Search This Blog

Monday, 26 September 2016

FAIDA ZA KUJIUNGA NA VICOBA

FAIDA ZA KUJIUNGA NA VICOBA

1. Kupata fulsa ya mafunzo ya KUJITAMBUA,FEDHA,UJASILIAMALI na UWEKEZAJI na kukuwezesha kushiriki katika shughuli za kiuchumi na uzalishaji mali kwa mtizamo chanya, uelewa na ujuzi mkubwa.

2. Kupata fulsa ya kukutana na watu mbalimbali toka vicoba, serikalini, sekta binafsi, wabia wa vicoba nk katika mafunzo, mikutano, semina, makongamano, uzinduzi na sherehe mbalimbali na kubadilishana ujuzi, mbinu na uzoefu katika shughuli za kifedha, kiuchumi, kijamii na mfumo mzima wa maisha ya kila siku na maendeleo endelevu ndani na nje ya nchi.

3. Kupata fulsa za huduma za fedha kama vile;
    i) kuwa na akiba yako
   ii) kuwa na mfuko wako wa jamii
  iii) kupata mkopo kwa urahisi
  iv) kuwa na bima
   v) kupata mfumo wa malipo kwa urahisi (kielektroniki nk)

4. Kupata fulsa ya kuwa mwalimu wa vicoba na kuwafundisha wengine mfumo wa VICOBA endelevu, kujitambua na kujitegemea, ujasiliamali na fedha.

