Kikundi kitakuwa na maamuzi ya kutumia sanduku na wanakikundi husika kukubaliana
sehemu ya kuhifadhi sanduku lao. Kikundi kinashauriwa kutohifadhi fedha ndani ya
sanduku au kuziweka benki na zaidi viongozi watatakiwa kuwahamasisha wanakikundi
kila baada ya makusanyo kuchukua mkopo.
Faida ya kutumia sanduku ni kuwa fedha zinapokusanywa zinaonekana na hazipelekei
wanakikundi kuwa na wasiwasi tofauti na benki ambapo viongozi wanaweza kutumia
fedha zilizopo kwenye akaunti ya kikundi bila ya idhini ya wanakikundi.
Hasara ya kutumia sanduku kuweka fedha ni rahisi kwa wezi kuliiba hasa kama
litahifadhiwa katika maeneo ambayo siyo salama.
45
SEHEMU YA SABA
UTATUZI WA MIGOGORO
Lengo:
• Kuelimisha wanakikundi juu ya athari za migogoro katika kikundi
• Kuwaelimisha mbinu ya kutambua migogoro na hatua za kufuata ili kutatua
migogoro
• Kuchambua vyanzo vya migogoro
Vifaa:
• Bango kitita
• Karamu au chaki
• Kisimamisha ubao aubango kitita
Muda: Dakika 45.
Mbinu za kufundishia:
• Kuwasilisha mada
• Majadiliano
• Maswali na majibu,
• Hadithi
NINI MAANA YA MGOGORO
Migogoro ni hali ya kutoelewana inayotokea baina ya pande mbili au zaidi. Migogoro
inaweza kuwa kati ya mtu na mtu, mtu na kikundi au kikundi na kikundi. Bila kujali idadi
ya watu wanaogombana, mgogoro usiosuluhishwa mapema unaweza kuwa na athari
kubwa kwa mtu mmoja au kundi la watu.
Viongozi wa kikundi wanajukumu la kujenga na kudumisha hali ya amani na usalama
ndani ya kikundi, hivyo viongozi wanajukumu la kusuluhisha migogoro itakayojitokeza.
Misingi mikuu katika usuluhishi ni pamoja na:
• Kutambua chanzo cha mgogoro ni jambo la muhimu ili kuleta suluhu sahihi. Pia
inapunguza kuwepo kwa upendeleo wakati wa kusuluhisha.
• Ni muhimu pia kutoa nafasi ya kila pande katika mgogoro kutoa maelezo yao juu
ya mgogoro husika, bila kujali nani ni chanzo cha ugomvi. Haki ya kusikilizwa na
kujieleza ni haki ya msingi kabla ya kusuluhisha mgogoro.
46
• Msuluhishi kutokuwa upande wa mtu yeyote na kuto onyesha upendeleo.
• Kabla ya kuanza usuluhishi ni muhimu kwa msuluhishi kubainisha lengo kubwa la
usuluhishi huo pamoja na wahusika wa mgogoro ambao ni kupatanisha pande
husika na si kuongeza ukubwa wa tatizo.
• Kutoa nafasi kwa wanakikundi kutoa maoni yao juu ya mgogoro na athari ya
mgogoro huo kwa kikundi iwapo hautasuluhishwa na kuwaomba kupendekeza
suluhisho la mgogoro husika.
MADA YA KWANZA: VYANZO VYA MIGOGORO KATIKA VIKUNDI.
Waombe washiriki kutaja vyanzo vya migogoro.
Kati ya mambo yatakayo tajwa ni pamoja nai:
• Kutotekelezwa kwa sheria ipasavyo
• Viongozi kutotambua majukumu yao
• Kukosekana kwa elimu sahihi ya shughuli husika
• Majukumu ya kikundi kuachwa kwa watu wachache
• Kuwepo kwa makundi ndani ya kikundi
• Kuwepo kwa chuki binafsi miongoni mwa wanakikundi
• Kuwepo kwa dharau baina ya wanakikundi wenye kipato kikubwa na wenye kipato
kidogo
• Kusengenyana
• Kutokuwa wa wazi
• Uchu wa madaraka
• Wivu
• Ubinafsi
• Kuwa mjuaji kupita kiasi
• Ukabila, udini na u vyama.
• Wawezeshaji kupendelea wakati wa kufundisha
• Majungu
• Malumbano
MADA YA PILI: MATOKEO YA MGOGORO
Nini ni matokeo ya migogoro?
