AHADIWAY NI NINI?
Ni asasi
isiyo ya kiserikali inayoshughulika hasa na masuala ya kijamii.
Asasi hii
ilisajiliwa rasmi tarehe 06 Januari 2014 chini ya kifungu cha sheria 12(2) ya
2002 (The None Government Organisation Act)
Asasi hii imejikita katika mchakato wa kupunguza umaskini kwa kuwapatia watanzania wote mbinu za kuweza
kupambana na umaskini.
WALENGWA
NI AKINA NANI?
Kila
mtanzania aliyefikisha umri wa miaka kumi na nane na kuendelea aliye tayari
kubadilika kimtazamo na kuukataa umaskini.
NAWEZAJE
KUWA MWANACHAMA WA AHADIWAY?
Ili uwe
mwanachama wa Ahadiway unapaswa uwe katika kikundi cha watu watano ( 5) mpaka
kumi na tano (15) mliokubaliana kuungana . Gharama za kujiunga kama kikundi ni
sh laki tatu (300,000) Pesa hii itatumika katika usajili wa kikundi hicho kama
kampuni itakayotambuliwa na BRELLA. Cheti hicho kitasaidia kikundi katika
kutekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na kuaminika kukopeshwa pesa kutoka
taasisi za fedha,
FURSA
ZIPATIKANAZO AHADIWAY.
Kama taasisi
inayojishughulisha na mkakati wa kupunguza umaskini Ahadiway imeandaa fursa nyingi apatazo mwanachama
wake
Ø Kupata mikopo ya fedha taslimu
Ø Mikopo kwa ajili ya Miradi Mikubwa
Ø Mikopo ya bajaji zinazotumia umeme
Ø Mikopo ya magari
Ø Mikopo ya nyumba za bei nafuu
MIKOPO YA FEDHA TASLIM.
Mwanachama
akishajiunga anatakiwa kuanza kujiwekea akiba ambayo tunaita HISA.
Utaratibu wa kuweka hisa utamsaidia
kukopa `mara mbili pindi atakapofikisha zaidi ya miezi mitatu. Anachotakiwa kufanya ni
kujaza fomu ya mkopo na kueleza kusudi la mkopo na pia fomu yake lazima
isainiwe na wadhamini wanne ambao ni wanachama wenye hisa za kutosha ili
mkopaji akishindwa kulipa kwa muda uliopangwa ,hisa zake na za wadhamini wake
zitakatwa ili kufidia deni lake.
MIKOPO YA
MIRADI MIKUBWA.
Mikopo ya
miradi mikubwa ni mikopo itakayotolewa kwenye kikundi baada ya kukamilika kwa
taratibu zote za usajili. Wanakikundi wanatakiwa kuandaa mchanganuo wa biashara
wanayohitaji kuifanya. Mchanganuo huo wa biashara utawasilishwa makao makuu kwa
ajili ya kuufanyia kazi. Endapo kama kutakuwa na gharama zozote kwa ajili ya
ule mchanganuo, wanakikundi watapewa taarifa ili kulipia hizo gharama. Kiwango
cha mkopo wa mradi kitategemea na aina ya mradi ulioombewa pesa hata kama ni
milioni mia moja.
Pesa za
miradi zinatoka katika taasisi za fedha ambazo tumeingia nazo mkataba kwa ajili
ya wanachama wetu, hata viwango vya riba vitatokana na aina ya mkopo
uliotolewa.
BAJAJI ZA
UMEME.

Hizi ni
bajaji za aina yake ambazo hutolewa na Shirika la Ahadiway pekee. Bajaji hizi
hukopeshwa kwa mwanachama yeyote ili mradi akidhi vigezo na masharti. Kikundi
au mwanachama mmoja mmoja anaruhusiwa kukopa bajaji’ Anachotakiwa kufanya ni
kutanguliza milioni mbili (2,000,000) kama kianzio kisha anapewa bajaji yake.
Mwezi mmoja baada ya kuchukua bajaji anatakiwa kuanza kurejesha deni lake kwa
kipindi cha miezi minane. Gharama ya bajaji hizo ni sh milioni sita tu.
Mikopo ya
magari bado tunaifanyia kazi.
MIKOPO YA
NYUMBA ZA BEI NAFUU.
Tunawasiliana na mashirika yanayojenga nyumba na kuwapatia wanachama wetu fursa za nyumba za bei nafuu kwa ajili ya kutoa huduma hiyo.hata hivyo ahadiway itaanza kujenga nyumba kwa ajili ya wanachama wake tuu ili kuhakikisha kwamba kila mwanachama anapata nafasi ya kuishi katika nyumba bora.
HISA ZA
AHADIWAY.
Hisa ni
akiba au amana ambayo mwanachama atawekeza Ahadiway ili kumuwezesha
kuaminika na kumjengea mazingira mazuri
ya kukopesheka.
UNUNUAJI WA HISA.
Wanakikundi
wanahimizwa kukutana mara kwa mara kwa lengo la kununua hisa zao ambazo kima
cha chini ni sh 2000 na kiwango cha juu hutegemea na mwanachama mwenyewe jinsi
alivyodhamiria kupambana na umaskini. Hisa zinaweza kununuliwa mara moja kwa
wiki, mara mbili kwa mwezi au mara moja kwa mwezi kutegemeana na ratiba ya
wanakikundi wenyewe. Hisa zote zitawekwa benki kwenye akaunti ya Ahadiway Hisa
Account
FAIDA
ZITOKANAZO NA HISA.
Hisa yako
itakusaidia kupata mkopo wa fedha taslim ambao ni mara mbili ya hisa zako.
Kila baada
ya mwaka mmoja baada ya kununua hisa utapata gawiwo au faida ya asilimia
ishirini ya hisa zako au thamani ya kiwango cha faida iliyo patikana.
Pamoja na
hayo hisa itakuwezesha kuaminika na Ahadiway katika kutafutiwa fedha za miradi unayotaka kuifanya.
MATARAJIO
YETU.
· Wanachama wote wa Ahadiway wanatimiza
ndoto zao
· Kufikia mwisho wa mwaka kila kikundi
kiwe kimeshapata mradi mkubwa wa pamoja
· Wanachama wote tutakuwa tumepunguza
umaskini kwa kiwango kikubwa
· Wanachama wote tutakuwa na furaha na
amani tele.
Tunahitaji kila mtanzania apate nafasi ya kufanya kazi kwa hali yoyote na kwa kiwango chochote.
tunatoa mafunzo ya aina mbalimbali ili kuhakikisha walengwa wanapata huduma na fursa zote wanazoweza kuzifikia kwa uwezo wao au kwa msaada kutoka ahadiway.
akiba yako maendeleo yako.
Tunahitaji kila mtanzania apate nafasi ya kufanya kazi kwa hali yoyote na kwa kiwango chochote.
tunatoa mafunzo ya aina mbalimbali ili kuhakikisha walengwa wanapata huduma na fursa zote wanazoweza kuzifikia kwa uwezo wao au kwa msaada kutoka ahadiway.
akiba yako maendeleo yako.
No comments:
Post a Comment