5. Kupata fulsa ya kupata taarifa za Vicoba, sekta za Fedha na taarifa mbalimbali za maendeleo ya uchumi na za kijamii

Umuhimu wa vikoba kwa wananchi wa kipato cha chini

UTANGULIZI Takribani miaka 23 sasa tunashuhudia ukuaji mkubwa wa huduma za kifedha na mifumo mbalimbali ikiibuliwa na kuainishwa kwa wanajamii mbalimbali hasa walio katika kipato cha chini na cha kati. Japo mifumo ya kifedha imekuwa ikiongezeka vado taratibu na mifumo ya upatikanaji wa huduma hiyo kwa watu wengi wa kipato cha chini imekuwa ni tatizo hasa kutokana na msharti magumu. Masharti magumu ya upatikanaji wa huduma ya kifedha yanawafanya watanzania wengi kutonufaika na huduma za kifedha na matokeo yake kundi kubwa la watu wenye kipato cha chini kuendelea kuwa na umaskini uliokisiri. Masharti hayo ni pamoja na riba kubwa, gharama za maombi ya mikopo, kitangulizi cha mkopo, salio kwenye akaunti, dhamana isiyohamishika, kuapa mahakami na masharti mengine mengi. Kuanzishwa kwa vikundi vya VICOBA kumesaidia wananchi mbalimbali wakiwemo wenye kipato cha chini na cha kati waishio mijini na vijijini kuweza kunufaika na huduma za kifedha pamoja na za kijamii. Huduma zimekuwa zikiongezeka siku hadi siku kutokana na ukuaji wa mitaji ya kikundi na Viwango vya mikopo ndani ya vikundi. Mwongozo huu utamsaidia mtumiaji kuelewa vizuri maumbile na taratibu za uendeshaji wa vikundi vya VICOBA. Mwongozo huu umeandaliwa baada mfumo wa VICOBA Tanzania kutimiza miaka kumi kuanzia mfumo huu uanzishwe mwaka 2002 na utatumika kwa vikundi vyote vya VICOBA, IR-VICOBA, BENKIMANI na wadau mbalimbali wanaendesha na kusimamia vikundi katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi. CHIMBUKO LA MFUMO Mfumo wa VICOBA ulianzishwa mwaka 2002 kwa mara ya kwanza na shirika la Intereligious Council for Peace of Tanzania (IRCP) na kwa kipindi hicho shirika likijulikana kama World Conference on Religion for Peace (WCRP). Shirika la IRCP lilianzisha mfumo huu kwa mara ya kwanza kama mpango wa majaribio eneo la Ukonga mazizini wilaya ya Ilala Mkoa wa Dar es salaam na wilaya ya Kisarawe mkoa wa pwani ambapo vikundi vilianzishwa katika maeneo ya Kisarawe, Masaki, Sungwi na Kifuru. Shirika liliamua kufanya majaribio haya katika eneo la Ukonga na kisarawe ili kubaini umadhubuti wa VICOBA kati ya maeneo ya mjini na maeneo ya vijini. Mwaka 2006 IRCP walifanya tathimini na matokeo yalionyesha mfumo unafanya vizuri lakini Ukonga ilifanya vizuri zaidi kwa sababu ya mzunguko wa biashara za wanakikundi na mzunguko wa fedha wa Ukonga ulikuwa mkubwa ukilinganisha na kisarawe. 6 UTEKELEZAJI WA MRADI WA MAJARIBIO Katika utekelezaji wa mradi huu kwa upande wa Ukonga IRCPT waliingia ubia na UYACODE na kwa upande wa kisarawe waliingia ubia na KIYODENI. Dhumuni kubwa la kuingia ubia na taasisi hizi lilikuwa ni kuufanya mradi kuwa imara na endelevu na hasa mradi utakapo kwisha muda wake. Taasisi hizi zilishirikiana na IRCPT katika uhamasishaji ngazi ya jamii na maeneo ya taasisi hizi yalitumiwa na vikundi kukutanika na kufanya shughuli zao. Mfumo ulifanyiwa maboresho mbalimbali kulingana na mazingira ya kitanzania na kuufanya kuwa endelevu zaidi. Maboresho yaliyofanyika baada ya kuanzishwa na IRCPT ni pamoja na kuanzishwa kwa mfuko wa Bima, kushauri Viwango vya Ziada ya mikopo, vikundi kutovunja mzunguko kila mwaka kwa kugawana kila kitu badala yake kugawana faida tu kila mwisho wa mwaka, mfumo wa urejeshaji wa mikopo, muda wa urejeshaji wa mikopo, idadi ya hisa kuongezeka kutoka hisa moja hadi hisa tano na uboreshaji mfumo wa utunzaji wa kumbukumbu. Maboresho hayo yameufanya mfumo huu kuwa imara, na endelevu na kuweza kuonyesha mafanikio makubwa na ambayo hayakutarajiwa. Mafanikio haya ni pamoja na ukuaji wa Viwango vya mikopo, ukuaji wa uelewa wa uwekezaji na nidhamu ya urejeshaji wa mikopo. Wanachama wa vikundi wameweza kuboresha biashara, kujenga nyumba, kupanua miradi, kusomesha watoto na wengine wameweza kulipia huduma ya bima ya afya (CHF) na ni jambo ambalo halikuwepo kabla ya kujiunga kwenye vikundi vya VICOBA. Mafanikio haya yamechangiwa sana na mafunzo ya kina ya uendeshaji na usimamiaji wa vikundi vya VICOBA ,ushirikiano wa wanakikundi, sheria za kikundi, uwajibikaji wa viongozi, uwazi katika uendeshaji wa shughuli za kikundi, utunzaji wa kumbukumbu, ufuatiliaji wa wawezeshaji na uwajibikaji wa kila mwanachama katika shughuli za kikundi. MADHUMU YA KUANZISHWA KWA MFUMO WA VICOBA VICOBA ni Benki Jamii Vijijini na kwa kingereza ni Village Community Banks. VICOBA ni mpango wa kujenga uwezo wa ki-uchumi na ki-jamii kwa kutumia rasilimali za wananchi zinazowazunguka. Mfumo huu huwawezesha wananchi kujiunga katika vikundi na kuanzisha mfuko wa kukopeshana kwa ajili ya miradi ya kuingiza kipato na kutatua matatizo ya dharura yanayowakabili hasa matatizo yanayohusu elimu na afya. Mifuko hii hujengwa kwa njia ya kununua hisa na kuchangia mfuko wa jamii kila wiki. 7 Mradi huu ulipoanzishwa na IRCPT ulijulikana kama mradi wa Mtoto Nuru VICOBA ukiwa na malengo ya kuleta matumaini kwa vijana, wanawake na makundi yaliyotengwa kwa njia ya kuwekeza na kupata mitaji ya kuendeleza na kuanzisha miradi/biashara mbalimbali ili kupambana na umaskini, kusaidia watoto yatima na watu waishio na Virusi vya Ukimwi. MATOKEO YA TATHIMINI. IRCPT mwaka 2006 walifanya tathimini ambayo ilionyesha mfumo wa VICOBA ni mfumo imara, rahisi na endelevu hasa katika kukusanya rasilimali za wananchi na usimamizi wake. Mfumo huu ulionyesha jinsi unavyojiendesha kwa uwazi hasa katika kufanya maamuzi na taratibu za uendeshaji ambazo hufanywa kila wiki kwenye kikao kinacho hudhuriwa na wanachama wote. Tofauti na mifumo mingine mfumo wa VICOBA maamuzi hutolewa na wajumbe wote kwenye mkutano wa kikundi na viongozi wakiwa na majukumu ya kusimamia na kutekeleza. Vikundi 10 vilivyo anzishwa Ukonga na kisarawe mwaka 2002 vilikutwa vikiwa hai na imara. Mitaji ya vikundi ilikuwa imeongezeka, wanavikundi wapya walikuwa wamejiunga katika nafasi zilizo achwa wazi. Mikopo ilikuwa imekua, mfumo wa urejeshaji ulikuwa mzuri na mikopo yote ilikuwa ina lipwa kwa wakati. Mradi ulionekana endelevu na imara japo kuwa vikundi hivi viliachwa muda mrefu bila kupata msaada wa karibu kutoka IRCPT kutokana na sababu mbalimbali. Katika tathimini hii pia vikundi vyote vilionyesha wazi wanavikundi waanzilishi walikuwa wamefanikiwa na wanavikundi wapya walikuwa wanaonja Mafanikio. Idadi ya wanakikundi katika kila kikundi walikuwa ni 30 na hii ikionyesha walikuwa wanajiunga mara tu inapobainika kunawajumbe wamehama au kujitoa. Jamii ilionyesha kufurahishwa na manufaa na mabadiliko wanayoyapata wanakikundi wa VICOBA ukilinganisha na mifumo ya mingine. Wanawake walionekana wengi katika vikundi hivi na ambao walikuwa zaidi ya asilimia sabini na tano (75%) ya wanakikundi wote na hii ilijionyesha wazi katika vikundi vya VICOBA suala la jinsia lilikuwa siyo kikwazo. Miongoni mwa wanakikundi hawa ni pamoja na wafanya biashara, wakulima wa bustani, na wafanya kazi. Baada ya mafanikio haya taasisi mbalimbali za kidini, kiserikali na zisizo za kiserikali zimeweza kuanzisha mfumo huu katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi na ni mfumo ambao unauwezo wa kuwa na maingiliano na shughuli nyingine. 8 WADAU WANAOTEKELEZA MFUMO VICOBA TANZANIA Kwa miaka mingi sasa wadau mbalimbali wanahamashisha vikundi katika maeneo mbalimbali na miongoni mwa wadau hao ni pamoja na TEC, CCT, BAKWATA, AEE, Pathfinder International, AFRICARE, LAMP, LIWODET, MEPP, RUMAKI, Social Economic Development Initiative of Tanzania, SELL, VDSA, WWF, ORGUT, FLORESTA, ELCT(ND, ECD, Mbulu) TCRS, TANARELA, AXIOUS Foundation, WCST, ITECCO, Frankfurt Zoological Society, UYACODE, YWCA, EFG na wengine wengi. Maeneo mbalimbali ya Tanzania yameweza kufikiwa japo siyo wadau wote wanatekeleza mfumo huu kama inavyo takiwa. UMADHUBUTI WA VICOBA 1.3.1. Uanzishaji wa kikundi cha VICOBA hauhitaji mtaji. Makusanyo ya kila wiki yanayotolewa na wanakikundi ndiyo huanzisha mfuko wa kukopesha. 1.3.2. Vikundi huanzishwa karibu na maeneo ya wanachama wanayoishi hivyo hupunguza gharama ya nauli na matumizi mabaya ya muda. 1.3.3. Mikopo ya VICOBA haina ukiritimba kama fedha zipo, maana wanakikundi wanajua mwenendo mzima wa fedha za kikundi kwa sababu shughuli zote za kikikundi hufanywa mbele ya wanakikundi wote. 1.3.4. Kupitia mfumo huu wanakikundi wanatumia mikutano ya kikundi kama sehemu ya kujifunza mambo mengine kama vile elimu ya biashara, masuala ya kisheria, ukatili wa kijinsia, jinsi ya kuhudumia watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi, kuelimishana haki za kila mtu na mambo mengine ambayo wanakikundi wanaona ni muhimu kwao kuyajadili na kujifunza. 1.3.5. Mfumo wa utunzaji wa kumbukumbu ni rahisi ambao unawawezesha wanakikundi kusimamia kumbukumbu zao za fedha bila kuhitaji elimu ya juu ya utunzaji wa fedha. 1.3.6. Ziada ya mikopo inayopatikana hutolewa mgao kwa wanakikundi wote mwisho wa mwaka kwa njia ya mgao na kila mwanakikundi hupata faida kutokana na idadi ya hisa zake. MAPUNGUFU YA VICOBA 1.3.7. Viwango vya mikopo vinavyotolewa wakati kikundi kinapo anzishwa vinakuwa vidogo. Mikopo inaanza kutolewa katika kikundi baada ya kumaliza wiki nne za kuwekeza fedha. 1.3.8. Mikopo kutopatikana kwa wakati kama wanakikundi wasipo rejesha kwa wakati. 1.3.9. Mfumo wa VICOBA kutotambulika kisheria na kutokuwa na sera za uendeshaji kama mifumo mingine mfano Saccos na taasisi zingine za fedha. 9 1.3.10. Vikundi kutokupata mafunzo sahihi ya uendeshaji wa mfumo wa VICOBA hivyo vikundi kutoendeshwa kama inavyotakiwa. 1.3.11. Wawezeshaji wachache na baadhi ya watu kufundisha vikundi bila ya kupata mafunzo ya kina. TOFAUTI KATI YA VICOBA NA MIFUMO MINGINE VICOBA TAASISI NYINGINE ZA KIFEDHA Vikundi ni mali ya wanakikundi wenyewe Vikundi ni mali ya mashirika husika Mali za kikundi ni mali za wanakikundi wenyewe Mali za kikundi huwa chini ya mhamasishaji/mwenye taasisi husika Maamuzi ya kikundi yanafanywa na wanakikundi wote wakiwa pamoja Maamuzi ya kikundi yanafanywa na wanakikundi wachache (Viongozi). Wanakikundi hujenga mifuko yakukopeshana kwa kutegemea fedha zao wenyewe. Hutegemea sana misaada na michango kutoka kwa wahisani mbalimbali. Huanzishwa kutokana na malengo maalumu. Ziada ya mkopo ni mali ya wanakikundi wa kikundi husika na wanagawana mwisho wa mwaka. Riba ni mali ya taasisi husika kwa ajili ya kuendesha shughuli za taasisi husika Riba hupangwa na wanakikundi wa kikundi husika Riba hupangwa na taasisi husika 10 SEHEMU YA KWANZA KUANZISHA NA KUKUA KWA VIKUNDI VYA VICOBA Lengo: • Taratibu za kuunda kikundi • Kuonyesha vifaa vinavyo tumika • Kuelewa taratibu za uwekaji na uchukuaji wa mikopo • Kujibu maswali na kuondoa hofu Muda: Dakika 45 Vifaa: • Bango kitita • Marker pen • Flipchart stand Mbinu za kufundishia: • Kuwasilisha mada • Majadiliano • Maswali na majibu. • Mifano MADA YA KWANZA: MKUTANO WA UHAMASISHAJI KWA WANAJAMII MAELEZO YA MWEZESHAJI Mkutano huu ni mkutano wa awali kwa wanajamii husika ambao wanataka kuelewa au wanashauku ya kuujua mfumo wa VICOBA kwa undani. Mkutano huu unashauriwa uendeshwe na watu wenye ufahamu wa kina wa mfumo wa VICOBA. Mhamasishaji ni vyema kujitayarisha vizuri kwenye mikutano hiyo na vyema pia kujiepusha na ahadi ambazo hazitatekelezeka na ambazo zipo nje ya uwezo wake. Mara nyingi washiriki hupenda kumwambia mwezeshaji wamesikia na kuufahamu ujumbe na hutaka kujua mhamasishaji atawapa nini? Mwezeshaji afafanue kuwa hatawapa fedha zozote bali atatoa mafunzo kama atakuwa na uwezo huo na kama hatakuwa nao vikundi vitawajibika kumgharamia mwezeshaji wakati wa ushauri wa namna ya kuanzisha na kusimamia vikundi vitakavyo kuwa chini yake. 11 Katika mkutano huu mada zifuatazo zinatakiwa kufafanuliwa kwa undani: • Nini maana ya VICOBA • Jinsi mfumo wa VICOBA unavyofanya kazi • Mifumo ya uwekaji wa fedha • Taratibu za uwekaji wa fedha • Taratibu za urejeshaji wa mikopo • Tofauti kati ya mfumo wa VICOBA na mifumo mingine Nini maana ya kikundi. Kikundi ni ni kundi la watu waliokubaliana kukusanya rasilimali zao kwa pamoja ili kufikia lengo walilo kusudia. Umililiki wa Kikundi. Wanakikundi ndio wataendesha shughuli zote za kikundi kwa kupitia mikutano ya kila wiki na mkutano mkuu. Wanakikundi watachagua kamati ya uongozi na kuanzisha sheria za kikundi zitakazo waongoza. Mali zote za kikundi zitaendelea kumilikiwa na wanakikundi wenyewe na nivyema wawezeshaji wakajiepusha kuchukua fedha za kikundi kuzipeleka kwenye asasi nyingine au sehemu yeyote bila ya kupata ushauri wa kina. Muda wa kuweka fedha. Wanakikundi wataamua ni mara ngapi kwa mwezi watakuwa wanakutana na taratibu za utoaji wa mikopo ya hisa na jamii. Ni vyema pia kukubaliana matukio mbalimbali yanayo weza kuchangiwa na wanakikundi ilikuepusha lawama na manughuniko. Hata hivyo inashauriwa vikundi kukutana kila wiki ili kuongeza ukaribu na kusaidia kukua kwa mfuko wa kukopeshana kwa haraka. Uzoefu unaonyesha ukuaji wa mfuko wa kikundi kinacho kutana kila wiki ni tofauti na ukuaji wa kikundi kinacho kutana mara moja kwa mwezi maana uwezo wa wanakikundi kuhifadhi fedha nyingi na kuziwasilisha kwenye kikundi inakuwa shida. Kukutana kila wiki kunasaidia watu kulipa mikopo yao kwa wakati na kuufanya mzunguko wa fedha ndani ya kikundi kuwa imara. Dhana ya Riba. Dhana ya mikopo huleta mjadala wa riba ya mkopo, ambayo inapingana na maadili ya Imani za kidini mbalimbali. Mwezeshaji ni vyema ajiandae na atoe ufafanue wa kina na kueleza kwa uwazi tofauti kati ya Riba na Ziada ya mikopo ambayo inatozwa na vikundi vya VICOBA. Uanzishaji wa Kikundi. Baada ya mkutano huu washiriki watapewa nafasi ya kujadiliana na kutoa maamuzi kama wapo tayari kuanzisha kikundi au bado wanafikiria. Kama kutakuwa na walio tayari kuanzisha kikundi basi ni mwezeshaji atawasaidia kuanzisha na kuwaongoza katika mambo ya msingi ya kukubaliana. Wajumbe walio tayari watachagua viongozi wa muda, wataandaa sheria za muda, watakubaliana siku ya kukutana, sehemu ya kukutana na jinsi ya kuchangia vifaa vya zoezi la kibenki. 