Majibu ni pamoja na:
• Kuvunjika kwa kikundi
47
• Kupotea kwa mali za wanakikundi
• Kuendelea kwa uhasama
• Kudhorota kwa maendeleo ya kikundi
• Kutoaminiana na kuogopana
• Kukosekana kwa amani miongoni mwao
• Kukatisha tamaa wengine kujiunga kwenye vikundi
• Kudhorotesha ustawi wa kiuchumi kwa wanakikundi
MADA YA TATU: JINSI YA KUTATUA MGOGORO.
Migogoro yote itatuliwe ndani ya kikundi na kama viongozi ndio wahusika basi
wasimamizi wa vikundi, washauri au kikundi kipendekeze nani aombwe na kualikwa ili
kutatua mgogoro wao. Wanakikundi watapendekeza mtu ambaye wanamwamini na
anayekubalika pande zote mbili na ambaye atawaongoza kutatua mgogoro bila ya
upendeleo.
Msuluhishi wa mgogoro anashauriwa asiwe msemaji mkuu katika kutatua mgogoro huo
bali jukumu lake kuu liwe ni kuwaelekeza na kuwaongoza wajumbe katika kufikia suluhu
ya tatizo lao.
1. WAKATI WA KUTATUA MGOGORO HATUA ZIFUATAZO ZINAWEZA KUTUMIKA
1. Wahusika kulielezea tatizo
2. Kusikiliza pande zote ili kubaini chanzo cha mgogoro husika
3. Kuweka mapendekezo ya suluhu ya tatizo husika
4. Kutathimini mapendekezo yaliyo tolewa
5. Kuchagua pendekezo zuri zaidi
6. Tathimini matokeo ya mgogoro husika
7. Kuandaa mpango wa hatua ya jinsi ya kutatua tatizo hilo
Baada ya kutatua mgogoro ni vyema wajumbe wote wakapongezana na kuondoa
tofauti zote ambazo zilikuwepo miongoni mwao ili zisitokee tena. Wajumbe
wajipongeza kwa kushikana mikono.
Hadithi.
Katika kikundi cha mali asili mwanachama mmoja Koini alikopa mkopo wa shilingi
100,000/= za kikundi katika mfuko wa Hisa. Lengo la mkopo huu lilikuwa ni kuendeleza
biashara yake ya kupika vitafunwa. Sehemu kubwa ya fedha alizokopa zilitumika
kwenye harusi ya mwanae. Ilipofika muda wa kurejesha mkopo koini hakwenda
mkutanoni kwa vile hakuwa na fedha za kulipa mkopo wake. Siku iliyofuata aliwasikia
48
wanakikundi wawili wakiwasimulia watu wengine hadithi yake kisimani. Alipofika
nyumbani Koini alimsikia mke mwezie akimdhihaki. Koini alifahamu kuwa hadithi yake
imeenea kijiji kizima na aliamua kuinyamazisha kwa kukopa fedha kwa rafiki yake pale
pale kijijini na kulipa deni lake lote kwenye kikundi na kisha akaandika barua ya kujitoa
kwenye kikundi.
Tumia maswali yafuatayo baada ya kusimulia hadithi
• Unafikiri hadithi hii ina ujumbe gani?
• Unadhani Koini angelifanya nini?
• Wanachama wa kikundi wamefanya vizuri?
• Unadhani wanakikundi wangefanya nini?
• Kwa nini haya yote yalitokea?
• Je unadhani kikundi kingependekeza shauri gani kama ni suluhisho?
• Wanachama wafanye nini kuzuia migogoro kama hii isitokee ?
• Je mkopo upi unanafuu kati ya mkopo wa mtu binafsi au mkopo kwenye
kikundi?.
Mwezeshaji hitimisha hadithi hii kwa kutatua mgogogoro uliojitokeza kwa kufuata njia
ambazo wanakikundi wamejifunza katika somo hili. Muhimu katika utatuzi wa mgogoro
huu wanakikundi wa kaanza na chanzo, matokeo ya mgogoro na hatua za kutatua
mgogogoro.
2. UFUPISHO WA MWEZESHAJI
Migogoro yote itatuliwe ndani ya mkutano wa kikundi na wanakikundi wote wanahaki
ya kutoa mawazo yao kwenye mkutano wa kutatua mgogoro. Mjadala utaanza mara
baada ya shughuli za kibenki kumalizika na sanduku liwe limefungwa na kuondolewa
sehemu ya kikao. Kama muda hautatosha wanakikundi wanaweza kupendekeza
muda mwingine na ikubaliwe na robo tatu ya wanakikundi wote wa kikundi.
49
UENDELEVU WA VIKUNDI
UTANGULIZI
Mfumo wa VICOBA ni mfumo endelevu ambao unahamasisha vikundi kufunga hesabu
kila mwaka na kuhamisha taarifa za fedha kutoka mwaka mmoja na kwenda mwaka
mwingine. Kikundi kinapo anzishwa mikopo huwa midogo na baada ya miezi sita na
kuendelea Viwango vya mikopo hukua na kuwawezesha wanachama wa kikundi
husika kupata mitaji ya kuweza kuendeleza na kukuza biashara zao hasa katika
ulimwengu huu wa ushindani.