12 MADA YA PILI: KUUNDWA KWA VIKUNDI Mwezeshaji atawaomba washiriki mbao wamehudhuria kwenye mkutano wa uhamasishaji na ambao wapo tayari kuanza kikundi kubaki na wale ambao wanao kwenda kutafakari na familia zao watatakiwa kuondoka ilikuwapa uhuru walio baki kupanga mambo yao. Hatua ya kwanza katika uundaji wa kikundi ni kuundwa kwa vikundi vidogo vya watu watano na ambao watatengeneza kundi kubwa la watu wasio pungua kumi na tano na wasio zidi thelathini. Lengo vikundi vidogo vya watu watano ni kudhaminiana wakati wa kukopa na endapo mjumbe kati yao atashindwa kurejesha mkopo kama kanuni na taratibu zinavyo jieleza wadhamini watawajibika kulipia deni au kiasi kilicho salia. Vikundi vinatakiwa kutoelemea upande wowote wa kisiasa au wa kidini kwa sababu wanachama wake wanatakiwa kuwa mchanganyiko. Kuegemea kwa upande mmoja kutasababisha wanachama wengine kujitoa au kupunguza hari ya watu. Mfumo wa VICOBA haubagui jinsia ambapo wanawake na wanaume wanaruhusiwa kuwa wanachama katika vikundi hivi na kupata haki zote zinazo stahili. Mtu mwenye madeni mengi kwenye vikundi vingine haruhusiwa kujiunga katika kikundi kwani anaweza kudhorotesha maendeleo ya kikundi kwa kukopa fedha na kutozirejesha kwa wakati. Umeibuka pia mtindo wa vikundi kuwa na walezi na nijambo ambalo limerudisha nyuma maendeleo ya vikundi na mfumo wa VICOBA. Jambo hili nilazima liepukwe na wanakikundi maana fedha za kikundi ni mali ya wanachama na hakuna umuhimu wa vikundi kuwa chini ya walezi. Uzoefu unaonyesha walezi wa kikundi huingilia maamuzi ya kikundi na mwisho kudumaza maendeleo ya kikundi. Viongozi wa vikundi hivi ni Mwenyekiti, Katibu, Mwekahazina na Wahesabu fedha wawili. Iwapo kiongozi mmoja hajaudhuria katika mkutano nafasi yake itashikwa na mwanakikundi yeyote atakayechaguliwa siku hiyo na kusimamia au kutekeleza shughuli zote zinazohitajika kama utaratibu unavyoeleza. Kikundi kitakuwa na wajibu wa kumtafuta mwezeshaji kusaidia kutatua tatizo au kupata ufafanuzi wa jambo fulani ndani ya kikundi. Mwezeshaji ni vyema ashirikishwe mara kwa mara na ni vyema akajiepusha na jambo lolote ambalo litaweza kuathiri fedha za wanachama na kama kuna jambo litakuwa juu ya uwezo wake ni vyema na yeyé akaomba ushauri kwa wataalam zaidi. Watiaji saini kwenye hundi ya kikundi ni Katibu, Mweka hazina na mjumbe mmoja ambaye ni mwanakikundi lakini siyo kiongozi na wanakikundi watampendekeza kutokana na uadilifu na uaminifu wake katika jamii. Mwezeshaji atawasaidia washiriki kuchagua uongozi wa muda, kuanzisha sheria za muda, kukubaliana siku ya kukutana, sehemu ya kukutana na thamani ya Hisa pamoja na mchango wa mfuko wa jamii. Majengo ya kisiasa au ya kidini yatatumika tu iwapo 13 wanakikundi wote watakubaliana na kuridhia na endapo baadhi ya wanachama hawatakuwa tayari kutumia majengo hayo basi sehemu ya kukutana itatakiwa kubadilishwa. Mafanikio ya kikundi yanategemea sana jinsi wanachama wanavyojihusisha kikamilifu katika kushiriki mikutano ya kila wiki na jinsi wanavyo zifuata sheria na kanuni walizo jipangia. Mahudhurio ya wanakikundi yanasaidia kufanya mahesabu kuwa sahihi na kupunguza minongono na malalamiko ya wajumbe wengine. Vikundi vya VICOBA hutunga sheria zao za kujiongoza na vikundi hivi hujitegemea vyenyewe. Kila kikundi huwa na sheria zake na sheria hizo hutoa mamlaka kwa uongozi wa kikundi kuonyesha mwelekeo wa uendeshaji wa shughuli za kikundi. Kila mshiriki hutakiwa kuzijua sheria zote za kikundi na kuzifuata ipasavyo. Wajumbe wa kamati ya uongozi watachaguliwa kila baada ya mwaka mmoja na wanaweza kuondolewa wakati wowote iwapo 2/3 ya wanakikundi wa tapiga kura ya kuwaondoa na kuto kuwa na imani nao kutowajibika katika shughuli za kikundi ipasavyo. Kila mwaka kati ya viongozi watano wawili au watatu watapumzika na nafasi zao zitajazwa na wanachama wengine. Sababu za kupumishwa baadhi na baadhi kuendelea ni kujengeana uwezo na uzoefu na kati ya wajumbe watako ondoka ni lazima kati ya mwneyekiti, Katibu na mweka hazina mmoja aweze kupumzika. Mwaka utakao fuata wale walio baki wataondoka na nafasi yao kujazwa na wajumbe wapya watakao chaguliwa. MADA YA TATU: AWAMU ZA KIKUNDI KUPITIA Kuanzishwa kwa kikundi cha VICOBA hufuata awamu kuu nne ambazo ni awamu ya uhamasishaji, awamu ya mafunzo ya kina, maendeleo na awamu ya kupevuka na kukomaa kwa kikundi. Japo awamu hizi nne zinatoa taswira ya jinsi kikundi cha VICOBA kinavyoweza kukua, inawezekana kabisa kikundi kuamua kuingiza mfumo wa mafunzo mengine ya ziada hata katika hatua ya Mwisho ya ukuaji. Hatua za kuanzisha na kukua kwa kikundi cha VICOBA inaweza kuwasilishwa kama inavyo onyesha katika mchoro ufuatao. 14 1- AWAMU YA UHAMASISHAJI: Hii ni awamu ya kwanza kwa uanzishwaji wa kikundi cha VICOBA ambapo mhamasishaji ataelezea mfumo mzima wa VICOBA unavyo fanya kazi, faida zake, hasara zake na huduma zingine zitokanazo na mfumo wa VICOBA. Viongozi wa eneo husika hualikwa na kukaribishwa kama wahamasishaji wakuu kutokana na nafasi zao katika jamii. Baada ya wajumbe kuelimishwa juu ya mfumo wa VICOBA unavyofanya kazi, wajumbe walioshiriki kwenye mkutano watakuwa na hiari ya kuanzisha kikundi au wataomba nafasi ya kufikiria na kutafakari maelezo yaliyotolewa. Kama wajumbe watakuwa tayari kuanzisha kikundi, viongozi wa muda watachaguliwa ambao watakaa madarakani kwa muda wa wiki nne hadi kumi na mbili na ndipo uongozi wa kudumu utafanyika. 2- AWAMU YA MAFUNZO: Awamu hii ni awamu ya muhimu sana maana ndio msingi wa kikundi hujengwa na ambapo mada mbalimbali kuhusu mfumo wa VICOBA huwasilishwa. Kwa mfano katika awamu hii, sifa na kazi za viongozi hujadiliwa, sheria za kikundi hutengenezwa, malengo ya kikundi huanishwa, taratibu za kununua hisa na uwekezaji mwingine ndani ya kikundi huanza, viongozi wa kudumu huchaguliwa na mafunzo ya uendeshaji wa miradi hutolewa. Awamu hii ni lazima kuhudhuriwa na wanakikundi wote na baada ya awamu hii kikundi kinashauriwa kutoongeza mwanakikundi wapya hadi mwisho wa mwaka. 3. AWAMU YA UATAMIZI Miezi 4 4. AWAMU YA UANGALIZI NA KUPEA Miezi 4 1. AWAMU YA UHAMASISHAJI Wiki 4 2. AWAMU YA MAFUNZO YA KINA Mwezi 3 15 3- AWAMU YA UANGALIZI WA KINA: Hiki ni kipindi ambacho kikundi huwekwa kwenye uangalizi wa karibu na kikipewa nafasi ya kuanza kujiendesha chenyewe. Katika awamu hii mwezeshaji atakitembelea kikundi kila baada ya wiki mbili kwa mwezi wa kwanza na mara moja kwa mwezi kwa muda wa miezi mitatu mfululizo. Katika awamu hii kikundi kinapita katika wakati mgumu kwani ni awamu ambayo mikopo huanza kutolewa, uvunjifu wa sheria za kikundi hujitokeza, malalamiko ya baadhi ya wanakikundi kwa kutopewa huduma pia huibuka na mambo haya yanatakiwa kushughulikiwa haraka kabla hayaja sababisha madhara makubwa ndani ya kikundi. Mwisho wa awamu hii mwezeshaji huchambua udhaifu wa kikundi na kubaini kama kikundi kinaweza kujiendesha au bado kinahitaji huduma ya Karibu. Mwezeshaji atawasilisha fomu ya kipimo cha tathimini ambayo itajadiliwa na wanakikundi wote. 4- AWAMU YA KUPEVUKA: Awamu hii ni awamu ambayo mwezeshaji atakitembelea kikundi bila ya taarifa ilikufanya tathimini ya kikundi kinavyo jiendesha. Mwezeshaji atakitembelea kikundi baada ya miezi mitatu au minne au mara nyingi zaidi kama ataombwa na wanakikundi husika. Baada ya awamu hii vikundi ambavyo vinauwezo wa kujiendesha vyenyewe vitapewa vyeti baada ya kufanyiwa tathimini ya kina na watu wenye ujuzi na uzoefu wa vikundi vya VICOBA na vitapewa utambulisho wa kuwa huru baada ya kukamilisha awamu zote muhimu. Jukumu la mwezeshaji wa vikundi vya VICOBA ni kuwawezesha wanavikundi jinsi ya kukiendesha na kukisimamia kikundi chao. Mwezeshaji hapaswi kufanya maamuzi kwa niaba ya kikundi, bali awaelimishe wanakikundi ili waweze kukimiliki kikundi chao na kufanya maamuzi yao. Mwezeshaji haruhusiwi kukitawala kikundi maana jukumu lake ni la muda tu na baada ya kukamilika kwa mafunzo wanakikundi watajiendesha wenyewe na mwezeshaji atabaki kuwa mshauri. Fedha na mali za kikundi zitakuwa chini ya kikundi husika kwa hiyo hairuhusiwa taasisi yoyote kumiliki au kutumia fedha za kikundi maana hurejeshewa wanakikundi pale wanapo jitoa au kufariki. 16 SEHEMU YA PILI NAMNA YA KUENDESHA MIKUTANO Lengo: • Kuelezea aina ya mikutano ya kikundi • Jinsi ya kuendesha mkutano ya kikundi VIFAA • Bango kitita • Kalamu au chaki • Ubao MUDA: Dk 45 MBINU ZA KUFUNDISHIA: • Kuwasilisha mada. • Majadiliano. • Maswali na majibu. • Mifano. MADA YA KWANZA: AINA ZA MIKUTANO Kutakuwa na mikutano aina tatu ya vikundi vya VICOBA. Kutakuwa na mkutano wa kawaida, mkutano wa Dharura na mkutano mkuu. Mkutano wa Kawaida. Mkutano wa kawaida ni mkutano unaofanyika kwa wiki mara moja kwa lengo la manunuzi ya hisa, urejeshaji wa mikopo, ukopaji wa fedha na pia mkutano huu hutumika kama jukwaa la kuelezea mambo mbalimbali ya kimaendeleo yanayo wahusu wanakikundi. Katika mikutano hii wanachama wanaruhusiwa kuwaalika watu mbalimbali wenye ujuzi na kutoa mafunzo kutokana na mahitaji ya kundi husika. Mkutano wa Dharura. Huu ni ule mkutano maalum ambao huitishwa kwa sababu mbalimbali za maamuzi ambayo yatahitaji wanakikundi wote kushiriki katika jambo husika. Mambo mbalimbali yanaweza kusababisha kuitishwa kwa mkutano wa dharura na ambao ni pamoja na mabadiliko ya uongozi, uboreshaji wa sheria za kikundi, kutatua migogoro ya ndani ya kikundi na jambo lolote litakalo hitaji ushiriki wa wanakikundi wote. Tangazo la mkutano hutolewa siku 7 kabla ya mkutano ili kuwezesha wanakikundi wote kuhudhuria kikamilifu. 17 Mkutano mkuu. Mkutano huu hufanyika mara moja kwa mwaka na mambo mbalimbali hujadiliwa na kuamuliwa kwa maendeleo ya kikundi. Mambo hayo ni pamoja na kuwasilishwa kwa tarifa ya fedha ya kikundi ya mwaka, kupata taarifa na mchanganuo wa makusanyo yote ya kikundi, kuchagua viongozi wapya, kuboresha sheria, kuongeza au kupunguza thamani ya hisa na kugawana faida. Mkutano mkuu unatakiwa uandaliwe mapema na siku ambayo wanachama wanatakiwa kupongezana kwa kufanya tafrija fupi. Mfuko wa faini au michango kutoka kwa wanachama hutumika kwa ajili ya kugharamia sherehe. Inashauriwa katika sherehe hii wageni mbalimbali waalikwe na kipaumbele kitolewe kwa viongozi wa serikali waliopo katika eneo la kikundi na viongozi wa dini MADA YA PILI: UENDESHAJI WA MKUTANO Mfumo wa uendeshaji wa vikundi vya VICOBA unatofautiana na mifumo mingine hasa katika uendeshaji wa mikutano na shughuli zote. Mfumo wa VICOBA wanachama wanakutana mara moja kwa muda maalum na maamuzi yote hufanywa mbele ya wanachama. Jinsi ya uendeshaji Muda wa kuanza kufanya mkutano, kamati ya uongozi yenye wajumbe watano ambao ni Mwenyekiti, Katibu, Mwekahazina na Wahesabu fedha wawili wanakaa mbele wakitazamana na wajumbe wengine. Mwenyekiti atafungua kikao kwa kuwaomba washiriki kila mmoja kwa imani yake kuomba dua au sala ya kimya kimya angalau nusu dakika. Utaratibu wa kukaa wakati wa uendeshaji wa mikutano ya kikundi. Wahesabuji Katibu Mhazini Mwenyekiti Wanakikundi 18 1- KUANZA MKUTANO Mwenyekiti atatangaza mbele ya wanakikundi kuwa mkutano umefunguliwa na atawaomba washika funguo kufungua sanduku na mwekahazina kutoa ndani ya sanduku vitabu vya hisa, leja na bakuli tatu kwa ajili ya maandalizi ya shughuli za kibenki ndani ya sanduku. Bakuli kubwa ni kwa ajili ya kukusanyia Hisa, bakuli inayo fuata ni kwa ajili ya kukusanyia fedha za mfuko wa jamii na marejesho na bakuli dogo kuliko zote litatumika kukusanyia faini. Baada ya sanduku kufunguliwa na bakuli kutolewa Mwenyekiti atamwomba Katibu kuita mahudhurio na kukusanya faini kwa watu wote ambao wamekiuka kanuni na taratibu za kikundi. 2- AGENDA Mara baada ya kikao kufunguliwa mwenyekiti atatoa taarifa fupi ya makusanyo kwa wiki iliyopita iliyoandikwa kwenye leja au daftari kubwa na kutangaza salió la pesa zilizobaki kwenye sanduku baada ya wanakikundi kukopa kwenye mkutano uliopita. Mwenyekiti ataainisha agenda kuu ya mkutano na kuwauliza wanakikundi kama wanakubaliana na agenda hiyo na kama kuna pendekezo la agenda nyingine ya kujadiliwa. Mikutano ya kawaida agenda kuu itakuwa ni kununua hisa, mfuko wa jamii, kutoa marejesho, kupata mafunzo, kutoa mikopo na kujadili mengineyo kama yatakuwepo. 3- UWEKAJI WA FEDHA Mwenyekiti atamwomba katibu aendeshe shughuli za kibenki na uwekaji wa fedha za kikundi kwa kumtaka katibu kuwaita washiriki namba zao na kununua hisa kwa kila mmoja kutaja kwa sauti idadi ya hisa anazo nunua na kiasi cha mfuko wa jamii anachowekeza. Mwanachama atawasilisha fedha kwa wahesabuji na kitabu anakabidhiwa mwekahazina kwa ajili ya kujaza hisa na jamii alizo wekeza mwanachama. Baada ya makusanyo ya hisa Katibu ataongoza zoezi la urejeshaji wa mikopo na kila mwanachama anayerejesha atawasilisha mbele kiasi mbele na katibu atajaza kwenye daftari kubwa mwekahazina atajaza kwenye kitabu kidogo. Wahesabu fedha watapokea fedha na kuziweka kwenye bakuli husika wakati huo huo wajumbe wawili watapewa jukumu la kujaza leja. Mwisho Katibu atapiga mahesabu kwenye Daftari kubwa na Mwekahazina atapiga mahesabu kwenye vitabu vya wanakikundi na leja. Wahesabu fedha watatoa tarifa ya fedha taslimu zilizokusanywa na mwenyekiti atatangaza tarifa kwa wajumbe. 19 4- MAREJESHO Baada ya makusanyo Katibu atawaongoza wajumbe kwenye awamu ya kutoa marejesho ya mikopo. Katibu ataanza kuwaita majina wanakikundi ambao tayari muda wao wa kurejesha umewadia. Katibu ataandika idadi inayorejeshwa kwenye kaunta book, mwekahazina kwenye kitabu cha mwanakikundi na wajumbe wengine kwenye leja ya mikopo na wahesabu fedha watapokea fedha inayorejeshwa toka kwa mawanakikundi husika. Fedha zikikusanywa na kuhesabiwa na wahesabu fedha zitakabidhiwa kwa mhazina kwa uhakiki zaidi na takwimu sahihi kupelekwa kwa mwenyekiti na kutangaza jumla ya makusanyo yote. 5- MIKOPO Baada ya kukamilika kwa shughuli ya marejesho Katibu atazisoma fomu zilizo wasilishwa mbele na wakopaji. Kila fomu itajadiliwa na kupitishwa au kukatialiwa kwa sababu ambazo zitatajwa na mtoa hoja. Sababu zinaweza kuwa nyingi kiwa ni pamoja na kuto rejesha mikopo ya nyuma aliyo kopa kwa wakati, kutohudhuria kikamilifu, na kutokidhi masharti yaliyopangwa na wanakikundi. Wajumbe watamjadili na kupitisha au kukataa maombi ya mwanakikundi husika na kama watamkubalia basi fomu itapokelewa na mjumbe atakabidhiwa mkopo wake baada ya kutoa Bima ya mkopo. Katibu atasoma taarifa ya fedha zilizosalia baada ya kutoa mikopo kwa kuainisha fedha zitakazo baki sandukuni au benki. 6- KUTHIBITI FEDHA Makusanyo ya fedha ni lazima yatangazwe kwa wajumbe baada ya kukamika kwa zoezi la kibenki. Baada ya matangazo wahesabu fedha watamkabidhi mwekahazina na atazihakiki na kuziweka ndani ya sanduku au kuzipeleka benki na kipindi hicho takwimu itatolewa kwa mwenyekiti ya kuonyesha jumla ya makusanyo yote na atatangaza kwa wanakikundi. Iwapo kikundi kitafungua akaunti basi kiongozi au mwanakikundi yeyote atachaguliwa na kuombwa kuwasilisha fedha hizo katika benki husika. Ili kuhakikisha uhifadhi wa fedha ni salama yafuatayo yanapendekezwa yafanyike: 20 • Risiti ya kuweka fedha iwasilishwe katika kikao kinachofuata na mwanakikundi aliyepeleka fedha Benki, ikionyesha mhuri wa benki husika na tarehe fedha zilipopelekwa benki. • Kikundi kiombe taarifa fupi ya fedha toka katika Benki husika, kila mwezi. • Iwapo wanakikundi hawana ufahamu au uelewa juu ya taarifa za Benki basi mafunzo maalum yatolewe kwa wanakikundi kujenga uwezo wao. Angalizo. Kwa muda mrefu sana vikundi vya VICOBA vinatumia masunduku kuhifadhia fedha na kwasasa jambo hili limeonekana kuwa ni la hatari hasa baada ya watu wengi kubaini njia hiyo ya uwekaji wa fedha. Kutokana na kupungua kwa usalama na matukio kadhaa kutokea maeneo mbalimbali ya Tanzania kwa watu kuiba masanduku yakiwa na hela na mengine wakihisi kuwepo kwa hela. Kutokana na matukio kuendelea kukithiri vikundi vinashauriwa kutoweka fedha ndani ya masanduku zaidi ya Laki mbili na vikundi vinavyo bakiza fedha nyingi vifanye jitihada za kufungua akaunti benki za kuhifadhia fedha za ziada. Vikundi vinashauriwa pia kuhakikisha kila baada ya makusanyo mikopo inatolewa kwa wanachama wenye uhitaji na wakati wa kufunga hesabu za mwaka vikundi haviruhusiwi kukusanya fedha zote na kuanza upya bali vitafunga hesabu wakati mikopo ikiwa mikononi mwa wanachama. Kikundi kitatakiwa kufanya makisio ya faida itakayo gawanywa kwa wanachama mwisho wa mwaka na fedha hizo ndizo zitatakiwa kuhifadhiwa ili kutoa mgao na kipindi hicho fedha zingine zikiwa kwenye mzunguko wa wanachama. Matukio mengine yaliyojitokeza ni pamoja na fedha za kikundi kihifadhiwa kwenye akaunti za viongozi, watu binafsi au za wawezeshaji na mchezo huo pia hauruhusiwi maana unahatarisha fedha za kikundi. 7- KUFUNGA KIKAO Mwenyekiti atawauliza wanakikundi kama kuna mengineyo na baada ya zoezi hilo atawashukuru wanakikundi kwa kufika na kutoa matangazo kwa ufupi kama yapo kabla ya kuahirisha kikao hicho. 21 SEHEMU YA TATU UENDESHAJI WA SHUGHULI ZA KIBENKI Lengo: • Kufanunua maana na faida za kununua hisa. • Kutoa mwongozo wa jinsi ya kusimamia fedha za wanakikundi. • Kutoa ufafanuzi na taratibu za kutoa na kurejesha mikopo kwa wanakikundi. • Kufahamu viwango vya ziada ya mikopo • Kufahamu umuhimu wa uwekaji wa bima Vifaa: • Bango kitita • Karamu au chaki ya kuandikia • Ubao wa kuandikia Muda: saa Moja Mbinu za kufundishia: • Kuwasilisha mada • Majadiliano • Maswali na majibu. • Mifano na mengineyo Mada hii itaongelea mambo yote ya muhimu maana inajikita kwenye uendeshaji wa mifuko yote ya kikundi. Washiriki wanatakiwa kuelewa kwa undani mambo yote yanayo husu Hisa, Jamii, Mikopo, Marejesho, Bima, Ziada ya Mikopo na mfuko wa adhabu. Mwezeshaji na wanavikundi nilazima wakatenga muda wa kutosha kuyajadili mambo haya ya muhimu. Nimuhimu mwanachama mpya ndani ya kikundi wajumbe wengine wakatoa mafunzo kwa mjumbe mpya ili aweze kuyaelewa mambo ya msingi ya kuzingatia. MADA YA KWANZA: HISA 1. Mwezeshaji anza kwa kuwauliza washiriki hisa ninini? 2. Je nani amewahi kununua hisa sehemu yoyote na ananufaikaje na ununuaji huo? 3. Kunafaida gani ya kunua Hisa? 22 4. Kuna tofauti gani kati ya hisa na akiba Maelezo ya mwezeshaji. Hisa ni fedha inayowekezwa na mwanakikundi katika kikundi kwa lengo la kupata faida na kuwa mmiliki wa kikundi husika. Mwanakikundi anaweza kununua hisa kati ya moja hadi tano kila wiki. Thamani ya hisa moja itatokana na makubaliano ya wanakikundi wa kikundi husika na inashauriwa kiwango hicho kizingatie uwezo wa kiuchumi wa wanakikundi wake. Mfano kama thamani ya hisa moja ni shiling 2,000/- hisa tano thamani yake itakuwa ni shilingi 10,000/- kwa wiki na mwanakikundi anahiari ya kuwekeza kiwango anachoweza lakini isipungue hisa moja na isizidi hisa tano. Mwanakikundi anaruhusiwa kununua hisa moja hadi tano kila mkutano unapo fanyika, na lengo la kuweka uwiano huu ni kuepusha watu wachache wasiweze kukimiliki kikundi na kuwawafanya wengine kuwa wanyonge kwa upande wa kipato na sauti ndani ya kikundi. Pia husaidia kuleta uwiano wa karibu kwa upande wa mikopo wanayostahili pamoja na mafao ya mgao mwishoni mwa mwaka. Kuweka kikomo cha hisa tano ni kuondoa uwezekano wa baadhi ya washiriki kutumia uwezo wao kukitawala na kukiyumbisha kikundi kama wapendavyo. Hisa huwakilishwa katika kikundi na kupigwa muhuri au kuandikwa kwa tarakimu katika kitabu cha mwanakikundi husika na kwenye leja ya kikundi. Thamani huandikwa ndani ya leja ya kikundi na fedha zikisha kusanywa huwekwa ndani ya sanduku la fedha au hupelekwa benki. Ikumbukwe kuwa mwanakikundi akishindwa kutoa hisa zake basi wiki hiyo haitawezekana kufidiwa tena. Hisa ni mali ya mwanakikundi na mwanakikundi atakapo jiondoa, kikundi kitawajibika kumrejeshea hisa zake zote, mfuko wa jamii na malimbikizo mengine kama yapo ambayo mwanakikundi aliye jitoa katika kikundi anastahili lakini faida hataweza kupewa hadi kikundi kifunge hesabu za mwaka. MADA YA PILI: MIKOPO Anza na maswali haya 1. Kwa nini tunakopa 2. Wangapi wamewahi kukopa 3. Kluna faida gani ya kukopa 4. Kunahasara gani ya kukopa 23 5. Masharti gani nimuhimu kuyaweka kwa wakopaji Ni fedha au mali ambazo mkopeshaji anamtaka mkopaji azirejeshe kwa makubaliano maalumu. Katika mfumo huu kutakuwa na mikopo ya aina kuu mbili. Kutakuwa na mikopo itakayo kopwa kutokana na mfuko wa Hisa na kutakuwa na mikopo itakayo kopwa kutokana na mfuko wa jamii. Mikopo ya hisa, mwanachama ataruhusiwa kukopa mara tatu ya hisa alizo wekeza ndani ya kikundi na kurejesha na faida ambayo itatumika kuwagawia wanachama mwisho wa mwaka na mikopo ya jamii itarejeshwa bila ya faida. Kila mkopaji atajaza fomu ya mkopo na kubainisha dhamana ya mkopo wake. Dhamana ya mikopo itathibitishwa na wajumbe wa vikundi vidogo na dhamana hizo zitatakiwa kulingana au kuzidi kiasi cha mkopo anacho daiwa mwanachama husika. Mikopo yote katika vikundi vya VICOBA itatakiwa kulipwa kila mwezi na muda wa kurejesha mikopo ni kati ya miezi mitatu hadi mwaka mmoja. Mkopo wa kwanza mkopaji ni lazima aurejeshe ndani ya muda wa miezi mitatu, mkopo wa pili ndani ya miezi sita na mkopo wa tatu kikundi kinaweza kuamua wanachama akarejesha mkopo ndani ya mwaka mmoja. Mfumo haumkatazi mkopaji kutoa marejesho ya mkopo wake kila wiki na cha msingi anatakiwa kuzingatia kuwa ndani ya mwezi mmoja awe amekamilisha kiwango alichokuwa anatakiwa kukirejesha. Kikundi kinashauriwa kutunga sheria ambazo zitaainisha taratibu za kuchukua mkopo na hatua zitakazo chukuliwa iwapo mkopaji atashindwa kurejesha mkopo wake kwa wakati. Kikundi kinatakiwa kuhakikisha sheria zinasimamiwa na zinafuatwa na kila mwanakikundi ili kuweka nidhamu katika utoaji na urejeshaji wa mikopo kwa wakati. MADA YA TATU: MAREJESHO YA MKOPO • Je wangapi wamewahi kukopa. • Mikopo mnayokopa mnarejesha kwa muda gani Katika mfumo wa VICOBA mwanakikundi anatakiwa kutoa marejesho mara moja kwa mwezi na anaruhusiwa kulipa kidogo kidogo kila wiki kama taratibu za vikao vya kikundi vitakavyo bainisha na kama biashara yake inamruhusu kufanya hivyo. Wanakikundi wote watakao shindwa kurejesha mkopo kwa wakati kama ilivyo kubaliwa na alivyo jaza kwenye fomu yake ya mkopo basi atatakiwa kutozwa faini ya asilimia mbili ya mkopo aliotakiwa kuurejesha kwa mantiki kwamba kama angerejesha fedha hizo zingekopwa na mwanakikundi mwingine na kikundi kingepata faida. 24 Mfumo huu pia unamruhusu mwanakikundi kumaliza deni lake kabla ya muda wake na kumwezesha kuomba mkopo mwingine ndani ya kikundi bila kusubiliana. Nidhamu kubwa inatakiwa kuhakikisha kila mkopaji anatoa marejesho yake kama inavyo takiwa ili kuwawezesha wengine kukopa. Katika mazingira yasiyotarajiwa mwanakikundi akishindwa kurejesha mkopo kwa muda uliopangwa kikundi kitakuwa na uwezo wa kumuongezea muda au kuchukua dhamana zake na kama hazitoshi basi wadhamini wake wa kikundi kidogo watawajibika kulipa deni lililo salio. Mfumo wa VICOBA unaonyesha mafanikio makubwa kutokana na mfumo wa urejeshaji mikopo kila mwezi. Kurejesha mkopo kila mwezi kuna msaaidia mkopaji kupunguza hatari ya fedha za kikundi kupotea na marejesho ya kila wiki huwasaidia wanakikundi wengine kukopa. Kitendo cha kukaa na fedha muda mrefu bila kurejesha kina athiri maendeleo ya kikundi hasa kutokana na kutopatikana kwa mikopo kwa wakati na matokeo yake baadhi ya wanachama kusubiri muda mrefu bila kukopa na mwisho kukata tamaa na kujitoa. MADA YA NNE: ZIADA YA MKOPO 1. Tunaposema ziada ya mikopo tunamaanisha nini 2. Wangapi wanafahamu riba 3. Riba ni mali ya nani 4. Je kama kuna wakopaji wape nafasi ya kueleza ni asilimia ngapi ya riba hutozwa kwenye taasisi zingine. Tofauti kati ya ziada ya mkopo na riba Ziada ya Mkopo ni asilimia ya mkopo ambayo mkopaji anatakiwa kurejesha kwenye kikundi na mwisho wa mwaka fedha hizo humrudia mwenyewe kwa njia ya gawio la faida na, Riba ni fedha ambazo mkopeshaji amemtaka mkopaji kurejesha fedha alizo kopa na kiasi fulani na ambacho ni mali ya mkopeshaji. Kwa mfano mtu anapokopa benki faida inakuwa mali ya benki. 1.1. Umuhimu wa ziada ya mkopo. Hutengeneza mfuko wa faida ambayo wanakikundi hugawana mwisho wa mwaka kama gawio la hisa walizo wekeza. Katika kikundi siyo wanachama wote wanakopa fedha na kutokopa fedha kwao kunawasaidia wengine kukopa mara tatu ya hisa 25 walizo wekeza ndani ya kikundi. Uzoefu unaonyesha mwanachama anayewekeza hisa zake ndani ya kikundi anauhakika wa kupata faida kati ya asilimia kumi na mbili hadi kumi na tisa kwa mwaka na kiwango hiki cha fedha ni vigumu kupata kama umewekeza kwenye makampuni au taasisi nyingine za fedha. Mfuko huu pia husaidia kugharamia madeni mabaya ambayo mfuko wa bima umeshindwa kuyalipa. Kutofidiwa kwa mfuko wa bima kunasababisha hisa za wanakikundi wote kuwa kwenye hatari ya kufilisika. Mfuko huu pia unasaidia kukabiliana na majanga mbalimbali yanayoweza kujitokeza dhidi ya mali za wanakikundi. Viwango vya ziada ya mikopo vikiwa vidogo huathiri ukuaji wa mtaji wa kikundi na mgao wa faida mwisho wa mwaka na Wakati Viwango vya riba vikiwa vikubwa huathiri utashi wa mkopaji kuchukua mikopo. Mapendekezo: Inashauriwa Ziada ya Mkopo itozwe kwa asilimia tano (5%) kwa mkopo unaolipwa kwa miezi 3; asilimia kumi (10%) kwa mkopo unaolipwa kwa miezi sita; na asilimia kumi na tano (15%) kwa mkopo unaolipwa miezi kumi na mbili. Viwango hivi vinavyotozwa kama nyongeza ya mkopo vinaweza kupungua au kuongezwa baada ya wanakikundi kufanya tathmini ya kikundi chao mwisho wa mwaka na kukubaliana juu ya kubadilisha viwango hivi. MADA YA TANO: MFUKO WA JAMII 1. Je tunapo pata matatizo ya dharura tunapata wapi msaada 2. Je inaruhusiwa mwanachama kuchukua mtaji na kwenda kujitibia au kulipia ada ya Mtoto shule. Mfuko wa jamii una lengo la kutoa mkopo kwa wanakikundi ili kusaidia mahitaji ya afya na elimu yanayo jitokeza bila ya kujiandaa. Mfuko huu unatolewa kama mkopo usio na riba na ni mkopo unaomsaidia mwanakikundi moja kwa moja na wanafamilia wake pale wanapopata tatizo la dharura. Mfuko wa jamii hujengwa kwa kila mwanakikundi kuchangia kiasi cha fedha katika kikundi kila wiki wanapo kutana. Mfano: Kikundi kinaweza kuamua kila mwanakikundi kutoa shilingi elfu moja (1000/-) kwa wiki katika mfuko huu. Kama kila mwanachama atachangia kiasi hicho basi mwanachama ndani ya kikundi ataruhusiwa kukopa mkopo ambao hautazidi shilingi laki moja na hii itasaidia wanakikundi wenye matatizo mbalimbali kuweza kunufaika na mfuko huu. 26 Mkopaji atatakiwa kurejesha mkopo wa mfuko wa jamii ndani ya miezi mitatu naakilazi mika kurejesha moja ya tatu kila mwezi. Mkopaji akishindwa kurejesha mkopo ndani ya miezi mitatu bila sababu maalumu mwanachama huyo atatakiwa kulipa ziada ya mkopo kama mkopo wa kawaida. Iwapo pia mwanachama atafariki na deni la mfuko wa jamii kikundi kitakata kiasi kwenye mafao yake kulipia deni analo daiwa na kiasi kitakacho salia atakabidhiwa mrithi wake. Kila mwanachama anawajibika kuhakikisha kiwango alicho changia kwenye kikundi katika mfuko wa jamii kinalingana na idadi ya wiki. Iwapo mwisho wa mwaka itabainika miongoni mwa wanakikundi walichangia kiasi pungufu basi fedha zao za mgao wa faida zitakatwa ilikuweka ulinganisho kati yake na wanachama wengine ndani ya kikundi. MADA YA SITA: MFUKO WA BIMA 1. Je kunamwanachama ambaye amewahi kukatia bima 2. Je huduma gani ambazo hukatia Bima 3. Kuna faida gani ya kukatia bima 4. Matukio gani mngependa kukatiwa Bima Mfuko wa Bima ni mfuko ambao umeanzishwa kwa lengo la kulinda mikopo yote itakayo kopwa endepo wakopaji watafariki. Mfuko huu utakuwa na wajibu wa kuweka usalama kwa mtaji wa kikundi hasa pale mmoja wa wanakikundi anapofariki akiwa hajamaliza kulipa mkopo wake ndani ya kikundi. Mfuko wa bima utachangiwa na kila mwanakikundi atakayekopa mkopo katika kikundi husika. Mwanakikundi atachangia asilimia mbili ya mkopo wake kwenye mfuko wa bima ya kikundi. Fedha hizo hazitarudishwa kwa mwanakikundi baada ya kumaliza deni lake bali mfuko huu utaendelea kujengwa ilikuuwezesha kukabiliana na majanga makubwa yanayoweza kujitokeza. Mwanakikundi akijitoa katika kikundi hataruhusiwa kudai na hatarejeshewa fedha za mfuko wa bima maana mikopo bado itaendelea kukopwa kwa wale watakao baki katika kikundi. Fedha za bima ni mali ya kikundi na iwapo kikundi kitasambaratika fedha zote za Bima zitachanganywa na mfuko wa ziada ya mkopo na kugawanywa kama faida. 