Mjadala wa kugawana au kutogawana fedha zilizo changwa na kuwekeza kwenye
kikundi kila mwaka. Kunamaswali mengi tunatakiwa kujiuliza kabla ya kufanya
maamuzi na kutoa hitimisho na maswali haya ni pamoja na:
• Malengo ya kuanzisha kikundi hiki yalikuwa ni yepi
• Malengo hayo yamefikiwa
• Kama tuna gawana fedha kunahaja gani ya kuanza tena
• kwanini tuliamua kuanzisha kikundi
• Pia ni vyema kujiuliza sababu za kiuchumi je kiasi nilicho anza kukopa mwaka
uliopita na nikikopa leo nitakuwa na uwezo wa kuanzisha au kupanua biashara
yangu.
Baada ya majadiliano hayo wanakikundi wakubaliane kama watakuwa
wanagawana kila kitu kila mwaka au
WAKATI WA KUFUNGA HESABU ZA KIKUNDI
Kikundi kitafunga hesabu kila baada ya wiki 52 ambazo sawa na mwaka mmoja na
wanachama watagawana faida iliyopatikana kutokana na mikopo inayorejeshwa na
ziada. Mfuko huu utagawanywa kwa wanachama kila mwaka na mifuko mingine
itaendelea mwaka unaofuta. Mifuko itakayo endela ni pamoja na Mfuko wa Hisa,
Jamii na Bima.
Mifuko hii ndiyo mifuko inayoimarisha kikundi na kuwawesha wanachama wa kikundi
kukopa zaidi. Kwa wastani kwa sasa ndani ya vikundi vya VICOBA wanachama
wanakopo fedha hadi shilingi za kitanzania milioni miamoja akiwa na hisa zenye
thamani ya shilingi milioni thelasini na tano. Fedha hizi zinatokana na kudunduliza kila
wiki wanapo kutana na hatimaye mwanachama hujikuta amewekeza kiasi hicho.
50
Baada ya kufunga hesabu kikundi kinashauriwa kubadilisha leja, daftari kubwa na
taarifa zake kuzihamishia kwenye vitabu vipya vya kikundi. Hii ni kupunguza uwezekano
wa wanachama kushindwa kufunga hesabu ambapo zinaweza kuwayumbisha kama
uwezo wao wa kuweka na kutunza hesabu ni mdogo.
MAMBO YA KUZINGATIA
Ili kikundi kiweze kuwa endelevu ni vyema mambo yafuatayo yakazingatiwa.
Sheria. Wanachama ni vyema wakazingatia sheria zao kikamilifu na wale wote wanao
kaidi ni vyema wakatolewa katika vikundi na nafasi zao kujazwa na wanachama
wengine au kuachwa wazi.
Urejeshaji wa Mikopo. Kila mwanachama majukumu na wajibu wa kurejesha mkopo
wake kama kanuni na taratibu za VICOBA zinavyo eleza na wale ambao
wanashindwa kurejesha ni vyema hatua zikachukuliwa dhidi yao.
Mahudhurio. Kikundi hakiwezi kuwa kikundi kama hakutakuwa na wanachama wanao
hudhuria vikao kama inavyo takiwa. Mfumo wa VICOBA unahamasisha sana
mahudhurio na sababu ya msingi ni kwamba maamuzi yote ya kikundi hutolewa na
wanachama wa kundi husika.
Usalama wa Kikundi. Usalama wa mali na fedha za kikundi upo chini ya wanachama
wa kikundi husika cha watu thelasini. Wawezeshaji, waratibu na wasimamizi hawahusiki
kwa namna yoyote na fedha za kikundi hasa katika kuzihifadhi, kuzikusanya na hata
kuziunganisha kwenye mfuko wa pamoja. Fedha za wanachama zitaendelea
kusimamiwa na kikundi husika na kama vikundi vitaamua kuungana basi kati ya
mambo ya kuzingatia na ambayo kikundi hakipaswi kuyafanya ni kuchukua fedha za
kikundi kuhifadhi katika akaunti ya umoja. Kikundi kitakuwa ni mwanachama kitatakiwa
kulipa na kutoa michango kama katiba ya umoja itakavyoeleza na umoja wa vikundi
hauta kuwa na mamlaka ya kuvishawishi vikundi kuhifadhi au kukusanya fedha za
kikundi kuweka kwenye akaunti za umoja.
51
FOMU YA UFUATILIAJI WA MAENDELEO YA KIKUNDI.