27 2. Faini Kutakuwa na mfuko wa faini ambao utakuwa unajitegema katika kikundi na ukiwa na majukumu ya kugharamia shughuli zote za uendeshaji ikiwemo kutoa nakala za fomu, kununua vinywaji kwa wageni na wanakikundi wenyewe pale inapo hitajika na kununua vifaa vinapo kwisha. Faini ni fedha zitakazo kuwa zinalipwa na mwanakikundi anayekiuka kanuni na taratibu za kikundi walizojiwekea. Kanuni za kikundi hutungwa na wanakikundi husika na zikiainisha malengo ya kikundi, taratibu za kuendesha kikundi, vitendo visivyokubalika katika kuendesha kikundi na iwapo mwanakikundi atakwenda kinyume na makubaliano ya wanakikundi. . Fedha za faini zitatumika katika kugharamia shughuli za kikundi na muda mwingine wanakikundi husika wanaweza kujipongeza kwa kunywa vinywaji au matumizi mengine yoyote yatakayo pitishwa na wanakikundi. Mfuko huu pia unawajibu wa kugharamia safari za viongozi, gharama za mafunzo na kuandaa tafrija mwisho wa mwaka. Vikundi vingi vya VICOBA havioni umuhimu wa kufanya tafrija. Tafrija ni muhimu sana kwenye vikundi hasa baada ya kutimiza mwaka maana kwenye tafrija wageni mbalimbali hualikwa na mara nyingi tafrija huleta hamasa hasa kwa wengine kuja kujifunza. Wakati umefika sasa vikundi viwili hadi kumi kuunganisha kufanya tafrija sehemu moja na ambayo wanaweza kuwaalika wageni mbalimbali badala ya kila kikundi kualika wageni wao. MADA YA SABA: KUFUNGA MAHESABU MWISHO WA MWAKA Kila kikundi kitakuwa kinafunga hesabu zake kila mwaka baada ya kutimiza wiki 52 za uwekaji wa fedha na uchukuaji wa mikopo. Hesabu zitatakiwa kufungwa na ripoti ya jumla ya makusanyo ya hisa, mikopo, bima, mfuko wa jamii, faini na michango mingine kama itakuwepo itatolewa. Kikundi kitafunga hesabu za mwaka mzima kwa kutambua fedha zilizowekezwa ndani ya kikundi na kila mwanakikundi kwa mwaka mzima. Mwisho wa mwaka kila kikundi kinatakiwa kuhakikisha hesabu zinabainisha wazi kiasi cha fedha taslimu kilichopo ndani ya kikundi na kiasi cha fedha kilichopo mikononi mwa wanachama kwa njia ya mikopo. Fedha taslimu zinajumlisha fedha zote zilizopo kwenye kisanduku na zilizo hifadhiwa benki au katika taasisi yoyote ya fedha iliyoruhusiwa kwa mujibu wa Benki kuu ya Tanzania. Wakati wa mahesabu viongozi pamoja na wanakikundi watahakikisha takwimu za fedha zimetengwa kwenye makundi kama ilivyo kuwa inachangiwa na kikundi husika. 28 Viongozi watajumlisha mifuko yote na kupata jumla yake kama inavyo onyesha kwenye mfano hapo chini. S/N IDADI YA HISA THAMANI YA HISA MFUKO WA JAMII BIMA YA MKOPO ZIADA YA MIKOPO MADENI YA HISA MADENI YA JAMII 1 1000 5,000,000 104,000 2,000,000 8,000,000 0 2 1500 7,500,000 104,000 3,000,000 5,000,000 0 3 750 3,750,000 104,000 375,000 3,000,000 0 4 900 4,500,000 104,000 0 0 0 5 850 4,250,000 104,000 2,625,000 2,000,000 0 JUMLA 5,000 25,000,000 520,000 2,300,000 7,500,000 18,000,000 Hisa 25,000,000 Jamii 520,000 Bima 2,300,000 Ziada ya Mkopo 7,500,000 JUMLA ya fedha zote 35,320,000 Madeni ya Hisa 18,000,000 Taslim kwenye sanduku 17320,000 JUMLA KUU madeni na tslimu 35,320,000 Baada ya kukamilisha zoezi la kujua kikundi kinathamani ya shilingi ngapi kama inavyo onyesha hapo juu wanakikundi watakwenda kwenye zoezi la mwisho la kuhakikisha kama fedha tajwa hapo juu zipo au hazipo. Baada ya mahesabu kuwiana zoezi la mwisho litakuwa ni kugawana fedha za Ziada ya mkopo kama gawio la mwisho wa mwaka na kutoa fedha za wanachama wanajiondoa katika kikundi. 3. Jinsi ya kugawana faida mwisho wa mwaka. Mgao wa faida utafanyika kwa kutumia fedha za faida zilizo patikana na idadi ya hisa zilizo changiwa na wanachama kwa muda wote wa uhai wa kikundi. Baada ya kufunga hesabu mgao wa faida utafanyika kwa kuchukua faida iliyopatikana na kugawanya na idadi ya hisa zilizowekezwa ndani ya kikundi. Lengo la zoezi hili ni kubaini hisa moja imepata faida ya shilingi ngapi kabla ya kuigawa faida hiyo kwa kila hisa za mwanakikundi. 29 Kama inavyo onyesha jedwali hapo juu, kikundi kwa mwaka mzima kiliweza kununua hisa 5000 zenye thamani ya Tsh ml 25, 000,000 na mwaka kilipata faida ya Tsh milioni 7, 500,000. Kutokana na mfumo wa kupata faida ya kila hisa moja zitachukuliwa shilingi 7, 500,000 ambazo ni ziada ya mikopo na zitagawanywa na idadi ya hisa zilizo nunuliwa kwa kipindi chote ambacho ni hisa 5000. Baada ya kuzigawanya kila hisa itapata faida ya shilingi 1500. Baada ya kupata faida hiyo kila manachama atazidishiwa hisa zake na faida ya hisa moja iliyopatikana kama inavyo onyesha kwenye jedwali hapo chini. S/N IDADI YA HISA FAIDA YA HISA MOJA MGAO SAINI YA MPOKEAJI 1 1000 1500 1,500,000 2 1500 1500 2,250,000 3 750 1500 1,125,000 4 900 1500 1,350,000 5 850 1500 1,275,000 JUMLA 5000 7,500,000 Baada ya kuandaliwa kwa jedwali hili mgao wa faida utatolewa kwa wanakikundi wote ndani ya kikundi bila ya kujali kama walikopa au hawakukopa na kila mpokeaji atatia saini yake. Ikumbukwe kuwa mgao wafaida hautakuwa sawa bali mwenye hisa nyingi atapata faida kubwa na mwenye hisa ndogo atapata gawio dogo. 30 SEHEMU YA NNE UONGOZI WA KIKUNDI Lengo: ♦ Kuwasaidia washiriki kufahamu umuhimu wa kuwa na Kamati ya uongozi ♦ Kuwasaidia kutambua majukumu ya kamati ya uongozi na nafasi tofauti zilizomo kwenye kamati. ♦ Kuwawezesha washiriki kueleza majukumu, sifa na mamlaka ya wote ambao watashika nafasi za uongozi, pamoja na kuendesha vikao Vifaa: • Bango kitita • Kalamu • Ubao Muda: 1.00 Mbinu za kufundishia • Kuwasilisha mada • Majadiliano • Maswali na majibu. • Mifano MADA YA KWANZA: KAMATI YA UONGOZI Kamati ya uongozi itaundwa na wajumbe watano. Wajumbe hawa ni mwenyekiti, Katibu, mwekahazina na wahesabufedha wawili. Wajumbe hawa watachaguliwa miongoni mwa wanakikundi wenzao katika mkutano mkuu wa wanachama. Kamati hii ndiyo yenye dhamana ya kuongoza na kusimamia shughuli na rasilimali za kikundi. Wajumbe wa kamati watachaguliwa kwa mujibu wa sifa, uwezo na weredi wao katika jamii. Nafasi za viongozi kama watakuwa hawapo zitajazwa na mwanakikundi yoyote atakaye pendekezwa siku ya mkutano na atakuwa na madaraka ya kufanya shughuli zote ambazo kiongozi husika alitakiwa kuzitekeleza. 31 Hadithi. Hadithi hii ni ya kikundi cha maendeleo, kikundi kilianzishwa na washiriki 27 na baada ya wiki moja wakajikuta wameongezeka hadi wanakikundi 45. Washirki waliamua kujigawa katika makundi mawili. Katika kikundi cha pili wanakikundi walimchagua mke wa Kiongozi wa serikali na kuwa mwenyekiti wa kikundi. Mwezeshaji alijaribu bila mafanikio kuwaelimisha wanakikundi sifa za mwenyekiti wa kikundi lakini wanakikundi waliendelea kung’ang’ania awe mwenyekiti wao kwa sababu watapatiwa misaada na matokeo yake alishindwa kuendesha kikundi na kikundi kushuka kimaendelea siku hadi siku. Baadae wanakikundi waliamua kumbadilisha mwenyekiti lakini tayari wanachama wengi walikuwa wamejitoa na baadhi ya wanakikundi walikimbia bila kurejesha mikopo. A. Je mmejifunza nini kutokana na hadithi hii? B. Mnafikiri ingekuwa ni nyinyi mngefanya nini? 4.3. MAELEZO YA MAJUKUMU NA SIFA ZA KILA MJUMBE WA KAMATI YA UONGOZI. MWENYEKITI SIFA • Awe mwenye uwezo wa kuendesha mikutano • Mwenye tabia njema katika jamii • Mwenye kukubalika mbele ya jamii na kusikilizwa • Mwaminifu, mwenye heshima, mwenye hekima na busara. • Mwenye uwezo wa kutatua migogoro ndani ya kikundi. • Mvumilivu, mwenye kupatikana katika vikao vya kikundi na mwenye uwezo wa kusimama mbele ya watu. • Asiwe mlevi • Mwenye hamasa nzuri katika jamii. • Mwajibikaji na mfano wa kuigwa na wanakikundi wengine katika kikundi. • Mwenye ushawishi na utetezi mzuri katika maendeleo ya kikundi. MAJUKUMU • Kuongoza kikundi • Kuwakilisha kikundi kwa watu wa nje na wasio wanakikundi • Kuhakikisha sheria za kikundi za zinafuatwa na kuheshimiwa • Kuwashauri wanakikundi • Kutafuta suluhisho la ugomvi miongoni mwa wanakikundi • Kuhitimisha mikutano • Kufungua mikutano na kutangaza agenda • Kutangaza makusanyo yaliyo pita (uwekaji fedha) na baadae kutoa mikopo. • Kuhakikisha usalama wa mali zote za kikundi. • Kushirikiana na wajumbe wengine wa kamati ya uongozi kulipa mali pale inapobainika kuwa wao ndio wahusika wa upotevu wa mali hizo. KATIBU 32 SIFA • Ajue kusoma, kuandika na kuhesabu kwa ufasaha • Awe ni mwenye uwezo wa kutoa taarifa sahihi kuhusiana na mwenendo wa shughuli za kikundi. • Awe na mahudhurio mazuri kwenye kikundi. • Mwenye kuwajibika, hodari, mwaminifu na mwenye busara • Mwenye kuheshimu wenzake • Asiwe mlevi. • Asiwe na upendeleo MAJUKUMU • Kuandika na kukumbuka shughuli zote zinazofanywa na kikundi katika kila mkutano. • Kuita wanakikundi wakati wa kununua hisa na uwekaji wa mfuko wa jamii. • Kutoa taarifa na shughuli za kikundi kwa mwezeshaji wakati wa ufuatiliaji. • Kulipa fedha zinazo potea ikibainika kuwa kamati ya uongozi wa kikundi imehusika. MHAZINA SIFA ZAKE • Mwenye maudhuria mazuri kwenye kikundi. • Mwenye kujua kusoma kuandika na kuhesabu kwa ufasaha • Mwenye nyumba yenye usalama wa uhakika na inayoheshimika • Mwanifu katika jamii na mwenye busara • Inashauriwa awe mwanamke • Mwenye mahusiano mazuri katika familia yake • Mwenye familia na asiyehamishika kirahisi. MAJUKUMU YAKE • Kuweka fedha za kikundi • Kuhakikisha usalama wa fedha na mali za kikundi • Kutayarisha mahesabu katika sanduku la fedha na kusimamia mienendo yote ya shughuli za kibenki. • Kuhakikisha sanduku limefungwa baada ya mkutano wa kikundi • Kuhakikisha marejesho yanatolewa. • Kutunza kumbukumbu zote za fedha za kikundi • Kugonga mihuri kwenye vitabu vya Hisa. • Kutoa taarifa ya mapato na matumizi mwisho wa kufunga mwaka wa kikundi. • Kulipa fedha zinazo potea ikibainika kuwa kamati ya uongozi wa kikundi imehusika. WAHESABU FEDHA SIFA • Mwenye kupatikana kila wiki kwenye vikao vya kikundi • Awe mwaminifu • Awe menye busara na kauli nzuri • Mwenye kujua kusoma, kuandika na kuhesabu kwa ufasaha. • Asiwe mdokozi na ambaye amewahi kuhusishwa na mambo ya utapeli. MAJUKUMU • Kuhesabu na kuthibitisha fedha zinazo ingia na zinazotoka kwenye sanduku kabla na baada ya kukusanya fedha • Kutoa taarifa ya jumla ya fedha zote kwa mwenyekiti kabla ya makusanyo na baada ya makusanyo. • Kupokea fedha zote zinazo wekwa katika kikundi kuanzia hisa, mikopo na marejesho na ziada ya mikopo. 33 • Kulipa fedha zinazo potea ikibainika kuwa kamati ya uongozi wa kikundi imehusika. Kikundi kitakuwa na wajumbe wanne wenye dhamana maalumu na ambao ni washika funguo watatu na mjumbe mmoja mtiaji saini kwenye hundi ya kikundi wakati wa kuchukua fedha benki. Wajumbe hawa hawatakuwa viongozi na watakuwa na dhamana maalumu na inashauriwa wawe na sifa zifuatazo: WASHIKA FUNGUO WASHIKA FUNGUO SIFA Mwanakikundi mwenye uwezo wa kuhudhuria mikutano kila wiki Mwenye nyumba yenye usalama na uaminifu. Mwenye kumbukumbu nzuri Mwaminifu na mnyenyekevu MAJUKUMU YAO Kuwa mdhamini wa funguo Kuwasilisha funguo katika kila mkutano Kuhakikisha sanduku linafunguliwa na kufungwa kila siku ya mkutano. Kulipa gharama ya kufuli na nyinginezo iwapo atapoteza funguo za kikundi MTIAJI SAINI SIFA Awe mwaminifu. Mwenye hekima, busara na mcha mungu Asiwe mwenye dhiki Awe mkweli, mwazi na mpenda haki Awe mwenye msimamo Majukumu yake Kuchukua fedha kwa kushirikiana na wajumbe wengine benki au kusaini kwenye hundi ya kikundi inapobidi. 34 MADA YA PILI: UCHAGUZI WA KAMATI YA KUDUMU YA UONGOZI WA KIKUNDI Baada ya kujifunza na kutambua sifa na majukumu ya kila kiongozi uchaguzi wa kamati ya uongozi ya kudumu utafanyika. • Wanakikundi watajikumbusha sifa, na majukumu ya kila mjumbe wa kamati ya uongozi Kwa kawaida kwenye vikundi vingi washiriki hupenda kukwepa majukumu kwa kutokubali kuchaguliwa na vyema ikaelezwa wazi kwamba mtu ambaye atajiona yeyé apendi kuwa kiongozi kwa sababu zake binafsi basi hatastahili kuwa mwanakikundi katika kikundi. Kila mwanachama anadhamana ya kuhakikisha kikundi kinatimiza malengo yake na nivyema kila mjumbe akafahamu kuwa siku itakapo wadia atawajibika kukiongoza kikundi. Wakati mwingine pia washiriki huchagua viongozi mapema kabla ya kutambua sifa zao au wakati mwingine viongozi kujishinikiza wao wenyewe kutokana na maslahi yao binafsi. Mwezeshaji ni lazima ahakikishe uchaguzi unafanyika tena na wajumbe wenye sifa kuchaguliwa kushika nafasi zinazo takiwa na nivyema suala la kuchagua viongozi lisiingiliane na masuala ya siasa na dini maana kuviingiza vitu hivyo kutaathiri kama siyo kuvunja kabisa kikundi. Uchaguzi utafanyika kwa washiriki • kupendekeza majina ya wagombea kwa kila nafasi Washirika watapiga Kura kwa kila nafasi na kura zitapigwa kwa nafasi moja na baada ya kukamilika wajumbe watapendekeza majina ya nafasi inayofuata na inashauriwa uchaguzi uanze wa mwenyekiti wa kikundi. Mwezeshaji ahakikishe wajumbe waliochaguliwa wanaweza kufanya kazi na kama sivyo ni vyema aingilie kati na kueleza umuhimu wa kazi na sifa zinazohitajika. Mwezeshaji wapongeze wanakikundi waliochaguliwa kushika nafasi mbalimbali katika kikundi na watakie mafanikio mema katika kazi zao na wanakikundi wote wajipongeze kwa kukamilisha zoezi hilo kwa amani na upendo 35 MADA YA TATU: MAMLAKA Kipindi cha uongozi ni mwaka mmoja ambapo kikundi kitafanya tena uchaguzi mkuu wa kubadilisha wajumbe wa kamati ya uongozi. Kiongozi haruhusiwi kukaa madarakani zaidi ya awamu mbili za uongozi na hii ni kuonyesha kwamba mfumo huu unahitaji kila mwanakikundi ashike nafasi ya uongozi ndani ya kikundi. Katika mkutano mkuu ndio uchaguzi wa viongozi wapya na ambao wanamajukumu ya kuongoza, kuendesha na kusimamia fedha pamoja na shughuli zote za kikundi watapatikana. Lengo la mamlaka ni kuwaidhinisha wajumbe wa kamati ya uongozi kufanya kazi zao zilizoamuliwa na kukabidhiwa. Pia inasaidia kuweka mipaka kwa baadhi ya viongozi wanaofikiri kuwa wenye uwezo wa maamuzi ya kupindukia katika jamii ni wao. 4.3.1. Taratibu za kuachia madaraka Kama ilivyo elezwa hapo awali viongozi wa kikundi watakuwa wanabadilishwa kila mwaka ili kuonyesha ufanisi wa kikundi. Katika mkutano mkuu wa mwaka baada ya kutangaza hesabu za kikundi na wajumbe wote kuridhia taarifa iliyotolewa na uongozi ulio pita hatua itakayo fuata ni kufanya uchaguzi wa viongozi kwa kuwapigia kura wajumbe walio kuwa madarakani maana inashauriwa kila mwaka viongozi watatu lazima wapunguzwe na nafasi zao zijazwe na wajumbe wapya watakao chaguliwa. Wajumbe watapiga kura kwa kuandika majina ya viongozi gani wangependa wapumzishwe na viongozi gani wangependa wabaki. Kati ya viongozi watakao takiwa kutoka ni lazima kuwe na wajumbe kwenye nafasi ya mwenyekiti, au Katibu au mwekahazina atakaye ondolewa. Lengo la kufanya mabadiliko haya ni kuongeza ufanisi katika kikundi na kuleta hali ya uwajibikaji miongoni mwa wanachama maana kikundi ni mali ya wanachama wote. Mwaka utakao fuata wale viongozi walio baki wataondoka na nafasi zao zitajazwa na wajumbe wengine watakao chaguliwa. 36 SEHEMU YA TANO SHERIA ZA KIKUNDI Lengo: • Kuelezea umuhimu wa sheria katika kikundi. • Kuwasaidia wanakikundi kuandaa sheria zao VIFAA • Bango kitita • Kalamu • Ubao MUDA: 1.30 MBINU ZA KUFUNDISHIA: • Kuwasilisha mada • Majadiliano • Maswali na majibu. • Mifano 1. MAANA YA SHERIA Sheria ni mustakabali, taratibu na kanuni zilizokubalika na wanachama ili kuongoza kikundi. Kuheshimu sheria hizo ni muhimu kwani ndio muhimili wa kufikia malengo ya kikundi. Wanakikundi ni vyema wakatambua kuwa sheria walizozitunga ni zao kwa hiyo wanaweza kuzibadilisha kulingana na mahitaji au kuongeza wakati itakapobidi, ila sheria hizo zisiwe kinyume na taratibu za uendeshaji wa mfumo wa vikundi vya VICOBA. Baada ya sheria kuanzishwa ni lazima sheria hizo ziandikwe kwa lugha ambayo kila mwanakikundi ataweza kuzisoma na kuzifuata. Hivyo ni muhimu kila mwanakikundi kupata nakala na zingine zihifadhiwe kwenye faili la kikundi ambapo zitapatikana muda wowote zitakapohitajika. Ni vyema kila kikundi kikawasilisha nakala ya sheria katika ofisi za serikali za mitaa au katika ofisi za watendaji wa vijiji ili vikundi viweze kutambulika. Mfumo wa VICOBA hadi sasa hautambuliki kisheria na matokeo yake 37 baadhi ya vikundi vimesajiliwa chini ya mamlaka ya biashara yaani Brela, wengine Ushirika, wengine mambo ya ndani na matokeo yake kujiingiza katika sheria hizo baadhi ya vikundi vimepoteza mueleko vingine vingi vimesambaratika kabisa. Serikali inawajibu wa kuandaa sheria itakayo weza kuandaa utaratibu wa vikundi vya VICOBA kutambulika na hii itasaidia kulinda uhalisia wake. Ikumbukwe kuwa vikundi vya VICOBA vimeenea na vinaongezeka na tathimini iliyo fanyika mwaka jana mwezi decemba jumla ya shilingi bilioni 24 zinazunguka ndani ya vikundi. Hadithi. Juma ni mwanakikundi katika kikundi cha Sonaka na huudhuria mara chache kwenye vikao, lakini kwa kawaida hupeleka fedha za michango kwenye kikundi kwa kumuagiza mwanakikundi mwenzake. Siku ya Ijumaa Juma alikuwa na shughuli ya jamaa yake ambayo ilikuwa ni siku ya mkutano wa kikundi. Kama kawaida Juma alipeleka hisa yake yenye thamani ya shilingi 1000/= kwa kumpa jirani yake na akamtaka amwombee na mkopo wa shilingi 100,000/= katika kikundi ilikuchangia shughuli ya rafiki yake. Kwa kuwa Juma alikuwa hahudhurii kwenye kikundi mara kwa mara, wiki iliyopita wanakikundi walifanya mabadiliko ya sheria za kikundi ambazo zilikuwa hazifanyi kazi na hazikidhi kwa wakati huo. Kutokana na mabadiliko hayo wanachama walimkatalia mjumbe aliyetumwa na Juma ombi la mkopo na kumrudishia hisa yake ya shilingi 1000/=. Mwezeshaji au kiongozi wa kikundi wape nafasi wanakikundi kujadili kwa dakika tano na maswali yafuatayo yanaweza kuwaongoza. • Je unadhani ni kwanini walimrudishia ? • Je unahisi nini kilitokea ? 38 VIPENGELE VYA SHERIA ZA KIKUNDI 1. Jina na anuani 2. Malengo ya ya kikundi 3. Mamlaka ya kikundi. 4. Sifa za mwanakikundi 4.1. Jinsia 4.2. Umri 4.3. Makazi 4.4. Afya 5. Taratibu za kujiunga katika kikundi 6. Wajibu wa mwanakikundi 7. Mrithi 7.1. Taarifa za mrithi 7.2. Taratibu za kubadilisha mrithi 7.3. Idadi ya warithi wanaoruhusiwa kuandikwa kwenye daftari la kikundi 7.4. Mafao anayo stahili mrithi 8. Kufukuzwa/kusimamishwa ndani ya kikundi 8.1. Matukio yatakayo msimamisha/kufukuzwa mwanakikundi 8.2. Haki za mwanakikundi aliyefukuzwa 8.3. Muda wa kuzilipa haki za mwanakikundi aliyefukuzwa 8.4. Mwanachama asipo hudhuria mara ngapi mfululizo bila taarifa atakuwa amejifukuzisha ndani ya kikundi. 9. Ukomo wa mwanakikundi 9.1. Taratibu za kufuata iwapo mwanakikundi atajitoa katika kikundi. 9.2. Taratibu za kupata haki za mwanakikundi aliyejitoa 9.3. Muda wa kupewa mafao anayostahili 10. Uwanakikundi utasitishwa kwa: 10.1. Kutohudhuria mara nne mfululizo 10.2. Kutoa siri za kikundi 39 10.3. Kuchonganisha 10.4. Kutonunua hisa mara nne mfululizo 11. Taratibu za mfuko wa Hisa 11.1. Idadi ya hisa ambazo mwanakikundi anaruhusiwa kununua ni hisa moja hadi hisa Tano. 11.2. Thamani ya hisa moja ni tsh?. 11.3. Kiasi cha faini kwa watakao shindwa kununua hisa? 12. Mikopo ya Hisa 12.1. Taratibu za kurejesha mkopo 12.2. Viwango vya Riba/ziada ya mkopo 12.3. Taratibu za kufuata kwa wanakikundi watakao shindwa kurejesha mkopo. 12.4. Wajibu wa wadhamini (5) wa kikundi kidogo iwapo mkopaji ameshindwa kurejesha mkopo. 12.5. Vigezo vitakavyo weza kuchuja wakopaji iwapo fedha hazitoshi sandukuni 12.6. Jinsi ya kutathimini uwezo wa mkopaji 12.7. makosa gani yatamwezesha mwanachama kupewa mkopo kiasi kinacho lingana na hisa zake au mara mbili ya hisa zake. 13. Bima ya mkopo. 13.1. Kiwango cha kuchangia katika mfuko wa bima inashauri aslimia mbili 13.2. Mfuko wa Bima utafanya kazi iwapo mwanakikundi amefariki na deni la Mkopo wa Hisa. 13.3. Iwapo bima haitatosha kufidia deni kiasi cha fedha kitakatwa kutoka kwenye mfuko wa Ziada ya mikopo kabla ya kugawana mwisho wa mwaka. 14. Mfuko wa jamii (ELIMU NA AFYA) 14.1. Kila mwanakikundi atachangia shilingi …… katika mfuko wa jamiii 14.2. Mwanakikundi ataruhusiwa kukopa mkopo usiozidi shilingi …. Katika mfuko wa jamii na atazirudisha bila ziada ya mkopo. 14.3. Kiwango cha chini kinachotegemewa kiwepo kwenye mfuko wa jamii ndani ya kikundi kwa wakati wowote kwa dharula ni shilingi…………. 14.4. Mwanakikundi ataruhusiwa kukopa kwa ajili ya matatizo ya elimu na afya. 14.5. Muda wa kurejesha mkopo wa jamii 14.6. Hatua zitakazo chukuliwa iwapo mwanakikundi ameshindwa kurejesha mkopo wa jamii kwa wakati. 14.7. Hatua zitakazo chukuliwa iwapo mwanakikundi atafariki na deni la mfuko wa jamii. 40 15. Majukumu ya Viongozi wa kikundi 16. Mambo ya kufanya katika mkutano mkuu 17. Makosa yatakayo tozwa faini. 17.1. Kutohudhuria mkutano wa kikundi bila ya taarifa mwanakikundi atatozwa shilingi……………………….. 17.2. Uchelewaji kwenye mkutano wa kikundi bila ya taarifa ni shilingi … 17.3. Mwanakikundi aliyeomba udhuru tofauti na kuuguliwa au kufiwa atachangia shilingi ngapi kwenye mfuko wa faini? 17.4. Kuonyesha dharau kwenye kikundi 17.5. Kupoteza Kitabu 17.6. Kuzungumza kwenye mkutano bila ya ruhusa ya mwenyekiti……. 17.7. Kamati isipotekeleza majukumu yake sawasawa 17.8. Simu kuita kwa sauti kwenye mkutano 18. MENGINEYO 18.1. Mwanakikundi atakaye ugua muda mrefu ndani ya kikundi wanakikundi watachukua hatua gani ………………….. 18.2. Mwanakikundi aliye fariki mafao yake yatatolewa ndani ya siku tisini. 18.3. Iwapo mwanakikundi atafiwa atachangiwa Tsh ….. na kila mwanakikundi wa kikundi. 18.4. Kiasi gani kitachangiwa iwapo mwanakikundi atakuwa amefariki 19. Mwanakikundi aliye fariki 19.1. Hatua zitakazochukuliwa kwa mwanakikundi aliyefariki 19.2. Haki za mwanakikundi aliyefariki 19.3. Lini haki hizo zitalipwa 19.4. Ikiwa amefariki na mkopo wa kikundi hatua zipi zitachukuliwa 20. VYANZO VYA MAPATO YA KIKUNDI o Faini o Ziada ya mikopo o Na mikopo kutoka katika taasisi za fedha o Mfuko wa Hisa o Bima ya kikundi 41 SEHEMU YA SITA UTUNZAJI WA KUMBUKUMBU Lengo: 1. Kuelezea umuhimu wa kuweka na kutunza kumbukumbu za kikundi Vifaa: • Bango kitita • Karamu au chaki • Ubao wa kuandikia Muda: 45 Mbinu za Kufundisha: • Kuwasilisha mada • Majadiliano • Maswali na majibu. • Mifano MADA YA KWANZA: MFUMO WA UTUNZAJI WA KUMBUKUMBU Mfumo wa VICOBA ni kama mifumo mingine ya kifedha ambayo inahitaji umakini sana katika utunzaji wa kumumbuku na mali ya wanachama. Mfumo wa VICOBA unahamasisha kumbukumbu kutunzwa katika makundi tofauti na hii ni kurahisha na kuwa na uhakika pale moja ya kumbukumbu inapo someka tofauti au inapo leta utata wa maamuzi. Katika mfumo wa VICOBA kumbukumbu zitatuzwa kwenye kitabu cha mwanachama, Daftrai kubwa, leja ya kikundi na kutakuwa na fomu za mikopo. Kila kundi lina umuhimu wake kama inavyo onyesha hapo chini. KITABU CHA KUMBUKUMBU ZA MWANAKIKUNDI. Kitabu cha kumbukumbu za mwanachama ni kitabu kinachotunza kumbukumbu za mwanakikundi ambapo hisa, mfuko wa jamii, Bima, ziada ya Mkopo na mikopo hujazwa ilikumrahisishia mwanakikundi kufuatilia kwa karibu mwenendo wa fedha zake ndani ya kikundi. Ni muhimu kwa kila mwanakikundi kuwa na kitabu kwa ajili ya kumbukumbu zake zinazohusu hisa zake, mfuko wa jamii na mikopo. Kitabu hiki ambacho kitaandikwa 42 namba ya mwanakikundi ilikumwezesha kufuatilia mwenendo wa uwekaji wake na mikopo yake yote. MKUTANO WA MFUKO WA JAMII HISA 01 Kitabu hiki kinasehemu kuu mbili. Sehemu ya kwanza inatunza kumbukumbu za makusanyo na akiba za mwanachama na sehemu ya pili inaonyesha mikopo na kwenye mikopo kumegawanyika katika makundi Mawili. Kundi la kwanza mikopo ya hisa na kundi la pili mikopo ya jamii. Mikopo ya hisa taarifa zifuatazo zinapatikana: Tarehe aliyokopa mkopo, bima ya mkopo, kiasi kilichokopwa, ziada ya mkopo, kiasi alichorejesha, salio la mkopo na sahihi ya mhazina wa kikundi husika maana ndiye anayetakiwa kujaza katika kitabu hiki. TAREHE BIMA KIASI CHA MKOPO ZIADA YA MKOPO KIASI KILICHO REJESHWA SALIO SAHIHI YA MWEKA HAZINA Sehemu ya pili ni mikopo ya jamii na taarifa zifuatazo hujazwa: tarehe aliyokopa, kiasi alichokopa, kiasi alichorejesha, salio la mkopo na saini ya mweka hazina. Kitabu hiki ni lazimia kionyeshwe wakati wa kununua hisa, kukopa mkopo na kutoa marejesho. Wakati wa mikopo inashauriwa kitabu cha mwanachama anaye taka mkopo kiwasili mbele au apewe mwanachama mwingine na azihesabu hisa za mkopaji husika. TAREHE KIASI CHA MKOPO KIASI KILICHOREJESWA SALIO SAHIHI YA MWEKA HAZINA 1. LEJA YA KIKUNDI. Kikundi kitakuwa na Leja mbili za kumbukumbu za wanakikundi wote ambapo taarifa mbalimbali zitaingizwa kwenye ukurasa husika. Leja ya kwanza itahusika na makusanyo yote ya siku na taarifa zifuatazo zitapatikana kwenye leja ya kikundi nazo ni: majina ya wanakikundi, mahudhurio ya kila wiki, kitabu cha mahesabu, hisa za wanakikundi, mfuko wa jamii, fomu ya warithi wa mali za wanakikundi, faini inayokusanywa na leja ya pili itajishughulisha na mikopo ya hisa na jamii ambapo kila mwanachama atakuwa 43 na ukurasa wake na taarifa mbalimbali zitaainishwa kama zinavyo onyeshwa kwenye jedwali hapo chini. MIKOPO YA HISA TAREHE MUDA WA MKOPO BIMA YA MKOPO KIASI CHA MKOPO ZIADA YA MKOPO SAINI YA MKOPAJI MKOPO ULIO REJESHWA FAINI YA KUCHELEWESHA MKOPO MKOPO ULIo SALIA SAINI YA KATIBU MIKOPO YA JAMII TAREHE KIASI CHA MKOPO SAINI YA MKOPAJI MKOPO ULIO REJESHWA MKOPO ULIo SALIA SAINI YA KATIBU 2. DAFTARI KUBWA Kufanya kazi ya kurekodi makusanyo yote ambayo yanafanyika kwa wiki husika Kikundi kitakuwa na daftari kubwa moja ambalo litahifadhi taarifa zote za kila wiki kwa mujibu wa makusanyo yatakavyokuwa yanafanyika. Daftari kubwa litahifadhi taarifa zote kwa undani zaidi na hii itasaidia kuwa na usalama wa utunzaji wa taarifa nyingi ndani ya kikundi. Daftari kubwa litahifadhi taarifa za hisa, jamii, marejesho, mikopo, faini na kutoa taarifa ya salió la kila wiki katika kikundi. Ushauri: Inashauriwa daftari kubwa lisihifadhiwe kwenye sanduku au kama kikundi hakina sanduku basi aliyehifadhi vitabu pamoja na reja asihifadhi daftari kubwa. JINSI YA KUCHORA NAMBA JINA LA MWANACHAMA IDADI YA HISA THAMANI YA HISA MFUKO WA JAMII FAINI FOMU ZA MIKOPO Kikundi kitakuwa na fomu mbili tofauti za mikopo. Fomu moja itahusika na mikopo ya hisa na fomu nyingine itajihusisha na mikopo ya jamii. Ni vyema mkopaji ajaze fomu kabla ya kupewa mkopo wake kwa ajili ya kumbukumbu 44 Kutakuwa na aina kuu mbili za fomu za mikopo ambazo ni: Fomu ya mfuko wa Hisa ambao utaeleza kwa kina jina la mkopaji, kiwango anacho kopa, majina na saini za wadhamini na dhamana juu ya mkopo alio uomba. Fomu zote zitakuwa kwenye faili moja. Kutakuwa na fomu nyingine ya mfuko wa jamii ambayo itaonyesha jina la mkopaji na wadhamini wake pia. Hii inasaidia kuonyesha kumbukumbu za kikundi na iwapo kunatokea jambo lolote basi taarifa zisikosekane. Utaratibu utaandaliwa na kikundi juu ya upatikanaji wa fomu na kumwezesha mwanakikundi kupata fomu pale anapohitaji mkopo. Kikundi kinashauriwa kutumia mfumo huu na kuepusha kuwa na makaratasi mengi au daftari kubwa nyingi ndani ya kikundi maana karatasi nyingi huleta shida wakati wa kufunga hesabu na muda mwingine kujaza sanduku bila sababu. MADA YA PILI: MFUMO WA UHIFADHI WA FEDHA BENKI. Kutokana na hali halisi ya ukuaji wa fedha za kikundi maeneo mbalimbali na kwa kuzingatia kanuni za fedha kila kikundi kitashauriwa kufungua benki akaunti ambayo itawezesha kutunza fedha zake. Hatahivyo fedha hizo zitatunzwa pale tu iwapo hapatakuwa na wakopaji ndani ya kikundi. Vikundi pia vitaendelea kuangalia umbali wa kutoka kwenye eneo la kikundi na eneo ambalo benki ilipo na hii itasaidia kuepusha matumizi makubwa ya nauli wakati fedha zinapopelekwa. Hasara ya kupeleka fedha benki ni kukatwa kila mwezi na kutotolewa kwa mikopo kwa wakati ndani ya kikundi. Hata hivyo mafunzo maalumu yatatakiwa kutolewa jinsi ya kutunza kumbukumbu za fedha zilizopo benki na wanazozungusha mkononi. SANDUKU Kikundi kitakuwa na maamuzi ya kutumia sanduku na wanakikundi husika kukubaliana sehemu ya kuhifadhi sanduku lao. Kikundi kinashauriwa kutohifadhi fedha ndani ya sanduku au kuziweka benki na zaidi viongozi watatakiwa kuwahamasisha wanakikundi kila baada ya makusanyo kuchukua mkopo. Faida ya kutumia sanduku ni kuwa fedha zinapokusanywa zinaonekana na hazipelekei wanakikundi kuwa na wasiwasi tofauti na benki ambapo viongozi wanaweza kutumia fedha zilizopo kwenye akaunti ya kikundi bila ya idhini ya wanakikundi. Hasara ya kutumia sanduku kuweka fedha ni rahisi kwa wezi kuliiba hasa kama litahifadhiwa katika maeneo ambayo siyo salama. 45 SEHEMU YA SABA UTATUZI WA MIGOGORO Lengo: • Kuelimisha wanakikundi juu ya athari za migogoro katika kikundi • Kuwaelimisha mbinu ya kutambua migogoro na hatua za kufuata ili kutatua migogoro • Kuchambua vyanzo vya migogoro Vifaa: • Bango kitita • Karamu au chaki • Kisimamisha ubao aubango kitita Muda: Dakika 45. Mbinu za kufundishia: • Kuwasilisha mada • Majadiliano • Maswali na majibu, • Hadithi NINI MAANA YA MGOGORO Migogoro ni hali ya kutoelewana inayotokea baina ya pande mbili au zaidi. Migogoro inaweza kuwa kati ya mtu na mtu, mtu na kikundi au kikundi na kikundi. Bila kujali idadi ya watu wanaogombana, mgogoro usiosuluhishwa mapema unaweza kuwa na athari kubwa kwa mtu mmoja au kundi la watu. Viongozi wa kikundi wanajukumu la kujenga na kudumisha hali ya amani na usalama ndani ya kikundi, hivyo viongozi wanajukumu la kusuluhisha migogoro itakayojitokeza. Misingi mikuu katika usuluhishi ni pamoja na: • Kutambua chanzo cha mgogoro ni jambo la muhimu ili kuleta suluhu sahihi. Pia inapunguza kuwepo kwa upendeleo wakati wa kusuluhisha. • Ni muhimu pia kutoa nafasi ya kila pande katika mgogoro kutoa maelezo yao juu ya mgogoro husika, bila kujali nani ni chanzo cha ugomvi. Haki ya kusikilizwa na kujieleza ni haki ya msingi kabla ya kusuluhisha mgogoro. 46 • Msuluhishi kutokuwa upande wa mtu yeyote na kuto onyesha upendeleo. • Kabla ya kuanza usuluhishi ni muhimu kwa msuluhishi kubainisha lengo kubwa la usuluhishi huo pamoja na wahusika wa mgogoro ambao ni kupatanisha pande husika na si kuongeza ukubwa wa tatizo. • Kutoa nafasi kwa wanakikundi kutoa maoni yao juu ya mgogoro na athari ya mgogoro huo kwa kikundi iwapo hautasuluhishwa na kuwaomba kupendekeza suluhisho la mgogoro husika. MADA YA KWANZA: VYANZO VYA MIGOGORO KATIKA VIKUNDI. Waombe washiriki kutaja vyanzo vya migogoro. Kati ya mambo yatakayo tajwa ni pamoja nai: • Kutotekelezwa kwa sheria ipasavyo • Viongozi kutotambua majukumu yao • Kukosekana kwa elimu sahihi ya shughuli husika • Majukumu ya kikundi kuachwa kwa watu wachache • Kuwepo kwa makundi ndani ya kikundi • Kuwepo kwa chuki binafsi miongoni mwa wanakikundi • Kuwepo kwa dharau baina ya wanakikundi wenye kipato kikubwa na wenye kipato kidogo • Kusengenyana • Kutokuwa wa wazi • Uchu wa madaraka • Wivu • Ubinafsi • Kuwa mjuaji kupita kiasi • Ukabila, udini na u vyama. • Wawezeshaji kupendelea wakati wa kufundisha • Majungu • Malumbano MADA YA PILI: MATOKEO YA MGOGORO Nini ni matokeo ya migogoro? Majibu ni pamoja na: • Kuvunjika kwa kikundi 47 • Kupotea kwa mali za wanakikundi • Kuendelea kwa uhasama • Kudhorota kwa maendeleo ya kikundi • Kutoaminiana na kuogopana • Kukosekana kwa amani miongoni mwao • Kukatisha tamaa wengine kujiunga kwenye vikundi • Kudhorotesha ustawi wa kiuchumi kwa wanakikundi MADA YA TATU: JINSI YA KUTATUA MGOGORO. Migogoro yote itatuliwe ndani ya kikundi na kama viongozi ndio wahusika basi wasimamizi wa vikundi, washauri au kikundi kipendekeze nani aombwe na kualikwa ili kutatua mgogoro wao. Wanakikundi watapendekeza mtu ambaye wanamwamini na anayekubalika pande zote mbili na ambaye atawaongoza kutatua mgogoro bila ya upendeleo. Msuluhishi wa mgogoro anashauriwa asiwe msemaji mkuu katika kutatua mgogoro huo bali jukumu lake kuu liwe ni kuwaelekeza na kuwaongoza wajumbe katika kufikia suluhu ya tatizo lao. 1. WAKATI WA KUTATUA MGOGORO HATUA ZIFUATAZO ZINAWEZA KUTUMIKA 1. Wahusika kulielezea tatizo 2. Kusikiliza pande zote ili kubaini chanzo cha mgogoro husika 3. Kuweka mapendekezo ya suluhu ya tatizo husika 4. Kutathimini mapendekezo yaliyo tolewa 5. Kuchagua pendekezo zuri zaidi 6. Tathimini matokeo ya mgogoro husika 7. Kuandaa mpango wa hatua ya jinsi ya kutatua tatizo hilo Baada ya kutatua mgogoro ni vyema wajumbe wote wakapongezana na kuondoa tofauti zote ambazo zilikuwepo miongoni mwao ili zisitokee tena. Wajumbe wajipongeza kwa kushikana mikono. Hadithi. Katika kikundi cha mali asili mwanachama mmoja Koini alikopa mkopo wa shilingi 100,000/= za kikundi katika mfuko wa Hisa. Lengo la mkopo huu lilikuwa ni kuendeleza biashara yake ya kupika vitafunwa. Sehemu kubwa ya fedha alizokopa zilitumika kwenye harusi ya mwanae. Ilipofika muda wa kurejesha mkopo koini hakwenda mkutanoni kwa vile hakuwa na fedha za kulipa mkopo wake. Siku iliyofuata aliwasikia 48 wanakikundi wawili wakiwasimulia watu wengine hadithi yake kisimani. Alipofika nyumbani Koini alimsikia mke mwezie akimdhihaki. Koini alifahamu kuwa hadithi yake imeenea kijiji kizima na aliamua kuinyamazisha kwa kukopa fedha kwa rafiki yake pale pale kijijini na kulipa deni lake lote kwenye kikundi na kisha akaandika barua ya kujitoa kwenye kikundi. Tumia maswali yafuatayo baada ya kusimulia hadithi • Unafikiri hadithi hii ina ujumbe gani? • Unadhani Koini angelifanya nini? • Wanachama wa kikundi wamefanya vizuri? • Unadhani wanakikundi wangefanya nini? • Kwa nini haya yote yalitokea? • Je unadhani kikundi kingependekeza shauri gani kama ni suluhisho? • Wanachama wafanye nini kuzuia migogoro kama hii isitokee ? • Je mkopo upi unanafuu kati ya mkopo wa mtu binafsi au mkopo kwenye kikundi?. Mwezeshaji hitimisha hadithi hii kwa kutatua mgogogoro uliojitokeza kwa kufuata njia ambazo wanakikundi wamejifunza katika somo hili. Muhimu katika utatuzi wa mgogoro huu wanakikundi wa kaanza na chanzo, matokeo ya mgogoro na hatua za kutatua mgogogoro. 2. UFUPISHO WA MWEZESHAJI Migogoro yote itatuliwe ndani ya mkutano wa kikundi na wanakikundi wote wanahaki ya kutoa mawazo yao kwenye mkutano wa kutatua mgogoro. Mjadala utaanza mara baada ya shughuli za kibenki kumalizika na sanduku liwe limefungwa na kuondolewa sehemu ya kikao. Kama muda hautatosha wanakikundi wanaweza kupendekeza muda mwingine na ikubaliwe na robo tatu ya wanakikundi wote wa kikundi. 49 UENDELEVU WA VIKUNDI UTANGULIZI Mfumo wa VICOBA ni mfumo endelevu ambao unahamasisha vikundi kufunga hesabu kila mwaka na kuhamisha taarifa za fedha kutoka mwaka mmoja na kwenda mwaka mwingine. Kikundi kinapo anzishwa mikopo huwa midogo na baada ya miezi sita na kuendelea Viwango vya mikopo hukua na kuwawezesha wanachama wa kikundi husika kupata mitaji ya kuweza kuendeleza na kukuza biashara zao hasa katika ulimwengu huu wa ushindani. Mjadala wa kugawana au kutogawana fedha zilizo changwa na kuwekeza kwenye kikundi kila mwaka. Kunamaswali mengi tunatakiwa kujiuliza kabla ya kufanya maamuzi na kutoa hitimisho na maswali haya ni pamoja na: • Malengo ya kuanzisha kikundi hiki yalikuwa ni yepi • Malengo hayo yamefikiwa • Kama tuna gawana fedha kunahaja gani ya kuanza tena • kwanini tuliamua kuanzisha kikundi • Pia ni vyema kujiuliza sababu za kiuchumi je kiasi nilicho anza kukopa mwaka uliopita na nikikopa leo nitakuwa na uwezo wa kuanzisha au kupanua biashara yangu. Baada ya majadiliano hayo wanakikundi wakubaliane kama watakuwa wanagawana kila kitu kila mwaka au WAKATI WA KUFUNGA HESABU ZA KIKUNDI Kikundi kitafunga hesabu kila baada ya wiki 52 ambazo sawa na mwaka mmoja na wanachama watagawana faida iliyopatikana kutokana na mikopo inayorejeshwa na ziada. Mfuko huu utagawanywa kwa wanachama kila mwaka na mifuko mingine itaendelea mwaka unaofuta. Mifuko itakayo endela ni pamoja na Mfuko wa Hisa, Jamii na Bima. Mifuko hii ndiyo mifuko inayoimarisha kikundi na kuwawesha wanachama wa kikundi kukopa zaidi. Kwa wastani kwa sasa ndani ya vikundi vya VICOBA wanachama wanakopo fedha hadi shilingi za kitanzania milioni miamoja akiwa na hisa zenye thamani ya shilingi milioni thelasini na tano. Fedha hizi zinatokana na kudunduliza kila wiki wanapo kutana na hatimaye mwanachama hujikuta amewekeza kiasi hicho. 50 Baada ya kufunga hesabu kikundi kinashauriwa kubadilisha leja, daftari kubwa na taarifa zake kuzihamishia kwenye vitabu vipya vya kikundi. Hii ni kupunguza uwezekano wa wanachama kushindwa kufunga hesabu ambapo zinaweza kuwayumbisha kama uwezo wao wa kuweka na kutunza hesabu ni mdogo. MAMBO YA KUZINGATIA Ili kikundi kiweze kuwa endelevu ni vyema mambo yafuatayo yakazingatiwa. Sheria. Wanachama ni vyema wakazingatia sheria zao kikamilifu na wale wote wanao kaidi ni vyema wakatolewa katika vikundi na nafasi zao kujazwa na wanachama wengine au kuachwa wazi. Urejeshaji wa Mikopo. Kila mwanachama majukumu na wajibu wa kurejesha mkopo wake kama kanuni na taratibu za VICOBA zinavyo eleza na wale ambao wanashindwa kurejesha ni vyema hatua zikachukuliwa dhidi yao. Mahudhurio. Kikundi hakiwezi kuwa kikundi kama hakutakuwa na wanachama wanao hudhuria vikao kama inavyo takiwa. Mfumo wa VICOBA unahamasisha sana mahudhurio na sababu ya msingi ni kwamba maamuzi yote ya kikundi hutolewa na wanachama wa kundi husika. Usalama wa Kikundi. Usalama wa mali na fedha za kikundi upo chini ya wanachama wa kikundi husika cha watu thelasini. Wawezeshaji, waratibu na wasimamizi hawahusiki kwa namna yoyote na fedha za kikundi hasa katika kuzihifadhi, kuzikusanya na hata kuziunganisha kwenye mfuko wa pamoja. Fedha za wanachama zitaendelea kusimamiwa na kikundi husika na kama vikundi vitaamua kuungana basi kati ya mambo ya kuzingatia na ambayo kikundi hakipaswi kuyafanya ni kuchukua fedha za kikundi kuhifadhi katika akaunti ya umoja. Kikundi kitakuwa ni mwanachama kitatakiwa kulipa na kutoa michango kama katiba ya umoja itakavyoeleza na umoja wa vikundi hauta kuwa na mamlaka ya kuvishawishi vikundi kuhifadhi au kukusanya fedha za kikundi kuweka kwenye akaunti za umoja. 51 FOMU YA UFUATILIAJI WA MAENDELEO YA KIKUNDI. Maswali ya mwongozo wakati wa kutembela vikundi 1. Je wanachama wanaudhuria kwenye kikundi ipasavyo 2. Je wanachama wote wananunua hisa ipasavyo 3. Wanachama wote wanachangia jamii kama ilivyopangwa 4. Je kamati ya uongozi inawajibika 5. Je kumbukumbu zinajazwa kama inavyo takiwa 6. Kuna matatizo yoyote uliyo yabaini katika uendeshaji wa kikundi 7. Je vitabu vya hisa vinajazwa kama inavyo takiwa 8. Je leja zinajazwa na kuhifadhiwa ipasavyo 9. Je datfari kubwa linajazwa 10. Je kikundi kinahitaji msaada wowote wa kiutalaam 11. Je wanachama wanazingatia na kuzifuata sheria zao 12. Matatizo gani yanakisumbua kikundi 13. Kikundi kinatembelewa mara ngapi. 14. Makusanyo Hisa……………..… Jamii ……………..………. 15. Marejesho ya Hisa…………………. Jamii………………………….. 16. Mikopo ya hisa……………………….. Jamii………………..….. Angalizo. Mwezeshaji unapo tembela vikundi jiepushe na kukaa kwenye meza ya mbele au kuingilia shughuli za kikundi husika. Mwezeshaji kaa pembeni ambapo patakuwezesha kuona wanachama wote na viongozi wa kikundi. Kwa muda wote utajiuliza maswali na kupata majibu kwa kuona na kama majibu mengine hayatapatikana basi baada ya shughuli zao kukamilika utatakiwa kuwauliza viongozi na wanachama wote. Mwezeshaji kisaidie kikundi kujiendesha chenyewe kwa kusisitiza umuhimu wa kusimamia sheria na viongozi kuwajibika na kuwawajibishwa wanachama wote wanao kiuka kanuni na taratibu za kikundi husika. Baada ya kufanya tathimini yako jaribu kuainisha mapungufu yaliyojitokeza na toa ushauri jinsi ya kutatua au suluhisho ya mambo hayo. 52 TAARIFA YA MWEZESHAJI/MRATIBU WA MRADI KILA BAADA YA MIEZI MITATU JIna la mwezeshaji ……………………………………………….. Tarehe ……………………………………………………………… Wilaya/Kata………………………………………………………… 1. Idadi ya vikundi……………………………………………………….. 2. Idadi ya vikundi vilivyo anzishwa kwa mwezi/miezi mitatu ……………. 3. Taarifa ya umri wa vikundi ………………………………. 4. Je vikundi vinavunja mzunguko au avivunji mzunguko na kama vinavunja ni vingapi 5. Je umewahi kuomba msaada wa kutatua matatizo kutoka kwa mratibu wako wa mradi ………………………… 6. Matatizo gani yamekuwa sugu katika vikundi………………………… 7. Matatizo haya yanatatuliwaje katika vikundi………………………….. 8. Unatoa mapendekezo gani juu ya matatizo ya mara kwa mara yanayo jitokeza 9. Msaada gani wa ziada ambao unahitajika …… 10. Kunafulsa gani ambazo zinaweza kusaidia katika kuboresha maendeleo ya vikundi 11. Je kunataasisi nyingine zinazo fanya kazi na vikundi na kama zipo zinaitwaje na zinatoa huduma gani. 12. Unamapendekezo gani ili kuboresha maendeleo ya vikundi kwa ujumla 13. Mafanikio gani wanachama wameyapata kutokana na kujiunga na vikundi vya VICOBA. Onyesha vielelezo kama vipo kwa mfano picha na visa mkasa. 14. Je vikundi vinafedha kiasi gani. Onyesha kwa kuchora duara kama lifuatalo JINA LA KIKUNDI HISA JAMII BIMA JUMLA Angalizo. Waratibu, wawezeshaji na wasimamizi wa vikundi hawana muda wa kukaa na kufuatilia shughuli za vikundi na muda mwingi wanapita kukusanya ripoti bila kushiriki na kuona jinsi kikundi kinavyo fanya kazi. Waratibu ni vyema wakaheshimu pia mikutano ya vikundi na kama kuna wageni au watu wanataka kujifunza watu hao wafanye shughuli zao ndani ya ratiba za mikutano ya kikundi husika. Kubadilisha mikutano ya kikundi kwa maslai ya watu wan je hairuhusiwi. 53 Mwandishi wa mwongozo huu ni Evance Chipindi ambaye amekuwa katika shughuli za uendeshaji wa vikundi vya VICOBA kwa zaidi ya Miaka kumi na moja.

KUUNDA KIKUNDI CHA VICOBA

VICOBA (Village Community Bank) ni mfumo wa kuweka na kukopa kwa wanachama waliojiunga kwa pamoja na kuunda kikundi kwa malengo ya kujikwamua kiuchumi. Mfumo huu ulianza Tanzania miaka kumi iliyopita na umeonyesha mafanikio makubwa kwa wanachama wake kuweza kukopeshana, kusaidiana katika matatizo mbalimbali, kuanzisha miradi ya pamoja ya kiuchumi.

LENGO/MADHUMUNI YA KUUNDA VICOBA
Madhumuni ya kuunda vicoba ni kuunganisha nguvu na rasilimali za wanachama ili kuondoa umaskini na kuleta maendeleo kwa kufanya yafuatayo:-
  • Kuchangia/kununua hisa
  • Kuchangia mfuko wa jamii
  • Kuendesha mfuko wa kuweka na kukopa
  • Kushiriki katika mafunzo ya kuongeza ujuzi wa biashara, uongozi na uanzishaji wa shughuli mbalimbali za pamoja za maendeleo.
  • Kutafuata soko la pamoja na la uhakika kwa bidhaa za wanakikundi 

Kuna tofauti gani kati ya VICOBA na SACCOS?
VICOBA na SACCOS ni vikundi vya kiuchumi vyote vina malengo sawa isipokuwa mfumo wa uendeshaji.
  1.  Katika VICOBA wanachama uweka kiwango cha hisa na mara nyingi huanzia Sh.1000 na kuendelea, kiwango hicho ni kidogo ukilinganisha na kiwango cha hisa katika SACCOS.
  2.  WanaVICOBA umaliza mzunguko wao baada ya miezi kumi na mbili (12) na kufanya tathmini ikiwemo kugawana makusanyo na faida.
  3. Riba ya mkopo katika VICOBA ni ndogo (mara nyingi haizidi 10%)
  4. Kikundi cha VICOBA kinaundwa na wanachama 15-30, wanaoishi eneo moja au wanaofanya kazi pamoja.
  5.  Gharama za uendeshaji wa VICOBA ni ndogo kwani hakuna ofisi (wanachama huchagua mahali pa kukutana kwa muda usiozidi saa moja), vile vile viongozi wa VICOBA hawaajiriwi (wanafanya kazi za kujitolea)
Vicoba ikikuwa inaweza kuunda SACCOS. Mfumo wa Vicoba ni mzuri hasa kwa falsafa ya kuanza kidogo ili kuwa na kitu kikubwa hapo baadae. Licha ya kujihusisha na shughuri za kuweka na kukopa, wanavicoba husaidiana katika matatizo mbalimbali kama msiba na ugonjwa. Vile vile wanavicoba wanaweza kuanzisha mradi wa pamoja wa kikundi kwa kuunganisha rasirimali ndogo walizonazo. 
Hatua za Kuunda kikundi cha VICOBA
  1. Watu wenye wazo la kuanzisha kikundi kukutana (watu hao wasipungue kumi na tano na wasizidi therathini)
  2. Wanachama kukusanya fedha za kiingilio (mara nyingi ni Sh. 10,000) kwa mwanachama. Fedha hiyo hutumika kununua vifaa kama leja,kasiki n.k. Fedha ya kiingilio vilevile hutumika kugharamia mafunzo ya awali na gharama ya usajiri wa kikundi)
  3. Wanachama kuanza mafunzo yatakayosimamiwa na mwalimu mtaalamu wa mfumo huu wa vicoba.
  4. Wanachama kutunga katiba na sheria zitakayojumuisha kiwango cha hisa, mfuko wa jamii, siku ya kukutana n.k

Vicoba husajiliwa Brela kama jina la biashara (Business name) na kutambuliwa na halimashauri ya manispaa husika kupitia ofisi ya maendeleo ya jamii.
Mfumo huu ni mrahisi kuuendesha na unamanufaa makubwa katika maendeleo ya kiuchumi. Ni fursa kwa vijana wenye mitaji midogo kuanzisha vikundi hivi ili kuunganisha rasirimali ndogo walizonazo na kwa pamoja kujiletea maendeleo.

Kwa maelezo zaidi na ushauri juu ya uanzilishajiwa vicoba wasiliana nasi.

Monday, 5 September 2016

MKOPO WA MWEZI MMOJA UKIKOPA 100,000 UNARUDISHA TSH 102,500

TANGAZO LA MKOPO
PATA MKOPO WA TSH 100,000 KWA RIBA YA TSH 2500. MKOPO WA MWEZI MMOJA UKIKOPA 100,000 UNARUDISHA TSH 102,500. KILA JUMATANO SAA TATU ASUBUHI HADI SAA TANO NA NUSU ASUBUHI. MAFUNZO YA UJASIRIAMALI YANATOLEWA NA MAELEKEZO YANATOLEWA. VIKUNDI VYOTE VINAKOPESHWA NA AMBAYO HAVIJA SAJILIWA VITASAJILIWA HAPO HAPO VIKIWA VIMEJIANDAA KUPATA USAJILI. WANAVICOBA WOTE MNAKARIBISHWA MUWEZE KUSAJILI VIKUNDI VYENU NA KUPATA MIKOPO. KILA KIKUNDI KINACHOVUNJWA MWISHO WA MWAKA SASA HAKITAVUNJWA TENA MAANA BADALA YA KUVUNJA MGAWANE PESA MNAPATIWA MARATATU YA PESA AMBAYO MNGEGAWANA YAANI KAMA UNGEPATIWA 100,000 BASI UTAPATA 300,000 KAMA MKOPO. UKIPATA UJUMBE HUU MSHIRIKISHE NA MWINGINE.
WAPI: TABATA BIMA.
JINSI YA KUFIKA : PANDA DALADALA  ZINAZOENDA TABATA KIMANGA OMBA MSAADA USHUKE CAMP. HAPO ULIZIA ST VINCENT PAUL  NDIO HAPO UMEFIKA.
JUMATANO TAR  7/9/2016

SAA TATU ASUBUHI HADI SAA TANO NA NUSU. 9AM TO 11AM
https://www.facebook.com/JAMES-AHADI-OBEDI-236330979855579/?fref=hovercard