Maswali ya mwongozo wakati wa kutembela vikundi
1. Je wanachama wanaudhuria kwenye kikundi ipasavyo
2. Je wanachama wote wananunua hisa ipasavyo
3. Wanachama wote wanachangia jamii kama ilivyopangwa
4. Je kamati ya uongozi inawajibika
5. Je kumbukumbu zinajazwa kama inavyo takiwa
6. Kuna matatizo yoyote uliyo yabaini katika uendeshaji wa kikundi
7. Je vitabu vya hisa vinajazwa kama inavyo takiwa
8. Je leja zinajazwa na kuhifadhiwa ipasavyo
9. Je datfari kubwa linajazwa
10. Je kikundi kinahitaji msaada wowote wa kiutalaam
11. Je wanachama wanazingatia na kuzifuata sheria zao
12. Matatizo gani yanakisumbua kikundi
13. Kikundi kinatembelewa mara ngapi.
14. Makusanyo Hisa……………..… Jamii ……………..……….
15. Marejesho ya Hisa…………………. Jamii…………………………..
16. Mikopo ya hisa……………………….. Jamii………………..…..
Angalizo. Mwezeshaji unapo tembela vikundi jiepushe na kukaa kwenye meza ya
mbele au kuingilia shughuli za kikundi husika. Mwezeshaji kaa pembeni ambapo
patakuwezesha kuona wanachama wote na viongozi wa kikundi. Kwa muda wote
utajiuliza maswali na kupata majibu kwa kuona na kama majibu mengine
hayatapatikana basi baada ya shughuli zao kukamilika utatakiwa kuwauliza viongozi
na wanachama wote. Mwezeshaji kisaidie kikundi kujiendesha chenyewe kwa kusisitiza
umuhimu wa kusimamia sheria na viongozi kuwajibika na kuwawajibishwa wanachama
wote wanao kiuka kanuni na taratibu za kikundi husika. Baada ya kufanya tathimini
yako jaribu kuainisha mapungufu yaliyojitokeza na toa ushauri jinsi ya kutatua au
suluhisho ya mambo hayo.
52
TAARIFA YA MWEZESHAJI/MRATIBU WA MRADI
KILA BAADA YA MIEZI MITATU
JIna la mwezeshaji ………………………………………………..
Tarehe ………………………………………………………………
Wilaya/Kata…………………………………………………………
1. Idadi ya vikundi………………………………………………………..
2. Idadi ya vikundi vilivyo anzishwa kwa mwezi/miezi mitatu …………….
3. Taarifa ya umri wa vikundi ……………………………….
4. Je vikundi vinavunja mzunguko au avivunji mzunguko na kama vinavunja ni vingapi
5. Je umewahi kuomba msaada wa kutatua matatizo kutoka kwa mratibu wako wa
mradi …………………………
6. Matatizo gani yamekuwa sugu katika vikundi…………………………
7. Matatizo haya yanatatuliwaje katika vikundi…………………………..
8. Unatoa mapendekezo gani juu ya matatizo ya mara kwa mara yanayo jitokeza
9. Msaada gani wa ziada ambao unahitajika ……
10. Kunafulsa gani ambazo zinaweza kusaidia katika kuboresha maendeleo ya vikundi
11. Je kunataasisi nyingine zinazo fanya kazi na vikundi na kama zipo zinaitwaje na
zinatoa huduma gani.
12. Unamapendekezo gani ili kuboresha maendeleo ya vikundi kwa ujumla
13. Mafanikio gani wanachama wameyapata kutokana na kujiunga na vikundi vya
VICOBA. Onyesha vielelezo kama vipo kwa mfano picha na visa mkasa.
14. Je vikundi vinafedha kiasi gani. Onyesha kwa kuchora duara kama lifuatalo
JINA LA KIKUNDI HISA JAMII BIMA JUMLA
Angalizo. Waratibu, wawezeshaji na wasimamizi wa vikundi hawana muda wa kukaa
na kufuatilia shughuli za vikundi na muda mwingi wanapita kukusanya ripoti bila kushiriki
na kuona jinsi kikundi kinavyo fanya kazi. Waratibu ni vyema wakaheshimu pia
mikutano ya vikundi na kama kuna wageni au watu wanataka kujifunza watu hao
wafanye shughuli zao ndani ya ratiba za mikutano ya kikundi husika. Kubadilisha
mikutano ya kikundi kwa maslai ya watu wan je hairuhusiwi.
53
Mwandishi wa mwongozo huu ni Evance Chipindi ambaye amekuwa katika
shughuli za uendeshaji wa vikundi vya VICOBA kwa zaidi ya Miaka kumi na moja.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment